Napendekeza taa za mwanga barabarani na nyaya za simu zifungwe kwenye nguzo za umeme

Napendekeza taa za mwanga barabarani na nyaya za simu zifungwe kwenye nguzo za umeme

Naona ushauri umeanza kufanyiwa kazi kwenye baadhi ya mitaa jijini Dar es salaam
 
Yaani badala ya kununua milingoti ya chuma na wire kwa ajili ya kufunga zile taa za mwanga barabarani, napendekeza taa ziwe zinafungwa kwenye mistimu ya umeme iliyopo kando kando ya barabara na ziungwe kwenye umeme moja kwa moja, hii itakoa fedha nyingi mno.

Pia badala ya kusimika mistimu ya nyaya za simu napendekeza hizo nyaya za simu zifunge tu kwenye mistimu ya umeme ambayo ipo tayari hivyo kuokoa gharama kubwa sana katika usambazaji wa mawasiliano
Nguzo za Taa nesi siko zinaanguka kila siku, mtamudu kutembea giza huko barabarani? na hizo waya za simu ni zipi maana waya za simu ziliachwa zamani kabisa siku hizi ni wayaless kwenda mbele
 
Barabara ninayokaa nguzo ziko mita 10 hadi 20 kutoka barabarani unataka wafunge taa kwenye nguzo ili uwe unawanga gizani?
1623736836825.png
 
Nguzo za Taa nesi siko zinaanguka kila siku, mtamudu kutembea giza huko barabarani? na hizo waya za simu ni zipi maana waya za simu ziliachwa zamani kabisa siku hizi ni wayaless kwenda mbele
Kwamba zisipofungwa hizi taa ndio zitaacha kuanguka?
 
Update: 08/09/2021

Hatimaye, Nyaya za mawasialiano ya simu za mkongo (Fiber network) kufungwa kwenye nguzo za umeme

 
TTCL na Tanesco wameshatia saini mkataba wa kupitisha nyayabza simu kwenye nguzo za umeme
Teh teh[emoji1787][emoji1787][emoji1787]!

Sasa hao wabishi na wajuaji waliokukejeri na kukung'ong'a mbona leo hawajitokezi angalau kiungwana 'kuunga mkono hoja', au bado tu wamechutama na kuendelea kuficha aibu zao?
 
Teh teh[emoji1787][emoji1787][emoji1787]!

Sasa hao wabishi na wajuaji waliokukejeri na kukung'ong'a mbona leo hawajitokezi angalau kiungwana 'kuunga mkono hoja', au bado tu wamechutama na kuendelea kuficha aibu zao?
😂😂😂😂, mi ndio maana siku zote napenda mtu ajadili kwa hoja, ukijadili kwa vijembe haujengi bali unaharibu mjadala. Biguo kwa Tanesco na TTCL, maana wataboresha mno mawasiliano kwa gharama ndogo sana ukikinganisha kama wangelazimika kuchimba mitaro mipya au kusimika nguzo upya nchi mzima.. 👏👏👏
 
Kuhusu taa kufungwa kwenye nyaya za umeme sina pingamizi lakini nyaya za simu kidogo kuna shida kidogo.
Hujasema nguzo za umeme za msongo mkubwa(high tension) au msongo mdogo.
Kuna kanuni inaitwa kanuni ya kiganja cha kulia cha mkono ya Jean Ampere'.(Ampere's hand right rule).Kanuni inasema ukikamata waya wa umeme(grip) welekeo wa dole gumba ni welekeo wa umeme na welekeo wa vidole vingine vilivyobaki ni welekeo wa mawimbi sumaku(electromagnetic fields) kwa welekeo wa kinyume saa(anticlockwise).
Waya wowote unaopitisha umeme kando kando yake kuna mawimbi sumaku.Yanakuwa na nguvu kubwa kama umeme ni wa msongo mkubwa.
Ndio maana chunguza panapokuwa na umeme wa msongo mkubwa sana kunakuwa na eneo kubwa chini yake hairuhusiwi kujenga.
Kumbuka waya wa umeme ulio wazi hasa msongo mkubwa unapokuwa na nia ya kuugusa kiukweli kuna umbali kabla hujaugusa unakuvuta wenyewe shauri ya haya mawimbi sumaku.
Tuje kwenye mada nyaya za simu kumbuka sio tu zinapitisha mawimbi umeme ya maongezi zinapitisha mawimbi mengine mfano channel za TV,Fax,computer,wakati mwingine maongezi ya radio,fiber optics n.k.
Hivyo kuchanganya hizi nyaya na za umeme kuna uwezekano mkubwa wa muingiliano(interference) wa mawimbi sumaku na kuleta sintofahamu kubwa kimawasiliano.
Tanesco na TTCL wametiliana saini jana mradi wa kupitisha nyaya za mawasiliano kwenye nguzo za umeme 😉
 
Back
Top Bottom