Napendekeza Makonda apewe sasa Ukatibu mkuu wa Simba sc

Napendekeza Makonda apewe sasa Ukatibu mkuu wa Simba sc

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Nafasi ya 'katibu mkuu' yaani Afisa mtendaji mkuu (CEO) wa Simba kwa sasa iko wazi mara baada ya aliyekuwepo awali kujiuzuru ghafla.

Huu ndio wakati muafaka wa Simba sc kumpa hiyo nafasi Paul Makonda ambaye kwa sasa hana kazi rasmi mara baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya ukuu wa mkoa wa Dar.

Kwa kifupi sana, Paul Makonda anazo sifa kadhaa ambazo huenda zikawa zinakidhi kuweza kupewa hiyo nafasi, ukizingatia ni mpenzi mkubwa wa Simba, msomi wa chuo kikuu (hata kama cheti chake cha kidato cha nne kina utata mkubwa sana, na uwezo wake chuoni unadaiwa ulikuwa chini), mbunifu na mwenye uthubutu.

Yote kwa yote huenda kwa sasa Makonda ameweza kujifunza namna ya kuongoza watu na kuheshimu watu wengine, baada ya kuonyeshwa cha mtema kuni na wajumbe wa CCM Kigamboni.
 
Napendekeza Makonda apewe sasa Ukatibu mkuu wa Simba sc.
Kwa kweli kuna utani mwingine mbaya sana. Hili la kuwasukumizia washamba na limbukeni madaraka yanayowazidi kimo ni kitendo cha busara kweli? Kama Simba imewahi kutukanwa na kukejeliwa, sidhani kama imewahi kufikia kiwango hiki.

Labda kama anasukumiziwa ubaunsa huko kwa watani! Huko ni ruhusa tu kwani hata akiokotwa wapi, twende tu. Ni kama kokoro, linazoa tu na yote poa tu. Jamani, baada ya Oktoba, taifa jipya likizaliwa hizi takataka za kuokoteza marufuku!
 
Ndugu mtangazaji uwe na adabu

huko unyamani wajumbe hawamtaki...hawafugi mbwa asiebweka
 
Hebu usiniudhi Mimi mpenzi wa SIMBA toka Enzi za Sunderland hatujawahi kufanya kosa Kama Hilo kwenye uongozi
 
Huyu ceo alipatikana baada ya nafasi kutangazwa na watu wenye vigezo wakaomba kama unampenda makonda kaolewe naye
 
Nafasi ya 'katibu mkuu' yaani Afisa mtendaji mkuu (CEO) wa Simba kwa sasa iko wazi mara baada ya aliyekuwepo awali kujiuzuru ghafla.

Huu ndio wakati muafaka wa Simba sc kumpa hiyo nafasi Paul Makonda ambaye kwa sasa hana kazi rasmi mara baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya ukuu wa mkoa wa Dar.

Kwa kifupi sana, Paul Makonda anazo sifa kadhaa ambazo huenda zikawa zinakidhi kuweza kupewa hiyo nafasi, ukizingatia ni mpenzi mkubwa wa Simba, msomi wa chuo kikuu (hata kama cheti chake cha kidato cha nne kina utata mkubwa sana, na uwezo wake chuoni unadaiwa ulikuwa chini), mbunifu na mwenye uthubutu.

Yote kwa yote huenda kwa sasa Makonda ameweza kujifunza namna ya kuongoza watu na kuheshimu watu wengine, baada ya kuonyeshwa cha mtema kuni na wajumbe wa CCM Kigamboni.
Simba hatuna katibu mkuu, Yanga huko ndo kuna katibu mkuu
 
C.E.O. Na Katibu mkuu ni nafasi mbili tofauti .....Senzo hakuwa Katibu mkuu.
 
Back
Top Bottom