Napendekeza kufutwa kwa somo la ‘Slavery’ kwenye mitaala ya ufundishaji historia nchini

Binti yangu Fransica, ndio maana nimekuambia karudie Form IV ufute hiyo Zero uliyopata.
TOPIC = MADA
Kama unai- ‘soma’ hiyo mada darasani, basi ni somo, ndio maana unasom. ‘Somo la leo - Slavery’
 
Wewe umechanganyikiwa, kama ni ili wao watuonee huruma, then fine, wafundishane wenyewe kwa wenyewe hukoooooooo..., huku kwetu hakuna kufundisha mtoto huo utopolo, unatunyongesha sana kifikra, Frankly, hakuna wa kukuonea huruma, wali-replace ‘Slavery’ wakaleta ‘Colonialism’, na sasa ‘capitalism’, yote ni unyonywaji mtupu!!!! WaAfrika tusitafute kuonewa huruma, maana hakuna wa kutuhurumi, tujinasue wenyewe Kifikra!!, Futa hilo somo!!!!

Ni sisi pekee Wafrika tunaotegemea Wazungu, Waarabu kwenye historia zetu, maisha yetu kwa kiwango kikubwa.

Ingawaje tuna watafiti wengi wamefanya kazi kubwa sana.
 
Kwamba Marekani kuna watu weupe inamaanisha wao ndio walikuwa hapo toka awali? Kisa Red indians hawaonekami tena basi inamaana hawakuwepo? Tafuta ukweli ndugu yangu, based on evidence, na sio story za kutunga
Hawa weupe wa sasa walioko Misri wametoka wapi?
 
Pendekezo hilo nalitoa kwa sababu kuu tatu.

1.) Kitendo tu cha mimi kujua kwamba mzungu aliweza kuwakamata mababu zangu na kuwauza kama mbuzi kilinifanya nijione binadamu wa daraja la pili hapa duniani, inauma sana ila ukweli ndio huo; kwamba mzungu ni daraja la kwanza, ila sisi daraja la pili kama si la mwisho, naapa, kama nisingefundishwa haya, nisingeweza kupata mawazo hayo kamwe! Japo sasa nimekua na sina hata mawazo hayo, ila chini kwa chini kuna kitu nimeshaharibiwa na somo hilo.

2.) Si kila ukweli katika historia wenzetu huwafundisha watoto wao, huwa wanachagua, ikiwezekana hata kuedit historia ili kuwalinda kisaikolojia. Mfano wale Archeologists wa Kizungu walipogundua kwamba Mapharaoh wa Misri walikuwa ni watu weusi, na waliweza kuwafanya watumwa watu weupe (wayahudi) , walibadilisha na kupindisha ukweli, hata movie zao, mapharaoh wote wanaonyeshwa kwamba ni weupe, wakati michoro yote kwenye kuta za pyramid zimaonyesha vinginevyo..., mifano ni mingi mno!

3.) Hii ya sababu ya tatu ndio inaniumiza sana, sitaki hata kuitaja.., au basi siitaji
Hii ni sawa na yale makumbusho ya kibali Rwanda (Genocide memorials)naona yangefungwa make nahisi yanaongeza chuki ambayo unakuta mtoto amezaliwa leo halafu miaka 10 unaanza kumuelezea jinsi chuki ilivoanza huku akishuhudia mifupa,majeneza ya miaka 1994,Mimi niliona lakini sikupendezwa kabisa,halafu kibaya maelezo yanayotolewa hapo yanaelezea zaidi upande mmoja ulioathirika zaidi wanalishana sumu
 
Muafrika hakua na hakumtambua mungu hadi wageni walipokuja.............bulushit......historia yetu kabla ya hawa wageni kuja ni kama hakuna kitu tunachoambiwa ni kama maisha yetu yalianza walipoanza kuja hawa wageni

Huu ni uongo tuririokaririshwa. Concepts za maana za Mungu, culture, science zimetokea Afrika.

Ndio maana ni rasihi kutenganishwa kidini, kikanda, kikabila. Wazungu, wachina, Waarabu, Wahindi wenyewe wanafundishana ni watu wamoja.
 
