Napendekeza: Iwe ni lazima kutembelea Chato National Park

Napendekeza: Iwe ni lazima kutembelea Chato National Park

Tena pesa za malipo wakatwe kwenye mishahara yao, ikifika mwisho wa mwaka lazima wote waende kuangalia twiga waliopelekwa kwenye mbuga wakiwa wamevalishwa mizula.
 
Tanzania aisee Kuna watu mna mawazo , yani iwe lazima KWA pesa za mfanyakazi au KWA kulipwa na serikali
 
Katika hali ya kumuunga mkono mh Rais na jitihada zake za maendeleo nashauri iwe ni lazima kwa wafanyakazi wa serikali angalau kwa mwaka mara moja wawe wanatembelea Burigi- Chato National Park ili kuhamasishana ktk Utalii wa ndani...
Huko wataenda ndgu zako
 
Nakazia:

Ng'ara chattle ng'ara aaaa! Ng'ara magufuli ng'ara aaaa!
 
CCM hua wanaanza mambo kimasihara hivihivi kumbe wanapima upepo. Ukute mleta mada katumwa mana ccm sio wa kuwaamini kirahisi kumbuka hata mjadala wa term limit kwa rais ulianza kimasihara angalia leo ulipo...
 
Katika hali ya kumuunga mkono mh Rais na jitihada zake za maendeleo nashauri iwe ni lazima kwa wafanyakazi wa Serikali angalau kwa mwaka mara moja wawe wanatembelea Burigi - Chato National Park ili kuhamasishana katika Utalii wa ndani.

Pia na shule za sekondary nazo kwa mwaka ziwe zinatembelea Chato kuangalia wanyama na shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Katika eneo hili na chimbuko la uchapaji kazi wa Rais.

Katika watalii wanaokuja Tanzania kwenye package yao Visiting Chato iwe ni Must. Hiii itakuza sana mbuga hii ya kupendeza ambayo naamini muda si mrefu itaingia kwenye maajabu 7 ya Dunia kwa kuwa mbuga inayokua kwa kasi sana Duniani.

Watanzania tujifunze kupenda vya kwetu. Pia wafanyakazi wa Serikalini wapewe mikopo ya kujenga nyumba Chato ili yale mataa yawe serious yakifanya kazi kutokana na uwepo wa watu wengi na kuongeza shughuli za kiuchumi. Na pia Ijengwe Ikulu kwa Kanda ya ziwa.

Na pia wale wanaopiga piga kelele Chato kujengeka nawauliza kwani Chato ipo nchi gani? Nashauri hata ule mradi wa Bandari ya Bagamoyo ungehamishiwa Chato ili kuinua uchumi wa Kanda ya Ziwa.

Nawasilisha.

Namba yangu ya simu 078778371
Naunga mkono
 
Back
Top Bottom