Napinga ACT-Wazalendo kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) huko Zanzibar

Masahihisho : Mimi siyo ccm na sijawahi kuwa kwenye kundi la buku 7 fc
 
Unaweza kuta Zitto kazidiwa nguvu na wakina Maalim.

Amandla...
Siyo kama ''unaweza kukuta'' bali haya ni maamuzi ya Maalim Seif. Wengine wametumika kupiga rubber stamp tu. Nadhani Maalim ameona kuwa mwaka 2025 hatakuwa na nguvu za kugombea tena akaona akubali tu kuchukuwa ''pension'' yake ya kisiasa. Tatizo kubwa (kwa mpinzani yoyote Tanzania) ni kuwa wananchi hawajitokeza inapopaswa, kwa ajili ya woga. Na siku hizi kutegemea tu wahisani haisadii kwani wahisani hawawezi ku-act inavyotakiwa bila wananchi kukinukisha. Mfano ni Kenya. Kama wasingejitokeza ule uchaguzi enzi Mwai Kibaki alivyochakachua mpaka leo pengine wasingekuwa na katiba mpya. Maalim atakuwa amepiga hesabu na kuona mwaka 2015 walivyogeuza matokeo bila aibu na hakuna kilichofanyika. Akaona hata kipindi hiki kama asikubali angalau afaidi basi hakuna siku atakuja kupata tena.
 

Mkuu. Wewe Ni mrs Keyboard. Huna lolote. Hujui hata wananchi wtz wanataka nini. Unawaza zaidi uhalali wako wa kuandika hapa kuliko maisha ya mtz. Kwako hata kwetu upareni wakipata barabara huwezi sifia ila ikibomoka utaandika. Pole sana.
 
Loser!
Hakuna wa kukusikiliza,hata chadema wako watawasamehe wabunge wake 19
Ninyi ni wasanii tu mnakataza watu wasuse lakini mna mbunge na madiwani waliotokana na chaguzi hizo hizo lakini mmewauhusu waape.
 
Mh Mambo ya siasa bhana.Sefu amegudua kuwa mda unampa kono sasa hakuna namna.
 
Mh Jussa nimekuona ulivyotiwa ulemavu , Machozi yamenitoka ! Mungu akuinue tena
 
Dhambi kuu iliyotendeka ni kuwaambia Wazanzibar waingie mtaani kuandamana baada ya wizi wa kura uliokithiri. Watu wakateswa na wengine kuuawa, ushahidi upo.

Baada ya muda unakuja na kukana kuwa yaliyofanywa na dola si haramu. Hivyo, tunaingia kwenye SUK na kuanza kuiponya Zanzibar.

Huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine. Watu walidhurumiwa hali zao za kikatiba, pia ikiwemo haki ya uhai.

Mungu ni Mkuu na mwenye maajabu sana. Hakuacha hili lipite bure. Na laana hii itapita na wengi.

Naomba wajiandae kisaikolojia kuanzia sasa.
 
Yaliyopita yamepita. Isitoshe hata Magulifu aliwahi kumshangaa Dr Shein kwa kuendelea kugharamia matibabu ya Seif wakati Seif analeta upinzani kwenye serikali, cha ajabu mwisho wa siku wote wamekutana tena Chato.
 
Mwenyezi Mungu Mkubwa Mkuu. Huyu jamaa nilipoteza imani naye tangu alipoanza usaliti ndani ya Chadema. Pamoja na kuwa aliomba samahani hapa jamvini JF kwa kuanzisha uzi lakini baadaye akataka ufutwe na ukafutwa kwa sababu aliulizwa maswali mengi kuhusu hiyo samahani yake FEKI aliyoshindwa kuyajibu. Once A TRAITOR ALWAYS …..

Hakika Zitto kiukweli hayupo kabisa
 
Tulionya Mapema sana , lakini tulipuuzwa , Sasa leo ACT mnamlilia nani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…