#COVID19 Napendekeza mkoa wa Kilimanjaro uwekwe "lockdown"

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Kiukweli kama tunahitaji usalama basi mkoa wa Kilimanjaro uwekwe lock down. Hali huko ni mbaya kuliko inavyoelezwa.

Serikali kama hamtachukua tahadhari mapema msije kusema hamkuambiwa. Wageni wanoingia na kutoka kila siku ndani ya mkoa huo na kusambaa mikoa mingine ni kiama kwa wengine. Imeshakuwa hivyo kuwa Kilimanjaro ina wimbi kubwa la maambukizi ya Covid 19.

Familia moja inapoteza watu kwa zamu na naona serikali imechukulia poa watu wanapita pita tu.

Sisi tumesema!
 
Hizo familia zinazopoteza watu zamu kwa zamu ni kutokana na corona ama? ni familia ngapi zilizopoteza hao watu? Ama naww unahemshwa na mihemuko? Umejipanga kwa lock down? Uelewa wako kuhusu lock down ni kiac gan?
Achana nae huyo, kijana anaonekana haijui faida ya mkoa wa Kilimanjaro kitaifa na madhara yake endapo mkoa utawekwa lockdown.
 
Hiyo lock down iwe kwa muda gani labda manake tumeona walioweka lockdown nchi zao wametepeta?
 
Kiukweli kama tunahitaji usalama basi mkoa wa Kilimanjaro uwekwe lock down. Hali huko ni mbaya kuliko inavyoelezwa.

Serikali kama hamtachukua tahadhari mapema msije kusema hamkuambiwa. Wageni wanoingia na kutoka kila siku ndani ya mkoa huo na kusambaa mikoa mingine ni kiama kwa wengine. Imeshakuwa hivyo kuwa Kilimanjaro ina wimbi kubwa la maambukizi ya Covid 19.

Familia moja inapoteza watu kwa zamu na naona serikali imechukulia poa watu wanapita pita tu.

Sisi tumesema!
Walishangilia kifo cha Magufuli Mungu anawanyoosha
 
Wacha wapate adhabu kama ni baridi mbona Makambako,Njombe kuko poa ? Wacha wachaga waipate fresh ya shamba
Eneo hili linahitajika uchunguzi wa kisayansi kabisa kama waleta taarifa humu wanasema ukweli. Hili lifanyoke kabla ya kuchukua hatua pendekezwa kamq ni kweli.
 
Lockdown siyo ya lazima! Kinachotakiwa ni serikali kusisitiza wananchi kuzingatia taratibu zote za Afya ili kujikinga na ugonjwa huo.Kama kila mwananchi atakuwa serious kuchukua hatua zote za kujikinga madhara yanaweza yasiwe makubwa.
 
Mwezi march mwaka huu covid-19 ilimpiga vibaya sana bi mkubwa, alikuwa hoi akakata tamaa kabisa ya kuishi.

Nashukuru Mungu tulikuja kumpeleka hospitali moja akatibiwa vizuri na akapona.

Wakati huu wa wimbi la 3 tumemuelekeza abaki nyumbani tu. Hana chaguo lingine zaidi ya hilo.
 
Anaokaa nao wanabaki nyumbani?
Mwezi march mwaka huu covid-19 ilimpiga vibaya sana bi mkubwa, alikuwa hoi akakata tamaa kabisa ya kuishi.

Nashukuru Mungu tulikuja kumpeleka hospitali moja akatibiwa vizuri na akapona.

Wakati huu wa wimbi la 3 tumemuelekeza abaki nyumbani tu. Hana chaguo lingine zaidi ya hilo.
 
Bila chanjo watu wataondoka sana. Hakuna njia nyingine ya kupambana na COVID zaidi ya hiyo
 
Mwezi march mwaka huu covid-19 ilimpiga vibaya sana bi mkubwa, alikuwa hoi akakata tamaa kabisa ya kuishi.

Nashukuru Mungu tulikuja kumpeleka hospitali moja akatibiwa vizuri na akapona.

Wakati huu wa wimbi la 3 tumemuelekeza abaki nyumbani tu. Hana chaguo lingine zaidi ya hilo.
Kwahiyo bibi yako alikuwa mzurulaji sio!!??
 
Back
Top Bottom