Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Naona kuna watu hapa akiwemo Paschal wanajifanya kujua utaratibu kuliko walitengeneza utaratibu.

Duniani kote sidhani kama kuna nchi inaweza kuwa na utaratibu wa kijinga kisa kero kwa mwananchi kufika kwake NO!.

Basi airport nayo ijengwe kila wilaya au mnataka kukuza mjadala tu hapa kisa Amos Makala..!

Tufanye kwa big city as Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya (toa Dar) bus zinashushia wapi?, miji midogo as iringa au musoma basi zinashushia wapi?.

Na unapoongelea nchi nyingine siyo la kulinganisha na tz hata kidogo, mfamo j'berg au Nairobi kuna stendi kuu ya mabasi?.

Kuna sheria/utaratibu uliopo kwa miaka, labda turudi nyuma alafu tupate historia kidogo.

Kwa Dar miaka ya 198... stendi ilikuwa pale mnazi mmoja hata kisutu na mabasi karibia yote yalishushia pale hata yale ya kusini/mtwara, ndiposa kuja 1990 baadhi ya kampuni baada ya kuwa mabasi zaidi ya 5 daily wakaanza kujitafutia eneo binafsi.

Mfano Scandinavia terminal ilikuwa kamata, Saibaba kisutu. But now sababu ya ubungo ilikuwa ina tatizo na wamiliki kupewa ruhusa kuwa na terminal nje mkaona ndiyo utaratibu NO!.

Kwa upande wa historia, tunafahamu uwepo wa stendi kuu ya mabasi ni uwezekano wa abilia kutoka popote nje na ndani ya nchi kuwa na uhakika akifika pale kupata usafiri, pia basi karibia zote kupatikana eneo moja badala kila mtu kuweka kituo sijui mabwepande, mbagara, usariver, Nyegezi, nyakato, magomeni, uyole, bunju nk.

👉🏾Siyo sawa tuache unafiki.
 
huyu MAKALA atakuwa mkuu wa mkoa alietumikia muda mfupi sana Dar es Salaam.

yaani naishi Tabata kuna option ya kushushiwa Ubungo unanilazimisha nishushiwe huko porini Mbezi ili iweje?

Mtu ambae hakupitia shida kwa maana ameikuta mali kwa wazazi wake bila kuitolea jasho ni ngumu mno kuona changamoto/tabu wanazopitia wengine....hivi vyeo wangelikua wanapewa waliopitia changamoto/tabu kwenye maisha yao.
 
Kwa sasa ungetumika utaratibu kama zamani kutumia stendi zilizopo,ila kama mabasi yanayosafirisha abiria kupitia Morogoro Road yapitie kituo hicho lakini yasilazimike kuanzia hapo safari. Hadi itakapoletwa mpango wenye tija.
 
Hatupingi Stendi kuwa Mbezi , bali utaratibu mpya wa Makalla ndio unaopingwa
 
Hakuna soko lisilokuwa na Mwendawazimu. Tanzania yapo masoko mengi tu na baadhi ya Masoko hayo ni:

1. Bunge
2. RC's
3. DC's
4. Cabinet Ministers
5.
 
Kazi kubwa ya stendi ni mabasi kushusha na kupakiza abiria karibia na mahali wanapoenda au kuishi sio huo ugoro mwingine wa ziada unaouzungumizia wewe.

Yani mtu anaongea tu lakini hawafikirii na wengine..sijui mshkaji ana kibiashara chake pale stand akaona tutamharibia! Anajua yeye....
 
Hili ni gumu kutekelezeka kwa sasa na litaleta usumbufu kwa baadhi ya abiria na kujikuta wanaingia gharama zisizo za lazima.
 
Nilikutaga mamantilie anasukuma chapati kwenye veranda ya Mwanza Hotel,,ndo nikajua kumbe tuko choo cha kike..
Siyo hiyo tu...nenda hapo pembezoni mwa IFM uone walivyochafua barabara. Yaani wao hawatozwi kitu alafu miundombinu wanazochafua utozwe kwenye mafuta yako ya petroli.
 
Hatupingi Stendi kuwa Mbezi , bali utaratibu mpya wa Makalla ndio unaopingwa
Soma mpaka mwisho comrade.

Huo siyo utaratibu wa Amos bali ni Transportation contract regulations kuwa bus lako linaanzia stand kuu na kuishia stendi kuu.

Nipe picha ya kila mmiliki kuwa na kituo chake as kenya wanavyofanya ni mantanange aseee!.
☝🏾
Nilipata usumbufu sana kupata basi nilipokuwa nataka kulekea Eldoret huko kenya kisa hakuna stend maalum.
 
Umemaliza. Agizo lake halina afya kwa wananchi. Serikali ilenge kurahisisha maoshanya watu wake si kuwakwaza.
 
Wewe ndio Kilaza mkubwa. Unafikiri kila kitu kinachofaa Mwanza, Arusha au Mbeya kitafaa Dar es Salaam. Dar es salaam ni Dar es Salaam na hayo majiji mengine ni hayo. Binadamu mwenye akili njema anajifunza kwa wenzake kisha anaongezea na ubunifu wake kulingana na mahitaji ya mazingira yake.
 
