Napendekeza upimaji VVU kwa lazima kila mwaka; waathirika wawekewe alama sehemu za siri

Napendekeza upimaji VVU kwa lazima kila mwaka; waathirika wawekewe alama sehemu za siri

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Mpaka mwisho wa hii dunia hatutapata suluhisho; unless igunduliwe chanjo au dawa. Kinyime cha hapo dawa ni hiyo niliyowapa, ila mpango huu unahitaji ujasiri kuufanikisha, Rais legelege hatoweza kamwe! Pia Airport pawekwe utaratibu wa wageni wote kupimwa VVU kabla ya kuingia nchini, AIDS should be treated like EBOLA! Mi nashangaaga tunabembeleza bembeleza nini na huku watu wanazidi kuambukizana kila kukicha, tena tunapeana dawa za kurefusha maisha (kurefusha muda wa kusambaza), this is shear insanity! Its madness!!
========================================
UPDATE:16/02/2018
"hili suala inatakiwa liwe la lazima kwa sababu watu hawapimi, wanashindwa kujitambua hivyo wanaendelea kueneza kwa wengine sheria ikiwepo kila mtu apime kwa lazima itasaidia sana," alisema

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge, Dr Jasmini Bunga alikubalina na Ombi hilo na kueleza kuwa litasaidia mkakati wa serikali wa kukabiliana na Maambukizi mapya ya Ukimwi.

======================================

UPDATE: 31/05/2018
Wanaume kupima maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) Tanzania nzima

20180531_062303.jpg

Mh. Waziri Mkuu Kasim Majaliwa atazindua mpango huu mzuri wa kuwapima wanaume wote maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi nchi nzima. Uwe unataka ama uwe hutaki lakini ni lazima upimwe tu. Hakuna namna.
Tutatoboa tu.

=========

“Serikali tumeandaa kampeni maalum ya kuhamasisha upimaji wa VVU na kuanza matumizi ya dawa za kufubaza VVU mara moja, hasa kwa wanaume. Kampeni hii itazinduliwa rasmi na mimi mwenyewe jijini Dodoma 19 Juni 10,” alisema jana.

Alisema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR).

“Takwimu zinaonyesha watu ambao wako tayari kupima kwa hiari yao siku zote ni wanawake. Kinababa wakiambiwa hutoa sababu mara hiki, mara kile. Nitoe wito kwa wanaume wote, tubadilike! Ni vema tushiriki kampeni ya wanaume kujitambua na kupima ili tujue hali zetu,” alisema.

Amewataka wadau wa masuala ya Ukimwi washiriki kikamilifu katika kampeni hiyo baada ya uzinduzi na pia kuwataka wakuu wa mikoa yote wasimamie kampeni hizo muhimu katika mikoa yao hadi ngazi za vijiji.

Waziri Mkuu alisema ujio wa PEPFAR umeleta mafanikio makubwa katika vita dhidi ya Ukimwi na kupitia shughuli zake, elimu ya kinga na ufahamu kuhusu ugonjwa huo ilitolewa kwa watu wa rika na makundi mbalimbali ya jamii.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Tanzania inaendelea kukabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo ukubwa wa viwango vya maambukizi na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoambukizwa VVU katika baadhi ya mikoa nchini.

Kwa mujibu wa Majaliwa, kuna mikoa 14 ambayo kiwango cha maambukizi kiko juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia 4.7 na kuitaja ni Njombe asilimia 11.4, Iringa (11.3), Mbeya (9.3), Mwanza (7.2), Kagera ( 6.5) na Katavi (5.9).

Mingine ni Shinyanga (asilimia 5.9), Songwe (5.8) Ruvuma (5.6) Pwani (5.5) Tabora (5.1) pamoja na Tanga, Dodoma na Geita ambayo yote ina asilimia 5.0 ya maambukizi.

Waziri Mkuu aliitaja mikoa mingine sita ambayo ina ongezeko kubwa la watu wanaoishi na VVU ni Iringa (asilimia 11.3), Mwanza (7.2), Kagera (6.5), Tanga (5.0), Dodoma (5.0) na Manyara (2.3).

