Napendekeza rasmi jina la ufupisho la mama liwe SASHA

Napendekeza rasmi jina la ufupisho la mama liwe SASHA

Nzuri na la kijanja. Hivi Beyonce naye ni sasha?
 
Kama hatojali, napendekeza Rais wetu akubali tutumie jina lake la kwanza "Samia"....ni fupi, rahisi na zuri pia.
Tatizo wanaoongea kiinglishi watatuharibia...!! Si unakumbuka Rais wa SA alikuwa anatamka.. SAMAYA...!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Huoni kama jina Sasha ni jina jingine tena hilo na si rahisi mtu kuelewa ni kifupisho...(Sasha ni jina kama tu ilivyo Ummy, Samia n.k)
 
Natasha Obama ( Sasha Obama)!

Umejitahidi kuiga huku siyo mbaya ! Vyovyote mtakavyomuita ila Mama ni Jembe! Msihangaike sana ili la " MAMA" limeshashika!

Sasa hivi ukiwa kwenye mazungumzo serious kuhusu uongozi wa Nchi yetu halafu mtu akasema " MAMA" basi utajua tu ana maanisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Na kwa kweli kwa watu walivyoumia ktk kipindi cha Mwendazake basi hili la " MAMA" linaleta FARAJA sana!

Hata katika maisha ya kawaida ,katika shida au hatari kuu mtu huita " MAMAAAA"!
 
Rais wa South Africa alikuwa anamwita Samaiya

Hilo jina la Sasha limekaa ki new skul sn
Mtoto flani hivi mpenda mitoko,mvaa kibegi mgongoni analilegeza mikanda Hadi linagusa makalio,simu naweka kava linaning'inia kimdoli chenye manyoya laini na visandrozi vya manyoya,kiswanglish kiingi..kiufupi halifai kumwita mkuu wa nchi alafu mama mtu mzima

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Tumuite 'Ukizingua unazinguliwa'........
 
Back
Top Bottom