Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Weakman

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2021
Posts
995
Reaction score
1,607
Ndio, napinga!,

Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!

Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.

Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.

Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!

Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!

Kwa Wakristo ipo wazi;

"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"

Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.

"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"

Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?

"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"

Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.

Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?

"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"

Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.

Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.

Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.

Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.

Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,

Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.

Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!

Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!

Ikumbukwe dunia imebadilika.

Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.

Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.

Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.

Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?

Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.

What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?

Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!

Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"

Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.

Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!

Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?

Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?

Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!

Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?

Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.

Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!

Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.

Mume akifa unadai urithi wa mali zote!

Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hata mimi napinga ndiyo maana hata nikienda bar dem yoyote akiniomba nimnunulie bia moja hata awe mzuri vipi huwa najibu "Wewe umeninunulia ngapi?" Huku nimeweka uso wa Vladimir Putin. Wanazoea vibaya kupewa pewa tu na wanaona kama ni haki yao vile.
 
Ni kweli...

Sera ya usawa wa kijinsia haiendani na sheria ya ndoa inayotaka mwanaume awe provider.

Sera ya Usawa ililenga kumtetea mwanamke lakini kinyume chake inamuumiza kwa sababu imetengeneza derby kati yake na mwanaume hivyo wanawake wamekuwa na stress na frustration inayotokana na mfumo kuwanyisha kazi ngumu, kutokuolewa kutakana na midomo yao ya ushindani, nk
 
Kwa nini ukamtwae nyumbani mwa wazazi wake, kama huwezi ama hutaki kumtunza?

Kwao alikuwa anakula na kuvishwa vizuri hadi siku ulivyomtia maneno maneno yako ya ushawishi hadi akakubali kuishi na wewe.

Mwanaume anayekwepa majukumu yake, hana sifa za kuitwa mwanaume. Shame on you!
 
Unamaanisha usaidiane na mkeo kutunza familia bro au sio......
Kataa ndoa wanazidi kujifunua nini kipo nyuma ya movement zao. Ugumu wa maisha. Si unaona kijana anakimbia jukumu lake anataka alelewe.

Wenzake tupo kwenye ndoa mwaka 20 sasa na mke wangu ni mama wa nyumbani, simruhusu afanye kazi yoyote zaidi ya kunipikia, kunifulia, kulea watoto na kunipokea toka kazini na kunipa haki yangu. Baba nawajibuka kwa kila.kitu chake.

Huo ndio uanaume na sio hizo sarakasi na ndio maana vijana sasa wananyanyasika kwe ye ndoa sababu na kupenda kubebwa na wanawake.
 
Kwa nini ukamtwae nyumbani mwa wazazi wake, kama huwezi ama hutaki kumtunza?

Alikuwa anakula na kulishwa kwao vizuri hadi siku ulivyomtia maneno ya ushawishi hadi akakubali kuishi na wewe.

Mwanaume anayekwepa majukumu yake, hana sifa za kuitwa mwanaume. Shame on you!
Ndio kataa ndoa hao eti mwanamke atanufaika kwa jasho lake. Hiyo yote inatokana na umaskini, mwanume inatakiwa ujivunie kusimamia na kuprovide kwenye familia yako.

Binafsi najivunia kuwa Baba bora kwa watoto 4 na mme bora kwa mke wangu. Nahakikisha wanakula, wanavaa, wanasoma vizuri, wanapata matibabu sahihi pia kusaidia familia zetu kwa ujumla.
 
Ulikuwa hujui,
Unauliza Kama mtoto!
Kuwa wewe binti!
Ulidhani mke ni mtoto wa kwanza wa mume?
Kwahio unalilia 50/50 ya Nini?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Wait shemegi, huu usaidizi uanzie kwenye mahari....hapa napo mwanaume bado ana mzigo, walau mahari ya 1m mfano me atoe laki 6 ke laki 4.

Tunahitaji ndoa imara zilizojengwa katika misingi ya kusaidiana. Au???
 
Vijana shupavu hao,kazi ni kubwa sana inakuja mbele yenu.

Wewe nakumbuka kuna sehemu umeni-diss kwamba mimi sina akili na ni kwenye mada hizi hizi za ndoa,sasa kama wewe mwenye akili ndiyo huyu unaewaza umtie mkeo mimba azae then apeleke mwanao shule sijui nani atakuwa akili hana.
 
Back
Top Bottom