Huwezi kuwelewa hata wanachokitafuta ni kipi kwa sababu abiria anayetoka stendi halipi ushuru wowote !
 
Hilo li stand badala ya kuwapa wananchi ahueni ndiyo kabisaa limeleta karaha...

Yaani ukiwa unasafiri mkoani uamke saa 9 mida ya wanga...si adhabu tosha hiyo.

Sasa badala ya kuruhusu mabasi kituounguzia adha hii huyo mwana CCM eti anapiga biti.
 
Naona kama unatudanganya sasa. Tutajie kifungu cha hiyo 'Transportation Contract Regulations' inayo specify exactly wapi basi lako litaanzia na kuishia safari zake. Unataka kutuambia mabasi yote yaliyokuwa yakianzia safari zao Tandika na Shekilango walikuwa wanakiuka taratibu na serikali ilikuwa inawaangalia tu?

Hamna mtu aliyesema kuwa kila mmiliki awe na terminal yake, kama ilivyokuwa kwa Scandindavia ( ambae alitumia terminal ya Kamata) na hao wa sasa waliowekeza Shekilango. Kama sheria kama hiyo ipo basi Manispaa husika zilikosea kuwapa vibali vya ujenzi katika maeneo hayo.

Kutokujua basi lako linapotokea mjini Nairobi ni uzembe wako na sio wa wenye mabasi. Hasa huu wakati wa simu janja ambapo unaweza ku google basi litatokea wapi na kujipanga ipasavyo. Aidha, ukienda katika stendi yeyote utaelekezwa mabasi unayo hitaji yanaanzia wapi. Hapo zamani ilikuwa ukienda Ubungo wakati unataka kwenda Lindi utaambiwa uende Tandika. Ukikazania kwenda Kariakoo kulitafuta basi itakuwa ni uzembe wako.

Sisi ambao unatuona kama vile hamnazo tunahoji ulazima wa kuwa na kituo kimoja cha mabasi yeyote katika mazingira yafuatayo:
1. Kituo kinachopendekezwa hakiwezi kutoa huduma hiyo kwa miaka michache ijayo.
2. Miundo mbinu ya kuwafanya watu waweze kufika na kutoka hapo kwa urahisi haitoshelezi. Mnazi Mmoja inayozungumziwa na wengine ilikuwa inafikika kirahisi kutokana na ukaribu wake na Kariakoo, hivyo hivyo kwa Kisutu.
3. Upatikanaji wa huduma za watu kuweza kulala stendi wakisubiri usafiri.

Ukweli ni kuwa kituo kimejengwa bila tathmini ya kutosha ya mahitaji ya watu wanaotumia usafiri wa mabasi ya kawaida. Ni kama vile kujenga soko kwa mfano wa Mlimani City, hayatalipa.

Watawala wangeachia utaratibu uliopo uendelee wakati wakiboresha miundo mbinu ya kuwafikisha na kuwatoa abiria kwenye kituo hicho na vingine vilivyopo. Ni mawazo potofu kuvunja masoko yaliyo jirani na makazi ya watu na kuyahamisha kusiko na watu kwa kutegemea watu watapanda dala dala kwenda kununua tungule. Watarudi tu kufuata wateja.

Amandla...
 
Nilikutaga mamantilie anasukuma chapati kwenye veranda ya Mwanza Hotel,,ndo nikajua kumbe tuko choo cha kike..

Aisee 🤣🤣🤣 kama uko vizuri ni heri ukale hotel ya maana hata kama bei zao ziko juu sawa tu....afya muhimu mno kuliko pesa
 
Tukiendelea kuunga mkono kila linalosemwa na viongozi..kuna siku mtu atasema ikulu ya Magogoni ibomolewe ikajengwe Mbagala na tutakubaliana nae..yaan mimi nakaa Ubungo niache kupandia Kilimanjaro Express Urafiki(garage yao) nilifuate mpaka Mbezi huo si utwana sasa
 
Je, abiria wote hawa wapandao ndege wanakula na kunywa na kufanya shopping hapo airport kwenye restaurants na mini supermakets zilizopo hapo?

Kwangu makalla ana weak point. Na si kila abiria ana budget ya kula. Anapaswa kulitambua hilo. Abiria wanafuata unafuu wa usafiri na wenye magari wanaangalia kila siku namna ya kufikisha huduma bora kwa abiria wao. Lengo lake yeye ni kuwakomoa abiria na wenye magari pasipo kiangalia uhalisia. Mbona hizi mini terminals zilishakuwepo kabla hata ya ubungo terminal haijahamishiwa huko mbezi... mihemko ili kutafuta sifa haifai

Furthermore, watu wanapata ajira pia kqa hizi ofisi ndogo ndogo, kodi ya pango inapatikana, serikali inapata kodi pia. Mbona viongozi wetu hawapendi kufikiria zaidi? Pia tunastimulate vibiashara maeneo husika ya hizi ofisi. Kampuni zina mabasi kadha wa kadha. Mengine yataanzia huko mbezi na mengine yatawafata abiria wao wanakopatikana bila kukomoana.
 
Watu wa mipango miji hawajui wanachokifanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…