Napendekeza matumizi ya taxify na Uber kwenye kutuma na kupokea pesa; Je, inawezekana?

Napendekeza matumizi ya taxify na Uber kwenye kutuma na kupokea pesa; Je, inawezekana?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Unaweka pesa kwenye bahasha, kisha unatumia application ya Taxify / Uber na kuita chombo cha usafiri kilichokaribu, kisha unamkabidhi mzigo ila humwambii kuna nini ndani na kumpa maelekezo ya wapi apeleke.

Je, hii inawezakana?
 
Labda wewe binafsi ubuni kampuni ya kutuma na kupokea parcel hata kwa pk pk uajiri vijana waaminifu
 
Haina maana kwa sababu:
  • Utaingia gharama kwenye muda + pesa ya kuupeleka mzigo.
  • Kuna uwezekano mkubwa sana kuipoteza hiyo hela(risk ipo juu sana)
  • Kutuma kwenda nje ya mkoa haitowezekana.
 
Haina maana kwa sababu:
  • Utaingia gharama kwenye muda + pesa ya kuupeleka mzigo.
  • Kuna uwezekano mkubwa sana kuipoteza hiyo hela(risk ipo juu sana)
  • Kutuma kwenda nje ya mkoa haitowezekana.
Kwahiyo tukubali tu kulawitiwa mchana kweupe kwenye kodi za miamala ya simu?
 
Naona tunarudi enzi za kutuma pesa kupitia postal money order.
 
Kwakweli, haina namna...
Nimetizama gharama za kutuma na kutoa pesa safaricom Kenya kwa madhumuni ya kulinganisha na gharama za vodacom.
Gharama za kutuma na kupokea pesa Tanzania na Kenya(kiwango Tsh 50000 sawa na ksh 2300)
kampuni kutuma kutoa jumla
Vodacom 4370 (unregistred) + 2700 = Tsh 7070
Safaricom 74(unregistered) + 32 = ksh102 sawa na Tsh 2300.

Ni dhahiri kutuma na kupokea kiwango kilekile cha pesa mtanzania analipa takriban mara tatu zaidi kuliko Mkenya.
Tusitafute mchawi ,"manyan'gau" tunakula na kulala nao.
 
Back
Top Bottom