DOKEZO Napendekeza meter za maji zifungwe mifumo ya ‘LUKU’

DOKEZO Napendekeza meter za maji zifungwe mifumo ya ‘LUKU’

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mfumo huo ukianza ni noma tupu,

Kuna watu watawalaza wenzao bila kuoga.

Maana nyumba za wengi zina Mambo sn.
 
Mamlaka za maji zinatumia gharama kubwa sana kukusanya biki za maji toka kwa wateja wa maji ambao hawalipii hadi wakatiwe.

Hapa naona Dawa ni ‘Lipia maji kadri unavyotumia’. Zifungwe meter za kielectronic ambazo zitakuwa zinatumia umeme kujiendesha, na kwa sehemu ambazo hazina umeme, nasi meter iambatane na kisolar panel kidogo cha kuchaji betri itakayokuwa ndani kwa ndani.

Kazi ya mamlaka za maji itakuwa ni kuzikagua mara moja moja kwa kushtukiza iki kubaini zile meter ambazo zimechezewa.

Nakaribisha maoni
Usinifanye unapendekeza wakati mamlaka ilikwisha amua kubadilisha mita.
Ninatabiri utaandika Post kuhusu mita za maji.
 
Usinifanye unapendekeza wakati mamlaka ilikwisha amua kubadilisha mita.
Ninatabiri utaandika Post kuhusu mita za maji.
Mimi sikuwahi kuziona hizo meter wala kusikia kama zipo au zimeanza kufungwa, ndio maana nikasema napendekeza..
 
Hivi inakuaje,mimi niliungiwa meter toka mwaka,ila hawajawahi kunitembelea kabisa..yani sijawahi kulipa bill,kwamba mda bado au wao wenyewe kuna makosa?
 
Hivi inakuaje,mimi niliungiwa meter toka mwaka,ila hawajawahi kunitembelea kabisa..yani sijawahi kulipa bill,kwamba mda bado au wao wenyewe kuna makosa?
Kuna uhaba wa watendaji wa kuja kukata maji, hivyo hizi smart meter zitasaidia sana
 
Hiyo mifumo ya meter za malipo kabla zipo
Kuna kampuni inaitwa E-water imeshafunga hizo meter kwenye mikoa ya Singida na Dodoma Vijijini na sasa HV wanaenda Tabora na Tanga .
Aisee hii system kiboko inatumia Solar na card tu . Yaani hata SAA nane usiku unachukua kasi yako unaenda kuchota maji
 
E-water prepaid system DP
IMG_20220315_133519_4.jpg
IMG_20220315_133614_5.jpg
 
Kuna uhaba wa watendaji wa kuja kukata maji, hivyo hizi smart meter zitasaidia sana
Bora ziwekwe hizo,itasaidia sana kiukweli.

Sasa mfano wakija wakikuta nimetumia matumizi makubwa ndo wananikatia?
 
Hivi inakuaje,mimi niliungiwa meter toka mwaka,ila hawajawahi kunitembelea kabisa..yani sijawahi kulipa bill,kwamba mda bado au wao wenyewe kuna makosa?
Mkuu issue inakuja pale watakapo kutembelea na kugundua kwamba kuna deni la kiasi fulani..unaweza pewa invoice ya 1,000,000 shughuli inaanzia hapo
 
Hatimae RUWASA kuanza kutekeleza wazo

Back
Top Bottom