Napinga Daladala kuingizwa kwenye BRT

Kuna jamaa waliwahi kusema Kuwa hizo Engine za hayo mabasi hazina vipuri na ni ngumu kutengenezeka. Leo NDIO yamejidhihirishal, mtaalam Bujibuji Simba Nyamaume weka Neno hapa
 
 

Attachments

  • E09181C1-3B6C-45A5-8689-386351A90280.jpeg
    73.2 KB · Views: 1
Sasa daladala 15 zitasaidia nini kwa lile nyomi la Kimara-Kivukoni au Kimara-Gerezani?
Wanatest zali mtapiga kelele kiasi Gani, wakiona kimyaaa basi NDIO imetoka hio.

Mfumo wa Miundo mbinu hausapoti daladala labda zigeuzwe MILANGO hala zifungwe Spring na tairi kubwa hahaha ili ziweze kuendana na vile vituo
 
Mgonjwa yupo ICU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kula mijihela ndiyo wanachoweza hawa
Kusimamia na kuendesha miradi hawawezi

Ova
 
Sure mkuu 🤝
 
Hahahahaha [emoji1787]
Ule mradi wao wanaungangania kuendesha wakati wao kuendesha
Hawawezi na hawatokuja kuweza kuendesha...wampe tu mwekezaji/mtu binafsi tu
wao wanachoweza ni kuchota mijihela na kula basi

Ova
 
Ni waziri wako wa uchukuzi lakini 😆
Sasa mabasi ya BRT yamezidiwa na abiria, cha kufanya ni kuruhusu daladala tu kwenye route hizo hakuna jinsi, kwani asubuhi/jioni watu wanapata shida sana.
Kwahiyo wewe unaamini kwamba tuna Bilioni 75 za kulipa kesi ila hatuna pesa ya kununua / Kukarabati mabasi ya mwendokasi?!
 
Hiyo mwendo kasi ni sikio la kufa. Gari inaweza toka Kimara mpaka Jangwani ipo tupu inarudi yard. Kwa akili za kawaida kibiashara inategemewa ibebe walau abiria wanaoshukia njiani mpaka Jangwani lakini inawapita abiria vituo vyote mpaka inafika Jangwani. Watu wameshatoa sana maoni ya maana hapa JF na mpaka wao wenyewe walikuja wakafungua uzi wao hapa lakini hakuna hata ushauri moja waliotekeleza kwa nini kampuni isife?

Serikali iruhusu wafanya biashara wenye uwezo na uzoefu kwenye sekta ya usafiri kama Bakheresa, Abood, Shabiby na wengineo wapewe baadhi ya ruti kwa mfano Bakharesa unampa ruti ya Mbezi - Kariakoo na Abood unampa ruti ya Mbezi - Feri tu hakuna kusimama mahali. Hapa kati anabaki mwendokasi na mabasi yake mabovu ndio akili za kibiashara zitawakaa.

Serikali kama ina nia kweli ya kuondoa tatizo la usafiri kwa watu wa Dar iruhusu usafiri walau coaster chache zenye AC level seat ila waruhusiwe kuongeza nauli kidogo kwa mfano Kimara - Posta nauli iwe 1,500. Mwenye uwezo wa kupanda dala dala apande, mwenye uwezo wa kupanda coaster apande na hata mwenye uwezo wa kupanda mwendokasi apande. Ikumbukwe kuwa sasa hivi coaster nyingi zile zilizokuwa zinasafiri kwenda mikoani usiku maarufu kama hakuna kulala hazina kazi baada ya mabasi makubwa kuruhusiwa kusafiri usiku.

Ni mtizamo tu.
 
Viraka.?
Kweli bongo ni ya michongo Hizo daladala tenda yake imetangazwa wapi!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…