Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Si mara moja wala mara mbili au mara 3 ambapo jeshi la polisi limeua raia wakiwa wanashikiliwa, yaani wakiwa mikononi mwao, tena mara kadhaa raia hao wakijulikana ni raia wema. Na haya hayajaanza leo bali ni miaka mingi, na yanaendelea hadi leo.
Tuna kumbukumbu mbaya ya siku za nyuma, jeshi la polisi kufanya mauaji ya wafanyabiashara wa madini baada ya kuwapora pesa zao.
Tuna kumbukumbu mbaya ya miaka ya karibuni ya polisi kumwua mfanyabiashara kule Mtwara na kisha kumpora pesa yake.
Tuna taarifa mpya ya polisi kumwua mdogo wake Boniface.
Tuna kumbukumbu ya ushenzi wa jeshi la polisi kumwua Mwangosi akiwa anatekeleza wajibu wake halali kisheria.
Tunatakiwa tujiulize, hili kweli ni jeshi la polisi au kundi la majambazi linalofanya uovu wake kwa kutumia ofisi za Serikali?
Kama kuna majambazi yamejiingiza na kujazana ndani ya Jeshi la polisi, halafu tumeshindwa kuyatambua na kuyafukuza yakaisha, kisha jeshi la polisi likabakia kuwa kweli ni jeshi la polisi badala ya kuwa maharamia, basi ni vema tuanze kulitengeneza jeshi la polisi jipya, kisha kulifuta hili tulilo nalo.
Yaani tukishajenga jeshi jipya la Polisi, hawa wa sasa, wote wafutwe kazi na kuomba upya, huku maombi yao yakipitia assessment ya hali ya juu. La sivyo tutaendelea kushuhudia mauaji ya raia wasio na hatia yakifanywa na jeshi la polisi.
Polisi wanatakiwa kuwa kimbilio la ulinzi na siyo chanzo cha maanagamizi ya uhai wa watu wasio na hatia.
Tukatae katakata vitendo vya kiharamia vinavyofanywa na polisi. Tuikatae katakata CCM inayoshindwa kuthamini uhai wa Watanzania kiasi cha kuvifanya vyombo vya dola kuwaua raia pale wanapojisikia kuufanya uovu huo.