antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Hivi ni mzungu tu?mzungu aliweza kuwakamata mababu zangu na kuwauza kama mbuzi kilinifanya nijione binadamu wa daraja la pili hapa duniani, inauma sana ila ukweli ndio huo
Mbona sivyo kwa Tanganyika?
Kwani Tiptip alikuwa mzungu au mwarabu?
Maana inajulikana, Tiptip na Waarabu wenzake wakiwa na magobole, walikuwa wanawinda na kukamata wenyeji kama digidigi kule Kigoma, Tabora, Dodoma, nk na kuwafunga minyororo, kuwapeleka hadi Bagamoyo, na kuwavusha hadi Zanzibar kwenye mnada wa watumwa.
Huko mnadani, walikuwa wakiuzia waarabu wenzao kwa ajili ya kusafirisha kwenda kuuza Uarabuni na Ulaya!
Yawezekana kwingineko Afrika mchakato ulikuwa tofauti