The Worst
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 6,108
- 21,140
Wewe una utajiri gani hadi sasa ulioupata kwenye ndoa?fafanua na wenzako wachangamkie fursaNdoa ni kichaka cha mwanamke kujitajirisha.... Kataaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe una utajiri gani hadi sasa ulioupata kwenye ndoa?fafanua na wenzako wachangamkie fursaNdoa ni kichaka cha mwanamke kujitajirisha.... Kataaa
Sina ndoa mkuu ndio napambana kutafuta mchumbaWewe una utajiri gani hadi sasa ulioupata kwenye ndoa?fafanua na wenzako wachangamkie fursa
Be a gentleman,achana na wamarekani 50/50 haipoNdio, napinga!,
Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!
Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto Kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.
Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.
Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu Hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!
Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi?
Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?
Katika ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!
Kwa wakristo ipo wazi;
"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"
Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.
"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"
Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?
"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"
Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa Raha na shida Hadi kifo kiwatenganishe.
Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?
" Mwanamke amtii mumewe na Mwanaume ampende mkewe"
Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na Mali mbele ya mumewe.
Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao
Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa katoliki, nyakati za mtume Mohammed Hadi leo, Mume na mke wameshirikiana katika kazi
Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.
Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,
Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata ridhiki ya maisha yao
Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!
Vipi wewe Leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!
Ikumbukwe dunia imebadilika.
Kwa Sasa uchumi hauna mwenyewe Tena.
Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.
Leo hii mke aweza kuwa waziri au Raisi na akapata mamilioni ya fedha.
Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?
Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.
What if mtu Kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako Afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?
Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!
Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata Kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, " we mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati Mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"
Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.
Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa Ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya Ng'ombe!
Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!
Kwani Kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?
Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya Mume Ni Provider, mumetumia msingi gani wa Elimu?
Hapana, Mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda Kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!
Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?
Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.
Bahati mbaya cheo hiki alishapewa Mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na Neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!
Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.
Mume akifa unadai urithi wa Mali zote!
Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni Sana!
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mwenyewe anajiita Weakman masikiniBe a gentleman,achana na wamarekani 50/50 haipo
Ukiya-check hata maisha ya Bi mkubwa wako unamuona ana chochote alichokivuna kwenye ndoa zaidi yenu nyie watoto?Sina ndoa mkuu ndio napambana kutafuta mchumba
Amerithi jina lakeMwenyewe anajiita Weakman masikini
Mume atawaacha wazazi na mke atawaacha wazazi!Kwa nini ukamtwae nyumbani mwa wazazi wake, kama huwezi ama hutaki kumtunza?
Kwao alikuwa anakula na kuvishwa vizuri hadi siku ulivyomtia maneno maneno yako ya ushawishi hadi akakubali kuishi na wewe.
Mwanaume anayekwepa majukumu yake, hana sifa za kuitwa mwanaume. Shame on you!
Kachuma mali 😹Ukiya-check hata maisha ya Bi mkubwa wako unamuona ana chochote alichokivuna kwenye ndoa zaidi yenu nyie watoto?
Mke atakaeolewa na huyu bwana mdogo atapata shida sana,kwanza ni mgumu kuelewa kingine ni mbishi.Mwenyewe anajiita Weakman masikini
No matter what,a man is a man Wacha kuwa legelege iba pora wewe ndio Kichwa Cha familyLeo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.
What if mtu Kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako Afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?
Stress mambo magumu, mke anakuja kumuongezea mzigo, kuishi peke ake ishu.... Mie namuelewaMke atakaeolewa na huyu bwana mdogo atapata shida sana,kwanza ni mgumu kuelewa kingine ni mbishi.
Umasikini unawasumbua. Wanajitafutiza vijana.Stress mambo magumu, mke anakuja kumuongezea mzigo, kuishi peke ake ishu.... Mie namuelewa
Haina ubaya kudesign mfumo unaoutaka!Kataa ndoa wanazidi kujifunua nini kipo nyuma ya movement zao. Ugumu wa maisha. Si unaona kijana anakimbia jukumu lake anataka alelewe.
Wenzake tupo kwenye ndoa mwaka 20 sasa na mke wangu ni mama wa nyumbani, simruhusu afanye kazi yoyote zaidi ya kunipikia, kunifulia, kulea watoto na kunipokea toka kazini na kunipa haki yangu. Baba nawajibuka kwa kila.kitu chake.
Huo ndio uanaume na sio hizo sarakasi na ndio maana vijana sasa wananyanyasika kwe ye ndoa sababu na kupenda kubebwa na wanawake.
NI UTAPELI NA ULAGHAIKataa ndoa Liverpool VPN
Kachuma mali kutoka kwenye mti au kutoka kwa mumewe ambaye anaishi nae kwenye jamii,huyo mumewe kipindi akitafuta mali ilitegemewa aje kupewa nani?Kachuma mali 😹
Nakazia sana hapaNdoa ni kichaka cha mwanamke kujitajirisha.... Kataaa
Mahari ifutwe!Wait shemegi, huu usaidizi uanzie kwenye mahari....hapa napo mwanaume bado ana mzigo, walau mahari ya 1m mfano me atoe laki 6 ke laki 4.
Tunahitaji ndoa imara zilizojengwa katika misingi ya kusaidiana. Au???
Ndio kujitajirisha 🤣🤣🤣Kachuma mali kutoka kwenye mti au kutoka kwa mumewe ambaye anaishi nae kwenye jamii,huyo mumewe kipindi akitafuta mali ilitegemewa aje kupewa nani?
Then kwanini udhani kazichuma kutoka kwa mumewe unadhani ilibidi apewe nani kama siyo yeye,yumkini mumewe alifariki so wangemzika na mali zake kama angekuwa hana mke?
Acha blah blah. Usipende kubebwa kwenye majukumu yako. Wajibu wako ni kutunza familia. Ndio maana majiliza humu kupigwa, kugongewa na kunyanyaswa na wanawake. Bi alfa male dogo.Haina ubaya kudesign mfumo unaoutaka!
Ila usilazimishe kuwa ndio mfumo wa kisheria
Sababu historia ya maisha ya mwanadamu haitambui hio system ya kumfungia mke ndani
Historia inatunesha maisha ya mume na mke ni ya kushikamana kwa Kila jambo kwa umoja tangu Karne nyingi zilizopita