Napendekeza: TAKUKURU wajifanye kama kondakta wa daladala ili wadake traffic wala rushwa

Napendekeza: TAKUKURU wajifanye kama kondakta wa daladala ili wadake traffic wala rushwa

Kwanini lakini mnapingana na kauli ya Mkuu wa nchi? Ameshasema, wale urefu wa kamba zao. Wameruhusiwa hata hao Takukuru wanakula urefu wa kamba zao. Kipindi hiki ni unakuwa vile unataka, uwe na hela au kapuku.

Tukiachana na hayo, kiongozi wa nchi hakupaswa kutoa kauli ile, wale kutoka wapi na ni kodi za wananchi, kuwanyonya. Halafu mko humu kumpamba hapohapo mnalia rushwa. Aifute kauli yake, na Takukuru watangaze dau, kila ukiweza kupiga picha Traffic akipokea rushwa kuna zawadi. Angalau itapunguza.
Watu wanalalamika as if hiyo kauli mama hakuisema.
Huyo TAKUKURU aliisikia hiyo kauli,polisi pia aliisikia,nani wa kulaumiwa?
 
Makondakta wa Ukweli, watawapa Umbeya Tragic...!

Coz washazoea kutoa Rushwa.
 
Traffic wakisema wafuate sheria gari nyingi zitapaki na baadhi ya watu vifungo vitawahusu. Hawa jamaa huwa wanatumia tu busara. Hata TRA nao wakisema wafuate sheria nadhani zaidi ya nusu ya biashara Tanzania zitafungwa. Haya mambo yana mizizi kuanzia ngazi ya familia. Wengi wetu tumekuzwa tukiaminishwa tusome tuje kufanya kazi sehemu zenye marupurupu (rushwa & ufisadi) kama TRA, TPA au BOT. Kijana akianza kazi sehemu kama TRA akakaa miaka miwili bila kununua gari au kujenga hata familia huanza kumlaumu kuwa ni mzembe mbona mtoto wa fulani ana maendeleo. Wengi hapa mnalaumu ila mkipewa vitengo mtafanya kufuru kuliko waliopo.
Wafuate sheria ili nchi iendeshwe kwa kufuata sheria
 
Nina pendekeza kama kweli TAKUKURU wako pale kumdhibiti na kupambana na rushwa basi wajifanye kama Kondakta wa daladala hasa za hapa Dar Es Salaam ili wakamate Traffic ambao wanaomba rushwa.

Kama hilo haliwezekani basi nashauri hiki kitengo aidha kifutwe au kibadilishiwe majukumu. Maana inafikirisha sana kwamba kila Raia anaona jinsi rushwa inavyoliwa kwa wazi kabisa na hawa askari wa usalama barabarani lakini TAKUKURU hawaioni.

Au hadi wapewe agizo na kutumwa!? Kwani Sheria haiwaruhusu kujifanyia kazi kwa namna yao hadi waagizwe na mamlaka zingine?

Soma Pia: Je, nini kifanyike ili kuongeza Ushiriki wa Wananchi katika Mapambano dhidi ya Rushwa?
Tena kwa asubuhi na mapema wanajipanga kabisa kwenye vituo vya Daladala kuchukua mapato yao kabla jua alijazama. Really trafiki wamejisahau mno na wamelewa Rushwa kuliko kazi yao!
 
Huko kote mbali, Takukutu wakiwafanyia lifestlyee audit hakuna askari anachomoka,.
 
Wafuate sheria ili nchi iendeshwe kwa kufuata sheria
Wewe unafuata sheria? Hujawahi kuwatetea wamachinga wanaopanga bidhaa barabarani? Hujawahi kuwatetea mama ntilie wanaofukuzwa maeneo yasiyo rasmi? Hujawahi kuwatetea watu wanaovunjiwa nyumba zao kwa kujenga kwenye hifadhi ya barabara?
 
Tena hao sitaki hata kuwaona uliwahi niona wapi nawatetea!?
 
