Napendekeza Uongozi Uachane Na Wachezaji Hawa Wawili Wa Kigeni Kikosini Yanga SC.

Napendekeza Uongozi Uachane Na Wachezaji Hawa Wawili Wa Kigeni Kikosini Yanga SC.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Mpaka sasa wanayanga mnapaswa kujipiga kifuani kwa kazi kubwa sana iliyofanywa na viongozi wenu katika dirisha hili la usajili.

Wengi wenu mmeonekana kuridhishwa kwa asilimia 100 kwa namna usajili ulivyofanyika. Hata hivyo kuna idadi wa wachezaji wawili wa kigeni ambao hawajatangazwa kuachwa ili kubalance idadi ya wachezaji 12 wa kigeni.

Upande wa Kushoto:-
Yocouba Sogne
Bernard Morrison
Dickson Ambundo

Upande wa Kulia:-
Stephane Aziz Ki
Kambole Lazarou
Wonder Kid

Juu kati:-
Fiston Mayele
Herithier Makambo
Yusuph Athumani
Crispin Ngushi

Katika maeneo tajwa hayo juu ambayo ni ya msingi sioni umuhimu wa kuwepo kwa Chico Ushindi wala Jesus Ducapel Moloko.

Aidha eneo la kiungo kumejaa wachezaji wa nyota 5 kama vile AUCHO, GAEL, BANGALA, FEISAL na BABU KAJU.

Je kuna nafasi katika eneo la kiungo ambako anaweza kuingia Moloko au Chico? Jibu ni hapana.

Hivyo basi ni wakati sahihi wa kuwatakia mkono wa kwa kheri kwa kuwa sehemu ya ubingwa wa ligiKUU tanzania bara.
 
Mimi naona jesus bado tumpe nafasi jamaa ametoa mchango mkubwa sana na mpambanaji sana haogopi.

Ushindi ana vitu vingi zaidi mguuni lakini muoga na hawezi kusaidia kukaba mechi ya Coastal final ni reference nzuri
 
Wanasimba msijibu chochote kwenye huu uzi, acha wafu wazikane wenyewe
 
Msiajribu kumuacha Yacouba mkamtibua Ki aziz, shauri zenu na ujinga wenu wa kulala kambini hataki kuusikia.

Unaachana vipi na mchezaji mzuri kama Yacouba Sogne.?

Hakuna hata shabiki mmoja wa Yanga SC anataka Sogne aindoke.

Kwa iyo akiumia Wakili Msomi unataka acheze Ambundo. Hapana Sogne atabaki na ataendelea kukiwasha tena mpaka Makolo FC waseme Pooh.

Atake Ki aziz au Asitake. Yacouba SOGNE ni christiano ronaldo wa NBC PREMIER LEAGUE.
 
Tunasubiri club itoe tamko, nasikia wawili wa kimataifa wataachwa ila sijajua ni nani
 
Kama kuna majembe makali zaidi, basi Jesus Moloko na Chico Ushindi wanastahili kabisa kupewa mkono wa kwaheri.

Kimsingi Yacouba Sogne hana tofauti na Mapinduzi Balama. Kwa kiasi fulani majeraha yalidhoofisha viwango vyao.
 
Mpaka sasa wanayanga mnapaswa kujipiga kifuani kwa kazi kubwa sana iliyofanywa na viongozi wenu katika dirisha hili la usajili.

Wengi wenu mmeonekana kuridhishwa kwa asilimia 100 kwa namna usajili ulivyofanyika. Hata hivyo kuna idadi wa wachezaji wawili wa kigeni ambao hawajatangazwa kuachwa ili kubalance idadi ya wachezaji 12 wa kigeni.

Upande wa Kushoto:-
Yocouba Sogne
Bernard Morrison
Dickson Ambundo

Upande wa Kulia:-
Stephane Aziz Ki
Kambole Lazarou
Wonder Kid

Juu kati:-
Fiston Mayele
Herithier Makambo
Yusuph Athumani
Crispin Ngushi

Katika maeneo tajwa hayo juu ambayo ni ya msingi sioni umuhimu wa kuwepo kwa Chico Ushindi wala Jesus Ducapel Moloko.

Aidha eneo la kiungo kumejaa wachezaji wa nyota 5 kama vile AUCHO, GAEL, BANGALA, FEISAL na BABU KAJU.

Je kuna nafasi katika eneo la kiungo ambako anaweza kuingia Moloko au Chico? Jibu ni hapana.

Hivyo basi ni wakati sahihi wa kuwatakia mkono wa kwa kheri kwa kuwa sehemu ya ubingwa wa ligiKUU tanzania bara.
Mkuu Nadhani Kati Ya Moloko Na Chico Kuna Mmoja Atabaki, Sina Hakika Sana Na Yacouba Kuwepo Msimu Ujao Ndani Ya Kikosi Cha Yanga Kutokana Na Hali Yake...Kuna Tetesi Kwamba Anatolewa Kwa Mkopo Geita Gold.
 
Changia kambi ya yanga kwa namba
0789–09000 jina litakuja engineer hersi mchango wako ni muhimu sana mwanachi katika ujenzi wa team yetu. [emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama kuna majembe makali zaidi, basi Jesus Moloko na Chico Ushindi wanastahili kabisa kupewa mkono wa kwaheri.

Kimsingi Yacouba Sogne hana tofauti na Mapinduzi Balama. Kwa kiasi fulani majeraha yalidhoofisha viwango vyao.
Yacouba hawezi toka kabisaaa.
 
Chico Ushindi anaelekea Al Hilal Sudan na Yacouba anatolewa mkopo kama haitabadilika itakuwa ni Geita Gold. Kwa Yacouba kutolewa kwa mkopo ni sawa ili Yanga ijiridhishe kama atakuwa amepona kabisa na vile vile apate mechi "fitness" kwa kucheza mara kwa mara akiwa timu ndogo. Kumbuka kuwa akibaki Yanga hatapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa hiyo ni vigumu sana kurudisha kiwango chake kwa muda mfupi. Na Yanga kumtoa kwa mkopo ni faida kwao kwani wanaweza kumrudisha wakati wa dirisha dogo iwapo atakuwa ameimarika kifya na kiwango kimerudi na hasa iwapo kutakuwa na mchezaji wa kigeni aliyeshuka kiwango kuelekea dirisha dogo.
 
Mkuu Nadhani Kati Ya Moloko Na Chico Kuna Mmoja Atabaki, Sina Hakika Sana Na Yacouba Kuwepo Msimu Ujao Ndani Ya Kikosi Cha Yanga Kutokana Na Hali Yake...Kuna Tetesi Kwamba Anatolewa Kwa Mkopo Geita Gold.

Labda awe hajapona ila hizo zitabaki kuwa tetesi.

Kwa mchezaji mkubwa kiasi kile hawezi kubali kwenda Geita Gold FC
 
Back
Top Bottom