Napendekeza kuondolewa sifuri mbili kwenye sarafu na noti zote za Tanganyika

watanganyika mko wangap 🐒

kwa waTz hakuna haja na mapendekezo ya watanganyika 🐒
 
Zanzibar watalia sana na kukuchapa hadharani.
 
Napendekeza hili pia, inachosha balaa kuhesabu pesa, unahesabu pesa nyingiii ila zina thamani ndogo
 
Hayo mabegi ya pesa ya wapi mkuu. Siku hizi digital transaction ina take over. Hatutembei na hela, labda kwenda kwenye maduka ya Mangi tu kununua viberiti na sukari.
Maduka mengine ya Mangi yana lipa namba ujue
 
Zanzibar nao watatuiga... Hukumbuki walikuwa na elimu ya primary inayoishia darasa la sita wakaamua kubadili iendane na siye kuishia la sita. Sasa na sisi tumebadili kuwa darasa la sita. Sasa sijui itakuwaje
 
Mkuu hata namba zote zingetolewa hakuna kitakacho badilika ndani ya nchi hii matizo la nchi hii sio masufuri kwenye noti bali ni ufisadi ulio kithiri unao lelewa na kufungwa na ccm.
 
Suala la valuation itakuwaje mkuu?

Maana yangu ni kwamba mi nilinunua kwa laki ama nina amana yangu ya laki sehemu, kwa hiyo leo nilipwe buku, itamake sense kweli?

Emb naomba uniweke sawa.
 
W
Aisee, walifanikiwa?
Walifanikiwa pia hata msumbiji walitumia mbinu hii ila nenda mpakani mwa nchi hizo, wananchi wake hawataki kutumia hizo hela ingawa zinaonekana zina thamani kubwa ila uwezo wa kununua ni mdogo kwenye manunuzi.
Wachumi wanaweza elezea vizuri.
NB; Kumbuka hata mishahara kwa wanao pata itapunguzwa hizo sifuri mbili mfano unapata 1,800,000 utapata 180,000
 
Suala la valuation itakuwaje mkuu?

Maana yangu ni kwamba mi nilinunua kwa laki ama nina amana yangu ya laki sehemu, kwa hiyo leo nilipwe buku, itamake sense kweli?

Emb naomba uniweke sawa.
Kuna tatizo gani ukalipwa buku yenye uwezo wa kununua bidhaa zenye thamani ile ile ya laki moja? Maana mwenue laki moja benki akiangalii salio atakuta sifuri mbili hakuna, lakini nguvyu ya pesa yake ni ile ile sawa na laki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…