Kuna kiongozi mmoja wa Tanzania alipata kusema tufundishwe historia yetu, hakika alinena jambo jema sana, na ilipaswa kitachofuata ni kufadhili kazi za uandikwaji wa hii historia na wataalamu wa ndani na hatimae kuingizwa rasmi kwenye mitaala mbalimbali ya taaluma.

Historia yetu ni suala muhimu sana, vitu vingi vinafichwa fichwa na hata vile vingi vilivyopo viliandikwa na wazungu katika mitazamo yao, kuna wanahistoria wengi wa kiafrika lakini wengi machapisho yao yana ukakasi mkubwa na yameelemea katika pande zenye interest zao mf Mohammed Said et al. Sikatai suala la kuandika historia linategemea na mwanahistoria anapenda kugusa upande gani lakini ni muhimu zaidi wanahistoria hawa wakigusa maeneo mbalimbali na kutuachia urithi ambao utatufanya tujitambue.

Masuala kama biashara ya utumwa, ukoloni, uenezwaji wa kidini, kukua kwa nchi yetu n.k ulipaswa uangaziwe kihistoria kwa undani kabisa ili tufahamu tulitoka wapi na tunaenda wapi bila kuficha manyanyaso, ukatili, dhuluma, na hata faida zilizopatikan iwe kutoka kwa wageni dhidi yetu na yao, au sisi kwa sisi wenyewe.

Hii itatufundisha kujithamini na kujitegemea wenyewe pasipo na kutegemea na kujipendekeza kinafiki kwa watu ambao tumewageuza “miungu watu"
 
Hawa weupe wa sasa walioko Misri wametoka wapi?

Mashariki ya kati.

Unajua Afrika inaweza kuwa na watu wengi weupe, Wachina, Waarabu, wahindi kuliko Waafrika ndani ya miaka 200 tu?

Utauliza wametoka wapi? Jiulize mikopo yote muhimu,sekta zotemuhimu technologia, vyombo muhimu vya dunia nani anavi- control.
 
Pendekezo hilo nalitoa kwa sababu kuu tatu.

1.) Kitendo tu cha mimi kujua kwamba mzungu aliweza kuwakamata mababu zangu na kuwauza kama mbuzi kilinifanya nijione binadamu wa daraja la pili hapa duniani, inauma sana ila ukweli ndio huo; kwamba mzungu ni daraja la kwanza, ila sisi daraja la pili kama si la mwisho, naapa, kama nisingefundishwa haya, nisingeweza kupata mawazo hayo kamwe! Japo sasa nimekua na sina hata mawazo hayo, ila chini kwa chini kuna kitu nimeshaharibiwa na somo hilo.

2.) Si kila ukweli katika historia wenzetu huwafundisha watoto wao, huwa wanachagua, ikiwezekana hata kuedit historia ili kuwalinda kisaikolojia. Mfano wale Archeologists wa Kizungu walipogundua kwamba Mapharaoh wa Misri walikuwa ni watu weusi, na waliweza kuwafanya watumwa watu weupe (wayahudi) , walibadilisha na kupindisha ukweli, hata movie zao, mapharaoh wote wanaonyeshwa kwamba ni weupe, wakati michoro yote kwenye kuta za pyramid zimaonyesha vinginevyo..., mifano ni mingi mno!

3.) Hii ya sababu ya tatu ndio inaniumiza sana, sitaki hata kuitaja.., au basi siitaji

Haya mambo ya utumwa inabidi yawe footnotes, kujisomea zaidi badala ya kuwa ndio main topics.

Kutufundisha tusijikwae tena.

China Wametawaliwa Wamongolia, Wazungu. Japan, India, Korea, Middle east wote wametawaliwa.

Hawajaifanya historia waliopewa na watawala wao kuwa historia yao kuu.

Walichukua mazuri (technology, systems) vitu vitavyowasaidia lakini wakaundeleza na kuupigania utamaduni wao.
 
History, Historia inatokana na neno mawili His and story. Story hadithi za mtu, maisha yake tangu alipoanza kuwepo duniani.

The short version is that the term history has evolved from an ancient Greek verb that means “to know,” says the Oxford English Dictionary's Philip Durkin. The Greek word historia originally meant inquiry, the act of seeking knowledge, wisdom and knowledge that results from inquiry.