Alifafanua takwimu hizo zinaonyesha kuwa nguvu na jitihada zaidi zinahitajika katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU kwa kuweka utaratibu thabiti na endelevu wa kutoa elimu na hamasa ya kutumia huduma zilizopo za kupambana na UKIMWI nchini.

“Kwa hiyo, programu za kinga zinapaswa kuwa endelevu kwenye mikoa yote nchini, hususan mikoa yenye kiwango cha juu cha maambukizi. Pia huduma za ARV ziendelee kupewa kipaumbele katika mipango yetu,” alisisitiza.

Akimkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Tanzania kwa sasa ina watu karibu milioni moja ambao wako kwenye matibabu ya kufubaza VVU.

“Kutokana na mpango wa PEPFAR, Tanzania imeshapokea Sh. trilioni 10 tangu mfuko huu uanzishwe mwaka 2003 na matumizi ya dawa za kufubaza VVU yamesaidia kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na Ukimwi kwa asilimia 70, yaani kutoka vifo 110,000 mwaka 2003 hadi kufikia 33,000 mwaka 2016,” alisema.

Alisema kutokana na matumizi ya dawa hizo, maambukizi mapya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto nayo pia yamepungua kutoka asilimia 12 na kufikia 4.9.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson, alisema kati ya sasa na Septemba 2019, PEPFAR inatarajia kutumia dola za Marekani milioni 512 (zaidi ya Sh. trilioni moja) katika kuboresha huduma za kuzuia maambukizi ya VVU, upimaji na matibabu nchini.

Alisema wanapoendelea na utekelezaji wa kazi za mfuko huo na maadhimisho ya miaka 15 ya PEPFAR, kampeni yao itaendelea kwa mwaka wote wa 2018 na imelenga kupunguza unyanyapaa na tabia ya kuwatenga watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

“Kampeni ya PEPFAR15 inalenga kupunguza unyanyapaa, kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma zitolewazo za kukabiliana na VVU. Kila mtu atakayepimwa na kugundulika kuwa ana maambukizi ya VVU, ataanzishiwa matibabu mara moja,” alisema na kuongeza:

“Tutafanya kazi na watu wanaoishi na VVU nchini kote ili kusimulia habari nzuri za watu wanaoishi na VVU ambao waliwahi kuwa dhaifu ama wagonjwa, lakini sasa wana nguvu na afya; habari za akinamama wanaoishi na VVU na wanapata matibabu ili kuwalinda watoto wao.”

Chanzo: Nipashe
 
Aisee!.

Nakumbuka somo la kutowanyanyapaa wenye VVU.

Sasa tukifanya hivyo basi tunawanyanyapaa moja kwa moja, tunawakosesha ule Uhuru.
Hata kama tutawaekea alama, bado tu wataambukiza wengine kwani ugonjwa huo haumbukizwi tu kwa njia za kingono.

Ni kuwa makini tu na kumuomba Mwenyenzi Mungu.
 
Aahahaaaaaaaa
uko sawa kabisa.
Ingawa mijitu ya human right inaweza kupinga. Ila kama alama inawekwa karibu na sehemu nyeti mimi sioni kama ni tatizo.
Anayetaka kuuvaa na auvae makusudi.
Tena kwa wanaume inaweza ikawekwa insuch a way kwamba haionekani hadi uume usimame, kwahiyo haitamzuia kuoga na wenzake kama ni anaishi bwenini
 
Aisee!.

Nakumbuka somo la kutowanyanyapaa wenye VVU.

Sasa tukifanya hivyo basi tunawanyanyapaa moja kwa moja, tunawakosesha ule Uhuru.
Hata kama tutawaekea alama, bado tu wataambukiza wengine kwani ugonjwa huo haumbukizwi tu kwa njia za kingono.

