Napendekeza: TAKUKURU wajifanye kama kondakta wa daladala ili wadake traffic wala rushwa

Napendekeza: TAKUKURU wajifanye kama kondakta wa daladala ili wadake traffic wala rushwa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nina pendekeza kama kweli TAKUKURU wako pale kumdhibiti na kupambana na rushwa basi wajifanye kama Kondakta wa daladala hasa za hapa Dar Es Salaam ili wakamate Traffic ambao wanaomba rushwa.

Kama hilo haliwezekani basi nashauri hiki kitengo aidha kifutwe au kibadilishiwe majukumu. Maana inafikirisha sana kwamba kila Raia anaona jinsi rushwa inavyoliwa kwa wazi kabisa na hawa askari wa usalama barabarani lakini TAKUKURU hawaioni.

Au hadi wapewe agizo na kutumwa!? Kwani Sheria haiwaruhusu kujifanyia kazi kwa namna yao hadi waagizwe na mamlaka zingine?

Soma Pia: Je, nini kifanyike ili kuongeza Ushiriki wa Wananchi katika Mapambano dhidi ya Rushwa?
 
Hii itakuwa dawa!

Matrafiki ki ukweli, jamaa wale iwapo wamejenga, basi tofari zote za majumba yao ni pesa ya haramu tupu!

Sitashangaa ukisikia mtu kadondokewa ukuta wake maana hakuna haki hata moja iliyotumika katika kujenga kwake
 
Nina pendekeza kama kweli Takukuru wako pale kumdhibiti na kupambana na rushwa basi wajifanye kama kondakta wa daladala hasa za hapa dar ili wakamate traffic hawa jamaa wanakula rushwa hadi kichefuchefu.

Kama hilo haliwezekani basi nashauri hiki kitengo aidha kifutwe au kibadilishiwe majukumu. Maana inafikirisha sana kwamba kila raia anaona jinsi rushwa inavyoliwa kwa wazi kabisa na hawa askari wa usalama barabarani lkn Takukuru hawaioni.
Au hadi wapewe agizo na kutumwa!? Kwani Sheria haiwaruhusu kujifanyia kazi kwa namna yao hadi waagizwe na mamlaka zingine?
Sidhani kama kuna traffick atabaki road, itakuwa mtafaruku
 
Hizo buku buku ndo zinakutoa kamasi? Hizo ni kama TIPS tu, tunashughulikia mambo makubwa.
 
Nina pendekeza kama kweli Takukuru wako pale kumdhibiti na kupambana na rushwa basi wajifanye kama kondakta wa daladala hasa za hapa dar ili wakamate traffic hawa jamaa wanakula rushwa hadi kichefuchefu.

Kama hilo haliwezekani basi nashauri hiki kitengo aidha kifutwe au kibadilishiwe majukumu. Maana inafikirisha sana kwamba kila raia anaona jinsi rushwa inavyoliwa kwa wazi kabisa na hawa askari wa usalama barabarani lkn Takukuru hawaioni.
Au hadi wapewe agizo na kutumwa!? Kwani Sheria haiwaruhusu kujifanyia kazi kwa namna yao hadi waagizwe na mamlaka zingine?
Takukuru wenyewe ni wala rushwa tena ile mbaya kwani we unafikiri hawajui sehemu zinazo toa rushwa? rushwa ya trafiki ina pangwa na boss wao, ukiwagusa na wewe utaguswa tu.
 
TAKUKURU wenyewe ni njaa tu pale,wenye mishahara nafuu ni maafisa wachache wale wa chini tia tia maji.
Mwenye njaa hawezi kumkanata mwenye njaa.

By the way, authority na power of arrest ni complicated kwa TAKUKURU.
 
Naskia mkuu wao akikuoanga sehemu yenye maokoto mwisho wa siku na yeye anataka mgao la sivyo unapelekwa ndichi uko ambako gari za maokoto hazipiti.
 
Ila tuseme ukweli tu, watanganyika tuna magari mabovu ambayo yakipigwa fine kihalali kila siku nchi itaneemeka sana.
 
Traffic wakisema wafuate sheria gari nyingi zitapaki na baadhi ya watu vifungo vitawahusu. Hawa jamaa huwa wanatumia tu busara. Hata TRA nao wakisema wafuate sheria nadhani zaidi ya nusu ya biashara Tanzania zitafungwa. Haya mambo yana mizizi kuanzia ngazi ya familia. Wengi wetu tumekuzwa tukiaminishwa tusome tuje kufanya kazi sehemu zenye marupurupu (rushwa & ufisadi) kama TRA, TPA au BOT. Kijana akianza kazi sehemu kama TRA akakaa miaka miwili bila kununua gari au kujenga hata familia huanza kumlaumu kuwa ni mzembe mbona mtoto wa fulani ana maendeleo. Wengi hapa mnalaumu ila mkipewa vitengo mtafanya kufuru kuliko waliopo.
 
Kuna ndezi zinatetea, wtf?
Hawa jamaa ni wanapokea 2k-10k na hawakagui tena makosa ya magari, ndio maana tuna magari mabovu yanatembea tu barabarani bila shida, rushwa ya 2k. Kuna kadada kanasimama njia ya Goba pale kituo cha Manone(mbele ya Kwa robert), kale kadada imekuwa ndio kazi yake sasa. Badala ya kukagua magari, kanapoea tu 10k za watu, Kale ka Khadija kale..
 
Kwanini lakini mnapingana na kauli ya Mkuu wa nchi? Ameshasema, wale urefu wa kamba zao. Wameruhusiwa hata hao Takukuru wanakula urefu wa kamba zao. Kipindi hiki ni unakuwa vile unataka, uwe na hela au kapuku.

Tukiachana na hayo, kiongozi wa nchi hakupaswa kutoa kauli ile, wale kutoka wapi na ni kodi za wananchi, kuwanyonya. Halafu mko humu kumpamba hapohapo mnalia rushwa. Aifute kauli yake, na Takukuru watangaze dau, kila ukiweza kupiga picha Traffic akipokea rushwa kuna zawadi. Angalau itapunguza.
 
Back
Top Bottom