Napendekeza tuanzishe JF Jogging Club ya mtandaoni

Napendekeza tuanzishe JF Jogging Club ya mtandaoni

Usicheke, halafu wewe MamaSamia2025 inaonekana una kitambi.
Ndo kinakuja kwa kasi aisee.. ni hofu tupu. Kwa miaka mingi kina dada wamekuwa wakiniita handsome ila kwa sasa kumekuwa na uhaba mkubwa wa wanaosema hivyo. Majuzi nilimtembelea binamu yangu tukapiga picha kumbe nilikuwa sijui nilivyo kwa sasa... karibia nijikatae.... picha zilitoka kama nimevimba usoni.. shavu kama mtu aliyeumwa na nyuki.
 
Piga pushups 100 kila siku, anza kuruka kamba, kisha mazoezi ya tumbo.

Baada ya mwezi mmoja utakuja kunishukuru.
 
Wakuu leo ndo tunaanza program yetu rasmi. Mimi nitawapa update kilichojiri nikishatoka jogging... wenye muda pia msiache kwenda.
 
Wakuu binafsi. Nimekimbia 1km na kutembea 5km na matokeo ni kama yanavyoonekana.
IMG-20240325-WA0000.jpg
 
Wakuu sio siri kuwa ukivuka miaka 30 kuna mabadiliko ya kimwili lazima uyaone yakikujia kwa kasi ikiwemo kitambi. Kwa wale waliojaliwa riziki kidogo hali huwa mbaya zaidi ndo maana Mzee Janabi anazidi kutoa matamko. Wengi wetu tumekulia kwenye familia duni hivyo huku ukubwani baada ya mambo kuwa mazuri tunaanza kufakamia vyakula vya ndoto zetu. Sio mbaya ila lazima kuchukua tahadhari.

Sasa mimi nimekuja na hii hamasa ya members wa JF kujipa muda hata wa dakika 20 kufanya jogging ili kusaidia mwili kuwa fit. Kwa sababu humu hatutaki kujuana physically ninashauri tujiorodheshe tunaopenda mazoezi kisha kila siku tuji-committ kufanya mazoezi na kupeana updates kilichojiri huko uliko.

Binafsi sio mtaalamu wa mazoezi ila ningependa tuanze na 1KM CHALLENGE. Yaani kila siku members tupeane challenge ya kukimbia 1km.

Members watakaofanya hii challenge wanaweza tumia App ya jogging kama ile ya ADIDAS kwenye simu zao na kutupia matokeo yao kwa maana ya umbali waliokimbia, muda, calories burnes na pace. Ninaamini hii itahamasisha.

Ninakaribisha maoni.
Huu ni mfano wa report ya mazoezi niliofanya ya kutembea 5km na kukimbia 1km. Kama huna App fanya kupakua ADIDAS RUNNING.
View attachment 2943143
Wazo zuri
 
Mimi naenda Km 8 hadi 10 Kila siku jioni naenda kukimbia na Wakati wa kurudi natembea Huwa yanaambatana na mazoezi ya viungo,Kwa vile Niko Kisarawe huku nakutana na vilima viwili wakati wa kwenda na kurudi kimoja.Wakati huu wa Mvua na mwezi wa RAMADHANI Kwa wadau tumesimama.Ila Kila jioni pushups 10, Squatter series,mazoezi ya kukata tumbo pamoja na kunyosha mwili,haya nafanyia chumbani.Kwa Sasa Soda situmii kabisa,Nyama nimeacha kabisa.Niko na zaidi ya 40 lakini shemeji yenu anajua.

Daaah kisarawe sio Poa hasa ule mlima wa kuisaka Minaki Seco Ule mlima ni Balaaa kupandsha gari zenyewe tu Huwa zinapanda Taratibu
 
Back
Top Bottom