Napendekeza Tundu Lissu ateuliwe kuwania Tuzo ya Amani ya Nobeli kwa mwaka 2027

Napendekeza Tundu Lissu ateuliwe kuwania Tuzo ya Amani ya Nobeli kwa mwaka 2027

Naunga mkono hoja.
Hakuna sacrifice kubwa zaidi ambayo mtu anaweza kufanya kuliko kuweka maisha yake mwenyewe rehani kwa ajili ya wengine, tena huku akikataa maslahi yake binafsi.
Tundu Lissu for Noble Prize šŸ†
 
ok.
Na anavyotibua minywele kama wendawazimu, anavyopiga mayowe mahakamani na kurusha mikono hewani, anafaa sana kupewa tunzo hiyo aise.

naunga mkono hii porojo useless dhidi ya huyo kibaraka mropokaji wa mabwenyenye ya magharibi šŸ’
IMG_9365.jpeg
 
Naunga Mkono hoja.
Wazo zuri sana Mkuu
Mungu akubariki sana.
Huyu mtu anastahili kabisa hii tuzo.

Nitafanya kila maombi na bidii jamaa aingie kwenye Nomination
Akina Dr Slaa,Mama Kijo-Bisimba na Generali ulimwengu wawasiliane na Pro. Shivji aanzishe huo mchakato. Anahitajika mtu wa kuanzisha
 
Kwa juhudi zake tena bila kuchoka wala kukata tamaa katika kutetea haki za binadamu, kupigania utawala bora wa kisheria na kupigania demokrasia nchini, Tundu Lissu anastahili kabisa kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobeli 2027.

Kama mwaka jana Corina Machado ndio alishinda, sioni kwa nini Lissu asiweze kushinda. Machado hana resume inayoishinda resume ya Lissu.

Sasa kwa vile mimi sina sifa za kuweza kumpendekeza, napendekeza Watanzania walizo na sifa za kumpendekeza, wafanye hivyo.

Sifa za kuweza kumpendekeza zipo kadhaa. Ukitaka kuzifahamu, ingia Hapo kwenye tovuti yao: Nomination and selection of Nobel Peace Prize laureates - NobelPrize.org

Mtu kama Prof. Shivji anazo sifa za kumpendekeza Lissu huko kwenye kamati ya Nobeli.

Wakufunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, hususan wale wa kitivo cha sheria, wanazo sifa za kuweza kumpendekeza.

Hata wakufunzi wa vyuo vingine vilivyo na accreditation inayoeleweka na kukubalika [siyo kama kile chuo cha so called jenerali Mkunda], wanaweza pia kumpendekeza.

Tundu Lissu anastahili kabisa kupewa hiyo tuzo.

Na kama akishinda hiyo tuzo, hiyo itakuwa the ultimate slap kwa muuaji.

Kama unakubaliana na mimi, shusha maoni yako hapo chini na ikiwezekana tuanzishe kabisa kampeni ili nominations ziwezwe kutumwa kabla ya Januari 31, 2027.
Mbona Tayari aliteuliwa?

Unaweza ku google. Huko huwa hawatangazi majina. Ila kuna taarifa Tayari jina lake lipo ndani ya list
 
Ilikuwa December 2025. Ila Hawa jamaa huwa wanafanya majina siri mpaka baada ya miaka 50.
 

Attachments

  • IMG_5054.jpeg
    IMG_5054.jpeg
    356.3 KB · Views: 10
Naunga mkono. Hata ikipelekea kuwa nominated tu itakuwa ushindi mkubwa. Yule mama wa Mynamr alishinda, hakufanya makuu kuliko Lissu. Lissu kafanya makubwa kuanzia kupambanis wachimbaji hadi haki za kisiasa.
 
Majina ya wanaowania tuzo ya Amani ya Nobel huwa ni siri na majina yanapelekwa kabla ya tarehe 31 Januari na mshindi wa mwaka huu atatangazwa tarehe 9 Oktoba mwaka huu.
Nani mwenye sifa ya kupeleka jina ni hawa wafuatao
Kwa mfano, mteuaji halali anaweza kuwa:
1.Mbunge au mwanachama wa serikali ya nchi huru.
2.Mkuu wa nchi.
3.Profesa wa chuo kikuu katika taaluma zilizotajwa na kanuni.
4. Mshindi wa zamani wa Nobel Peace Prize.
5.Mwanachama wa Norwegian Nobel Committee.
6. Baadhi ya wataalamu na viongozi wa taasisi zinazotajwa katika vigezo rasmi.

Kwa vile mimi na wewe hatuko kwenye hayo makundi tuwaombe wabunge wa ACT wapeleke jina au akina Shivji wapeleke jina la Lissu.

Naunga mkono hoja
Warioba anaweza kupeleka jina likakubalika
 
Back
Top Bottom