Napendekeza kuondolewa sifuri mbili kwenye sarafu na noti zote za Tanganyika

Napendekeza kuondolewa sifuri mbili kwenye sarafu na noti zote za Tanganyika

Nchi ya Zanzibar wataamua wenyewe cha kufanya, ila upande wa Tanganyika, napendekeza ziondolewe sifuri mbili kwenye sarafu zake zote.
Kwa mantiki hiyo:-

1.) Tsh. 100/= itakuwa Tsh. 1/=
2.) Tsh. 200/= itakuwa Tsh. 2/=
3.) Tsh. 500/= itakuwa Tsh. 5/=
4.) Tsh. 1,000/= itakuwa Tsh. 10/=
5.) Tsh. 2,000/= itakuwa Tsh. 20/=
6.) Tsh. 5,000/= itakuwa Tsh. 50/=
7.) Tsh. 10,000/= itakuwa Tsh. 100/=

Halafu sasa, ichapishwe noti ya 1,000/= ambayo ndio sawa na laki 1. Kwahiyo ukiwa nazo 10 tu ni milioni tayari, ukiwa nazo mia ambazo ndio ujazo wa kibunda cha milioni moja ya sasa, ni milioni 10 tayari. Kwahiyo mtu ukiwa na vibumda vyako viwili tu, unaweza kuweka mfukoni ukaenda kununua Harrier used kwa mtu.

Hii itasaidia kupunguza uzito wa mabegi ya pesa.

==========================


View: https://youtu.be/3DfGfrUAbyo?si=1EIfC2Nmk0QClGDP

Nami ninapendekeza UV CCM na watoto wa mawaziri na wabunge wapewe hiyo kazi ya kuzikusanya hela zote na kuzifuta sufuri mbili.
 
Unataka iwe kama Zambia nao walitoa sifuri ila bidhaa zinaninuliwa kwa bei ile ile kwa mtu alie mbali atajua hela yao ina thamani kumbe wapi...
 
Ngoja ncheke....saiv tu nikidondosha jero natamani kupiga yowe siku nzima, afu ndo nna noti kumi tu eti milioni...nikidondosha moja tu kwisha habari.....🍸🍸🍸
kwa nini udondoshe? Na wala siyo ajabu kuwa na noti za thamani ndogo.

Ngoja nikueleze. Mimi nilianza kazi nimemaliza Form six mshahara ulikuwa Shilingi 760, noti ya juu kabisa ilikuwa shilingi mia (tena zilikuwa chache).

Mbona tulihifadhi fedha vizuri tu na hupotezi hata senti tano.
 
Wazo zuri kabisa, na wenzetu Zambia walifanikiwa. Kumbuka Zambia Ulifika wakati kwacha 1000, haizidi thamani ya Shilling 1 ya Tanzania. Wakaona isiwe tabu, bora nusu hasara.

Ila wazolako litapata wapinzani wengi maana unataka kumpunguza idadi ya mamilionea.
Hata Mozambique nilikwenda nadhani ilikuwa mwaka 2007 walikuwa wamebadilisha fedha na kuondoa sifuri tatu. Walikuwa na Old metical na new metical ambayo haikuwa na sifuri tatu na ndiyo zile za zamani zilikuwa zinaondolewa kila zikifika benki hazitoki tena.
 
Kuna tatizo gani ukalipwa buku yenye uwezo wa kununua bidhaa zenye thamani ile ile ya laki moja? Maana mwenue laki moja benki akiangalii salio atakuta sifuri mbili hakuna, lakini nguvyu ya pesa yake ni ile ile sawa na laki.
Kwa nchi yetu ilivyo shaghalabhaghala katika kusimamia bei za bidhaa katika soko la walaji, yaweza kuwa ni chanzo kingine kwa wafanya biashara wasio waaminifu kunufaika zaidi kuliko walala hoi.
 
Wachapishe noti ya 50,000 na 100,000
Ukiwa na noti ya laki moja mfukoni, unakwenda kwa mamalishe unakula chakula cha elfu2 unatoa noti yako hana chenji, unaondoka nayo hadi kwa sheli bubu unatiliwa mafuta lita2 unachomoa noti yako hana chenji, unafika baa ya uswahilini unakunywa bia2 hana chenji, unaondoka. Hadi jioni unakuwa umeshapata huduma zote za msingi bila kulipa, endapo utakuwa umenusurika kupigwa na wababe Kama makonda wa daladala.
 
Sijaelewa, dadavua..
OK Zambia sasa hivi wana 50 kwatcha,100 kwatcha na 10 Kwatcha hizo mwanzo zilikua 100,000 Kwatcha wakatoa sifuri tatu na kubaki na sifuri mbili tu ila thamani yake ipo vile vile baada ya kuitamka laki moja wanatamka mia ila bei ya kitu cha laki moja kipo ndani ya 100 kwatcha ndio maana nikasema wametoa sifuri ila thamani ya fedha kwa ununuzi wa bidhaa upo vile vile au umeshuka zaidi..
 
OK Zambia sasa hivi wana 50 kwatcha,100 kwatcha na 10 Kwatcha hizo mwanzo zilikua 100,000 Kwatcha wakatoa sifuri tatu na kubaki na sifuri mbili tu ila thamani yake ipo vile vile baada ya kuitamka laki moja wanatamka mia ila bei ya kitu cha laki moja kipo ndani ya 100 kwatcha ndio maana nikasema wametoa sifuri ila thamani ya fedha kwa ununuzi wa bidhaa upo vile vile au umeshuka zaidi..
So what? Jadili hoja yangu mimi
 
Naomba ufafanuzi vizuri, unaposema nguvu ya kununua bidhaa unamaanisha nini, kwani Zambia wananunua bidhaa kwa kutumia fedha ya wapi.
 
Back
Top Bottom