Ni kuwa makini tu na kumuomba Mwenyenzi Mungu.
Hilo somo la kunyanyapaa ni propaganda ya wamarekani kuhakikisha waathirika wanapata muda wa kutosha wa kuua wenzao, tujitoe akili hata kwa miaka mi5 mfululizo, Tanzania itakuwa ndio nchi pekee ambayo watu wataweza kufanya ngono bila kondom na bila wasiwasi wankuambukizwa, hii itapelekea kuongezeka kwa idadi ya watu wanaozaliwa, na hiki ndicho Marekani wanaogopa sana ( africa's potential for population growth)
 
Tena kwa wanaume inaweza ikawekwa insuch a way kwamba haionekani hadi uume usimame, kwahiyo haitamzuia kuoga na wenzake kama ni anaishi bwenini
Hii itapendeza sana kwa sisi tusio na VVU ila wenye VVU wataandamana mchana kweupe.
Utawasikia sisi tunapigania haki za binadamu si kwamba tuna UKIMWI. Ukimwona mtu kashika bango kuandamana ujue ameukwaa
 
Hii itapendeza sana kwa sisi tusio na VVU ila wenye VVU wataandamana mchana kweupe.
Utawasikia sisi tunapigania haki za binadamu si kwamba tuna UKIMWI. Ukimwona mtu kashika bango kuandamana ujue ameukwaa
Ndio maana nikasema anahitajika jasiri kutekeleza hili, kiongozi lege lege sio rahisi. Mimi kama nikigombea uongozi hii ndio itakuwa ajenda yangu ya kuombea kura
 
Namkijidai kuukaushia uzi na mimi ndio nitazidi kukomaa sasa.., kuchungulia na kukimbia bila kuchangia chochote sio utaarabu, tuwekani wazi, vikwazo ni vipi, how do we overcome them.., lengo ni tz iwe huru na matumizi ya mpira na VVU kwa ujumla.., nafikiria jinsi maisha kabla ya VVU yalivyokuwa.., watu walikuwa wanajipigia tu bila presha yoyote, we need those old days back!
 
HIV ni kirusi kilicho tengenezwa kwa special purpose.
Na wajinga wote watauliwa nacho kwa kukosa busara.
 
HIV ni kirusi kilicho tengenezwa kwa special purpose.
Na wajinga wote watauliwa nacho kwa kukosa busara.
Hata wewe mkeo anaweza akakuua pia.., je, huo ni ukosefu wa busara? Way foward ni hiyo niliyopendekeza hapo juu
 
Mpaka mwisho wa hii dunia hatutapata suluhisho; unless igunduliwe chanjo au dawa. Kinyime cha hapo dawa ni hiyo niliyowapa, ila mpango huu unahitaji dikteta kuufanikisha, Rais legelege hatoweza kamwe! Pia Airport pawekwe utaratibu wa wageni wote kupimwa VVU kabla ya kuingia nchini, AIDS should be treated like EBOLA! Mi nashangaaga tunabembeleza bembeleza nini na huku watu wanazidi kuambukizana kila kukicha, tena tunapeana dawa za kurefusha maisha (kurefusha muda wa kusambaza), this is shear insanity! Its madness!!
Hoja yako ingekuwa ya msingi sana iwapo ngono pekee ndio ingekuwa njia ya maambukizo,Maana halisi ya kuondoa unyanyapaa kwa waathirika ni kuwafanya waendelee kuwa ni sehemu ya jamii ambayo inawajibika kwao na wao wanawajibu wa kuilinda jamii hiyo.Ni rahisi sana kwa muuathirika wa ukimwi kuwa kama mbwa mwenye kichaa anapogundua jamii inamsimanga na kumtenga.Muhimu ni elimu iendelee kutolewa na raia tujiepushe na ngono ambazo si salama.
 
Francis pia Kama mke atakuletea vvu maanayake nikua ulikosa busara wakati unamchagua kua mkeo except kwa wale wanaopata kwa accident Kama wahudum wa afya na ajali zingine Kama za magari na kadhalika
 
ARV (waathirika wapate muda wa kutosh kuua wenzao kabla hawajafa)
Sasa mtu anakubalije kuuawa kizembe? Ukiondoa wachache sana wanaobakwa, mengine ni ya kujitakia. Yes. Kujitakia. Zamani enzi za ujana wangu nilikuwa nafanya uhuni na kuwatease baadhi ya mabinti. Unamwambia aisee tutumie condom au tusitumie? Unajibiwa " wewee tuu". Huu si uhayawani huu?
 
Back
Top Bottom