huduma ya prepaid ni nzuri kwa mteja asiye mwaminifu na mara nyingi inafaa kwa wateja wasumbufu kama mimi ambaye huwa nalipa ninapokaribila ceiling ndo nalipa kama nusu kisha maisha yanaendelea.
ni utaratibu mzuri kabisa kulipa huduma baada ya kutumia kwangu hata kodi ya nyumba huwa namlipa mwenye nyumba baada ya kutumia angalau mwezi mmoja.
ninyi unaopenda kulipa mapema kabla ya kutumia ni wale umliozoea boom likitoka mnalipa kabisa chakula na pia unalipa shuttle kabisa huu ni utaratibu mbaya na si mzuri katika maisha serikali yenyewe inawakopa wazabuni na pia wafanyakazi unafanyakazi kisha unalipwa baadaye sasa iweje wewe unayefanya kazi kuanzia tarehe moja na unalipwa tarehe 30 uwe na uwezo wa kulipa hela tarehe 30 huu ni wizi 🤣 🤣 🤣 !
ukiona kuna huduma ambayo unawaweza kuipata kwa kukopa bila riba wala ziada sio ya kuiachia itumie fursa vizuri acha uzembe na woga🤣🤣🤣 kila siku fedha ina thamani tofauti na fursa tofauti laizma uzingatie hilo mfano kwa mwezi uliopita mafuta yalikuwa labda 2500 kwa lita na kwa mwezi mzima ulihitaji shilingi 100,000/- kununua mafuta lita 40. kununua lita hizo mwezi huu unahitaji 128,000/- kwa nini ujipe tabu!
na wakati huo unajipendekeza kulipa bili 100,000 in advance wakati aliyetumia kwanza kiasi hicho hicho kapunguza deni kwa 30,000/- maji hajakatiwa na anaendelea kutumia maji huku akiendesha gari mwisho wa mwezi inakuja bili nyingi ya 100,000/- na ile inakuwa jumla170,000/- anapunguza tena 50,000/- na maisha yakienda🤣🤣🤣.
nyie vipi maisha mjini hesabu ala! hao watoto wakisure tu hawapendi kulipia huduma kabla ya kutumia.
hizo bia tu tunakunywa kwanza na tunalewa baadaye kisha ndo tunalipa itakuwa maji nyie vipi?