Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza masuala ya Law school, ikiwemo wanafunzi wengi kufeli mitihani, anapaswa kuwa mtu Muungwana, Mtulivu, Msikivu na asiye na makuu, anapaswa kuwa mkweli, Mwakyembe hana sifa hizi.
Napinga uteuzi wa Harisson Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume hii kwa vile Haaminiki, si mkweli na ni mpenda sifa.
Kwa mfano, alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge kuchunguza Richmond, katika Taarifa yake aliyoisoma bungeni ALIFICHA BAADHI YA TAARIFA ILI KUOKOA SERIKALI, maana yake ni kwamba alificha taarifa za Mhusika Mkuu wa Jambo lile na kuangushia jumba bovu wasiohusika, leo huyu awezaje kuaminika na kukabidhiwa tume nyingine? JE, SAFARI HII HATOFICHA TAARIFA ILI KUIOKOA SERIKALI?
Mwakyembe akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kupitia CCM, aliwaahidi watu wa Jimbo lake kwamba AMEPATA SOKO LA UHAKIKA LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI (ikumbukwe kwamba mchele wa Kyela ndio unaoongoza kwa utamu duniani)
Lakini hadi anang'olewa kwenye ubunge hakuwahi kusaidia hata kilo 10 za mchele wa Kyela kuuzwa Marekani, Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa kuongoza tume yoyote ile.
UNAPODANGANYA NYUMBANI KWENU HUWEZI KUAMINIKA UGENINI.
Harrison Mwakyembe ni mtu aliyejaa dharau kubwa sana , huyu hawezi kuwatendea haki watu wenye digrii moja wanaopigania haki yao ya matokeo.
ALIWAHI KUKATAA MASWALI KWAO KYELA kwa kisingizio kwamba wanaomhoji ni Darasa la 7, wakati yeye anamiliki digrii 4 na kwamba watu wasio na elimu wanachopaswa kumhoji ni kuhusu kama hawana hela mifukoni mwao na labda awasaidie. Huyu hafai kuongoza Tume ya kufuatilia haki popote duniani.
Tunamuomba Waziri wa Sheria ATENGUE HARAKA UTEUZI WAKE.
NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO.