Napendekeza tuanzishe JF Jogging Club ya mtandaoni

Mimi naenda Km 8 hadi 10 Kila siku jioni naenda kukimbia na Wakati wa kurudi natembea Huwa yanaambatana na mazoezi ya viungo,Kwa vile Niko Kisarawe huku nakutana na vilima viwili wakati wa kwenda na kurudi kimoja.Wakati huu wa Mvua na mwezi wa RAMADHANI Kwa wadau tumesimama.Ila Kila jioni pushups 10, Squatter series,mazoezi ya kukata tumbo pamoja na kunyosha mwili,haya nafanyia chumbani.Kwa Sasa Soda situmii kabisa,Nyama nimeacha kabisa.Niko na zaidi ya 40 lakini shemeji yenu anajua.
Madhara ya nyama ni yapi mkuu?
 
Wakuu sio siri kuwa ukivuka miaka 30 kuna mabadiliko ya kimwili lazima uyaone yakikujia kwa kasi ikiwemo kitambi. Kwa wale waliojaliwa riziki kidogo hali huwa mbaya zaidi ndo maana Mzee Janabi anazidi kutoa matamko. Wengi wetu tumekulia kwenye familia duni hivyo huku ukubwani baada ya mambo kuwa mazuri tunaanza kufakamia vyakula vya ndoto zetu. Sio mbaya ila lazima kuchukua tahadhari.

Sasa mimi nimekuja na hii hamasa ya members wa JF kujipa muda hata wa dakika 20 kufanya jogging ili kusaidia mwili kuwa fit. Kwa sababu humu hatutaki kujuana physically ninashauri tujiorodheshe tunaopenda mazoezi kisha kila siku tuji-committ kufanya mazoezi na kupeana updates kilichojiri huko uliko.

Binafsi sio mtaalamu wa mazoezi ila ningependa tuanze na 1KM CHALLENGE. Yaani kila siku members tupeane challenge ya kukimbia 1km.

Members watakaofanya hii challenge wanaweza tumia App ya jogging kama ile ya ADIDAS kwenye simu zao na kutupia matokeo yao kwa maana ya umbali waliokimbia, muda, calories burnes na pace. Ninaamini hii itahamasisha.

Ninakaribisha maoni.
Count me in.
 
Wazo Zuri na litaleta hamasa., km 1 ni ndogo at least 5 either mtu akimbie au atembee..watu wengi humu wanapenda privacy ni bora mtu akatuma details kutoka kwenye saa au app na sio ramani..

Kwa mahitaji ya vifaa vyote vya mazoezi kuanzia vipochi vya kubeba simu, nguo za kukimbilia, saa, etc na vifaa vyote vya mazoezi ya nyumbani kama Matt's, step board, weights etc..tuwasiliane...
 
Wakuu sio siri kuwa ukivuka miaka 30 kuna mabadiliko ya kimwili lazima uyaone yakikujia kwa kasi ikiwemo kitambi. Kwa wale waliojaliwa riziki kidogo hali huwa mbaya zaidi ndo maana Mzee Janabi anazidi kutoa matamko. Wengi wetu tumekulia kwenye familia duni hivyo huku ukubwani baada ya mambo kuwa mazuri tunaanza kufakamia vyakula vya ndoto zetu. Sio mbaya ila lazima kuchukua tahadhari.

Sasa mimi nimekuja na hii hamasa ya members wa JF kujipa muda hata wa dakika 20 kufanya jogging ili kusaidia mwili kuwa fit. Kwa sababu humu hatutaki kujuana physically ninashauri tujiorodheshe tunaopenda mazoezi kisha kila siku tuji-committ kufanya mazoezi na kupeana updates kilichojiri huko uliko.

Binafsi sio mtaalamu wa mazoezi ila ningependa tuanze na 1KM CHALLENGE. Yaani kila siku members tupeane challenge ya kukimbia 1km.

Members watakaofanya hii challenge wanaweza tumia App ya jogging kama ile ya ADIDAS kwenye simu zao na kutupia matokeo yao kwa maana ya umbali waliokimbia, muda, calories burnes na pace. Ninaamini hii itahamasisha.

Ninakaribisha maoni.
Mliofakamia vyakula hadi mkapata vitambi fanyeni, wengine tuko wembamba kama reli.
 
Back
Top Bottom