Pole sana.
Kama unaishi Dar, nenda soko la Kariakoo upande ulipo mlango mkuu kila siku wakati wa jioni huwa kuna watu
wanaleta dawa za asili.
Baada ya kufika utaona kibanda kwa maana ya turubai ambalo limezungushiwa pande Tano, juu na pande zote nne
tofauti na vibanda vingine.
Hao jamaa ni wakenya wameweka loud speaker nje wamebandika tangazo ambalo linawatambulisha kwa jina la
Mega herbs 'N' nutrition.
Hao jamaa wanajitahidi kwani kabla ya kukupa dawa wanakupima kwa mashine iitwayo 'Quantum Analizer' ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mengi hata ambayo dalili zake bado hazijaonekana. Pia wanazo dawa za kuaminika.
Sababu ya kukupa ushauri huo, ni kwamba kuna vitu vingi ambavyo vinasababisha hali hiyo badala ya kukutajia dawa
ambayo ilimsaidia mtu mwingine ni bora kwanza ukapate vipimo. Wenyewe wanadai kupima ni bure lakini ni lazima
kujiandikisha kwa shilingi 5,000/-.
Nakutakia mafanikio mema, uende na upone haraka !.