Buku ni rushwa ama hela ya maji waoneeni huruma kukaa kwenye jua sio mchezo
Hiyo ni kazi kama kazi nyingine kama kukaa kwenye jua kuna askari anaona sio mchezo basi iache kazi hiyo ili wenye uwezo nayo waifanye. watu wanalima na mvua nini jua.
 
Nina pendekeza kama kweli TAKUKURU wako pale kumdhibiti na kupambana na rushwa basi wajifanye kama Kondakta wa daladala hasa za hapa Dar Es Salaam ili wakamate Traffic ambao wanaomba rushwa.

Kama hilo haliwezekani basi nashauri hiki kitengo aidha kifutwe au kibadilishiwe majukumu. Maana inafikirisha sana kwamba kila Raia anaona jinsi rushwa inavyoliwa kwa wazi kabisa na hawa askari wa usalama barabarani lakini TAKUKURU hawaioni.

Au hadi wapewe agizo na kutumwa!? Kwani Sheria haiwaruhusu kujifanyia kazi kwa namna yao hadi waagizwe na mamlaka zingine?

Soma Pia: Je, nini kifanyike ili kuongeza Ushiriki wa Wananchi katika Mapambano dhidi ya Rushwa?
Janja janja😆
 
Hii nchi si takukuru wala tiss wote hakuna kitu!!
Huwaga najiuliza kazi zao ni zipi!?
Tiss wanashindwaje kujifanya wasaka viungo vya albino Ili wajue mtandao!??
Tiss wanashindwaje kujifanya mateja wajue wauza unga wapo wapi na ni akina nani!?
Tiss wanashindwaje kujua kama peas za sauz zinaweza kulimwa hata lushoto Kwa kupeleleza udongo na climate ya sauzi!??
Huku Tanga na maeneo ya same wakenya wanakuja kuzoa machungwa na vitunguu nasikia wanauza ulaya !! Kwann watz wasiuze wao ulaya direct!? Hili wangeweza kulifanya! Ila hakuna kitu!!
Takukuru ndio usiseme rushwa kibaoo za trafik !! Wanachujua ni kuendesha vi Toyota vya mkopo vya premio[emoji42][emoji42]
 
Nina pendekeza kama kweli TAKUKURU wako pale kumdhibiti na kupambana na rushwa basi wajifanye kama Kondakta wa daladala hasa za hapa Dar Es Salaam ili wakamate Traffic ambao wanaomba rushwa.

Kama hilo haliwezekani basi nashauri hiki kitengo aidha kifutwe au kibadilishiwe majukumu. Maana inafikirisha sana kwamba kila Raia anaona jinsi rushwa inavyoliwa kwa wazi kabisa na hawa askari wa usalama barabarani lakini TAKUKURU hawaioni.

Au hadi wapewe agizo na kutumwa!? Kwani Sheria haiwaruhusu kujifanyia kazi kwa namna yao hadi waagizwe na mamlaka zingine?

Soma Pia: Je, nini kifanyike ili kuongeza Ushiriki wa Wananchi katika Mapambano dhidi ya Rushwa?
Hiyo ishashindikana

Nchi ngumu hii ile hela wanaokula matrafik na wao wanaeleka mgawo wao kwa wakubwa zao
In short wametumwaaaa

Ova
Tlaatlaah
 
Hiyo ishashindikana

Nchi ngumu hii ile hela wanaokula matrafik na wao wanaeleka mgawo wao kwa wakubwa zao
In short wametumwaaaa

Ova
Tlaatlaah
nadhani kila taasisi ya umma humu nchini,
inawajibika kwa sehemu yake kwa mujibu wa sheria na katiba,

na kwa utashi wa waandamizi wake wanaoongoza taasisi hizo kuona namna ya kuzingatia maoni, mitazamo na ushauri wa wananchi kujiimarisha zaidi na kuongeza ufanisi kiutendaji kazi wa taasisi hizo :pulpTRAVOLTA:
 
Kila daladala kuna vituo lazima waache 2000
Konda anashuka anakwenda mminyia traffic

Ova
Wala hahitaji mshahara
Ila ukiangalia malori tairi zimeisha kabisa na zikiuwa wanakuambia break zimefeli kumbe kaachiwa kwa buku
 
Back
Top Bottom