Inabidi kujiuza, tujiulize kutafakari kwa undani mambo muhimu kama haya. Huwezi kumwambia Mchina Mjapan, Mkorea, Mrusi historia imeanxa na utumwa.

TIME Homepage › History › language.

1651224701863.png
 
Huwa nachoka sana nikisikia Mlima fulani ulizinduliwa na Mzungu...

Africa tuna vituko sana.
 
Mashariki ya kati.

Unajua Afrika inaweza kuwa na watu wengi weupe, Wachina, Waarabu, wahindi kuliko Waafrika ndani ya miaka 200 tu?

Utauliza wametoka wapi? Jiulize mikopo yote muhimu,sekta zotemuhimu technologia, vyombo muhimu vya dunia nani anavi- control.
Aisee ni kweli, tusipoangalia Afrika litakuja kuwa bara la watu weupe, weusi tutabaki kama digi digi tu humu
 
Huwa nachoka sana nikisikia Mlima fulani ulizinduliwa na Mzungu...

Africa tuna vituko sana.
Yaaani vitu vingine vinachekesha sana, na unakuta eti huo ndio mtaala na watoto mamilioni kwa mamilioni tunawalipia ada ili wafundishwe huo upupu?!
 
Aisee ni kweli, tusipoangalia Afrika litakuja kuwa bara la watu weupe, weusi tutabaki kama digi digi tu humu

Angalia trends, wafanyabiashara wote wakubwa TZ, Angalia Angola, Zambia, DRC mnufaika, Kenya, South Afrika, Namibia mnufaika mkubwa wa rasilimali za nchi ni nani?

Mikopo yetu tunaitoa wapi , sisi ndio ilibidi tuwe wakopeshaji wakubwa kama waarabu. Wanaokukopesha ndio wenye nguvu kukwambia ufanye nini? Wachukue nini mbadala kama ardhi, rasilimali.

Ila sasa angalia sera zetu za kutembeza bakuli. Kutojiamini, hatuna sera za kuwasaidia wengi. Matokea yako wazi.

Wachache wanufaikaji,wanajipigia debe, wengi vijijini, mtaani hawana milo mitatu? Situation kama hii ikiendelea hata kwa miaka 20/ 50/ 100 tutakuwa wapi?
 
Ndio maana hata Loliondo iliuzwa, mikopo imezidi!!
 
Kwani mkuu si hata marekani ilitawaliwa na sasa iko huru na na ni tajiri.

China pia si ilitawaliwa, wao wana hadi movies zinazoelezea ukatilia waliofanyiwa na wajapan lakini bado wanajifunza na wanaendelea pia.

Tatizo letu watz tunapenda kumtafuta wa kumtupia lawama.
 
Tatizo ni of course kuna mtu wakumtupia lawana. Ila hizo lawama haziwezi kukusaidia kuendelea.

Muhimu kuwa na mikakati,mipango.
 
Pendekezo hilo nalitoa kwa sababu kuu tatu.

1.) Kitendo tu cha mimi kujua kwamba mzungu aliweza kuwakamata mababu zangu na kuwauza kama mbuzi kilinifanya nijione binadamu wa daraja la pili hapa duniani, inauma sana ila ukweli ndio huo; kwamba mzungu ni daraja la kwanza, ila sisi daraja la pili kama si la mwisho, naapa, kama nisingefundishwa haya, nisingeweza kupata mawazo hayo kamwe! Japo sasa nimekua na sina hata mawazo hayo, ila chini kwa chini kuna kitu nimeshaharibiwa na somo hilo.

2.) Si kila ukweli katika historia wenzetu huwafundisha watoto wao, huwa wanachagua, ikiwezekana hata kuedit historia ili kuwalinda kisaikolojia. Mfano wale Archeologists wa Kizungu walipogundua kwamba Mapharaoh wa Misri walikuwa ni watu weusi, na waliweza kuwafanya watumwa watu weupe (wayahudi) , walibadilisha na kupindisha ukweli, hata movie zao, mapharaoh wote wanaonyeshwa kwamba ni weupe, wakati michoro yote kwenye kuta za pyramid zimaonyesha vinginevyo..., mifano ni mingi mno!

3.) Hii ya sababu ya tatu ndio inaniumiza sana, sitaki hata kuitaja.., au basi siitaji
Nini maana ya historia
 
Back
Top Bottom