Napinga ACT-Wazalendo kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) huko Zanzibar

Umechelewa kwani wameshajiunga na SUK
 
Unajisi mtupu! Zto alitaka "kumpindua" Mbowe kwa kutaka madaraka-uenyekiti, hivyo kwa hili waliloliamua, sishangai katu!
Just imagine Zitto ndio angekuwa mwenyekiti wa chadema

Sio chadema muda huu ingekuwa wapi ?[emoji1787][emoji1]

Zitto Ni ndumi la kuwili[emoji1787][emoji1787]
 
walichofanya ACT wananikumbusha enzi za shule, mnaazimia kwa pamoja kugoma bt badae wenzenu wanajitoa mnabaki kuzagaa tu, hapa naona ngoma nzito imebaki kwa chadema.
HalAfu FFU wanakuja kuwapiga virungu
 
Wanashiriki kwenye serikali wakati makamo wa rais wa kwanza hana meno yoyote ya kuiambia serikali wala act hawana wawakilishi wakuweza kubadilisha sheria yoyote ile sasa wanashiriki kwa manufaa ya nani
 
Pale mnafiki anapojifanya yeye ni mtu mwema!
 
Kwani Pascal Njaa anasemaje? Naona atakuwa kafurahi mpaka jino la 32 linaonekana .
 
Sasa je watumie njia gani mbadala ?
 
Wewe unawashwa na nini kwenye hili., wanasema Wazanzibari majority wamebariki GNU wew na utanganyika wako ata uandike kurasa ngap itasaidia nini, siasa za Zanzibar ni tofauti sana na huko kwen
 
Wewe unawashwa na nini kwenye hili., wanasema Wazanzibari majority wamebariki GNU wew na utanganyika wako ata uandike kurasa ngap itasaidia nini, siasa za Zanzibar ni tofauti sana na huko kwen
Sasa mbona wakiuawa wanatangaza mpaka huku Tanganyika?
 
Rekodi yake ya unafiki inajulikana huyu.
Mimi nadhani kwenye hili itakuwa hamumtendei haki. Huyu bwana amefanya juhudi kubwa ili Watanzania wamkubali tena kama mpinzani makini. Kwa sababu hiyo sidhani kama atachangamkia msimamo wenye tija zaidi Zanzibar kuliko Bara. Mpaka sasa sioni Zitto kama Zitto anafaidika vipi kutokana na haya makubaliano zaidi ya kuzidi kukosa credibility.

Amandla...
 
Reactions: BAK
Nakubaliana na yote uliyoyaandika. Siku chache kule Twitter Zitto alitoa kauli kwamba hawawezi kushirikiana na wauaji. Nimeitafuta hiyo clip kule Twitter siioni. Wamekusanya ushahidi mbali mbali kupeleka katika taasisi mbali mbali za Kimataifa ikiwemo ICC Na UNHCR halafu kuwashtaki maccm na udhalimu wao wa kutisha halafu hata vyombo husika havitajoa kauli yoyote ile unageuka nyuma na kushirikiana na huyo uliyemshtaki!!! Ni akili kweli hiyo? Wana nia hawa ya kuleta mabadiliko ya kweli au ni waganga njaa? UNAFIKI ni kitu kibaya sana.
 
Hata ukipinga haitakusaidia mama, pamoja na maumivu makali amabyo wanachama wamepitia wakati wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha, kupigwa, kuwekwa ndani, kuumizwa na kujeruhiwa kwa kila namna, nimebaki mdomo wazi kupna Act wanaunga mkono udhalimu huo ikiwa bado watu wapo kwenye misiba na maumivu, wengine wapi hospitali na wamekua vilema

Zitto kweli wewe ni msaliti na hupaswi kuaminika
 
Pamoja na jitihada za wakina Nondo hapa wakina Zitto wamekabidhi chama kwa CUF ya zamani.
Nisichokielewa ni nini ACT-WAZALENDO Zanzibar watakachopata kutokana SUK.

Mimi ningewaelewa kama wangesema kuwa wamekubali kuingia kwenye SUK baada ya serikali iliyopo kukubali kufanyia kazi malalamiko yao. Na waseme hivyo akiwepo mwakilishi wa serikali.

Lakini hii ya kuamini kuwa watatoa presha kwa sababu Maalim atakuwa Makamu na watakuwa na mawaziri watatu na wawakilishi wanne wala haiingii kichwani.

Wameishajionyesha kuwa si watu wa msimamo kwa hiyo hamna gharama yoyote katika kuwapuuza. Mimi nadhani wangegawana fito ili wakina Zitto waweze kujitenga na mambo ya Zanzibar ili waendeleze mapambano yao huku Bara.

Amandla...
 
πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½
Pamoja na jitihada za wakina Nondo hapa wakina Zitto wamekabidhi chama kwa CUF ya zamani. Nisichokielewa ni nini ACT-WAZALENDO Zanzibar watakachopata kutokana SUK....
 
Unapinga kama nani wewe? Nyinyi ndio munatumiliwa na CCM kuleta mawazo mbadala hapa jf kuwachanganya watu ili munufaike hizo buku 7., issue ya maalim seif anasema wao wamepata ridhaa kutoka kwa wananchi wao sasa ulitaka nini tena na wananchi ndio mtaji kwa wanasiasa? Chama kinaangalia option nyengine mbadala 2025 vipi wataikabili ccm labda na wao wakiwa madarakani. mara hii ndo mushaona walifanya watakavyo hakuna kura hata moja iliyotoka kituoni matokeo yote yamepikwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…