Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Kwanini yeye afanywe kuwa special namna hiyo na sio mimi mwanaume?

Kwani mimi sinawaacha wazazi wangu?

Kuishi na sisi wanawake wanataka hata bila ushawishi wa maneno
Nyieeee mjue mnapitiliza???? Ndio maana siku hizi wanaume nanyie mnafanyiwa wanayofanyiwa wanawake.
 
Huo uwajibikaji uwe kwenye kutoa pesa tu au na mengine tutashirikiana?!!
Sawa nitakubali kuwajibika ila na wewe usiwe mkali nikiomba tuwajibike wote kwenye kufua, kupika na usafi wa nyumba. Sababu hata maandiko yanasema, “ Mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu” hapo naomba twende sawa.!!
Msiwe mnachagua vifungu vya kuwafurahisha na kuwalinda nyinyi…!!
 
Hata mimi napinga ndiyo maana hata nikienda bar dem yoyote akiniomba nimnunulie bia moja hata awe mzuri vipi huwa najibu "Wewe umeninunulia ngapi?" Huku nimeweka uso wa Vladimir Putin. Wanazoea vibaya kupewa pewa tu na wanaona kama ni haki yao vile.
😀😀😀😀 wakishavaa vimini vinavyoacha mapaja nje au vile vitop vya brazil vinavyoacha kitovu wazi basi wanafikiri wana haki ya kununuliwa bia, makange na kugharamiwa usafiri
 
Wait shemegi, huu usaidizi uanzie kwenye mahari....hapa napo mwanaume bado ana mzigo, walau mahari ya 1m mfano me atoe laki 6 ke laki 4.

Tunahitaji ndoa imara zilizojengwa katika misingi ya kusaidiana. Au???
😀😀😀😀😀
 
Huo uwajibikaji uwe kwenye kutoa pesa tu au na mengine tutashirikiana?!!
Sawa nitakubali kuwajibika ila na wewe usiwe mkali nikiomba tuwajibike wote kwenye kufua, kupika na usafi wa nyumba. Sababu hata maandiko yanasema, “ Mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu” hapo naomba twende sawa.!!
Msiwe mnachagua vifungu vya kuwafurahisha na kuwalinda nyinyi…!!
Mume atakula kwa jasho, wewe utakulaje?
Kama unataka Kula, lazima umpe sapoti kwa vyovyote unavyoweza pale mume anapopambana kutoa jasho, kwa maana wewe ni msaidizi wake
 
Kwanini yeye afanywe kuwa special namna hiyo na sio mimi mwanaume?

Kwani mimi sinawaacha wazazi wangu?

Kuishi na sisi wanawake wanataka hata bila ushawishi wa maneno
Uko sawa sana. Mwanamke ni spesho na pia ana privilej asizokuwanazo mwanaume. Ndivyo ilivyo kiasili, na wala haiwezi kubadilika.

Unadhani kwa nini Ukreni, mathalani, raia wanaokamatwa na kushurutishwa kwenda mstari wa mbele vitani ni jinsia ME na wala si KE?

Nadhani elimu ya sayansi jamii imekupita kushoto. Pole sana.

Sababu pekee niionayo ya mwanaume kutotambua huo uspesho wa mwanamke ni uvivu, kutopenda uwajibikaji, elimu duni, kutokamilika kiasili kama mwanaume (kasoro ya kimaumbile).
 
Nyie ndo mnafanya ndoa ziwe ngumu. Wewe kama hauko tayari kuhudumia na kupambania matumbo ya familia yako, usioe mwanangu. Endelea kusikiliza nyimbo ya bachelor ya Nay wa mitego.
Nilichoongea ndicho kilicho exist tangu Dunia ianze

Mume na mke wameshirikiana kwa kazi tangu enzi na enzi

Hili la kutaka mwanamke asishiriki kwenye ustawi wa familia ni geni ktk tasnia ya ndoa
 
What a weak man
Hongera kwa kulishwa na kuveshwa ukiwa umejikalia bila kumsapoti mume kwa lolote

Eva mwenyewe alishirikiana began kwa began na Adamu kulima ngano na kufuga kondoo kwa ustawi wa familia yao
 
Nilichoongea ndicho kilicho exist tangu Dunia ianze

Mume na mke wameshirikiana kwa kazi tangu enzi na enzi

Hili la kutaka mwanamke asishiriki kwenye ustawi wa familia ni geni ktk tasnia ya ndoa
Kushiriki anashiriki ila tayari kuna mipaka ilishachorwa kupitia kwenye division of labour kwenye societies. Hayo unayotaka wewe wafanye wanawake inabidi labda uunde dunia yako ili yatekelezwe.
 
Mume atakula kwa jasho, wewe utakulaje?
Kama unataka Kula, lazima umpe sapoti kwa vyovyote unavyoweza pale mume anapopambana kutoa jasho, kwa maana wewe ni msaidizi wake
Nitakula kupitia jasho lake, kwani kwenye kuzaa ananisaidia?? Halafu wanaume kwann mnakataa majukumu yenu ya asili ya kutunza familia?!!
Pesa ni sauti ya mamlaka kote duniani, sasa ukitaka pesa yangu iwajibike lazima na mamlaka niwe nayo. Huwezi kupigania kitu usichokihudumia
 
Kushiriki anashiriki ila tayari kuna mipaka ilishachorwa kupitia kwenye division of labour kwenye societies. Hayo unayotaka wewe wafanye wanawake inabidi labda uunde dunia yako ili yatekelezwe.
Mwambie huyo, anataka asaidiwe na sauti awe nayo. Hawa ndio wale wanaume wanyanyasaji wake zao wakashinde kutafutia watoto wenyewe wakashinde vilabuni
 
Wewe kibuyu, leo imekuwaje tumekaa upande mmoja kwenye hii mada..? Haha
Lazima mtoa mada atakuwa kibuyu zaidi yetu
 
Huo uwajibikaji uwe kwenye kutoa pesa tu au na mengine tutashirikiana?!!
Sawa nitakubali kuwajibika ila na wewe usiwe mkali nikiomba tuwajibike wote kwenye kufua, kupika na usafi wa nyumba. Sababu hata maandiko yanasema, “ Mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu” hapo naomba twende sawa.!!
Msiwe mnachagua vifungu vya kuwafurahisha na kuwalinda nyinyi…!!
wifi,,hayo ya usafi atakuwekea house girl usijal,,au atanunua mashine,,au robot Eunice ataletwa hapo,, kazana kuuza vijora uache kitu mezani
 
Wewe kibuyu, leo imekuwaje tumekaa upande mmoja kwenye hii mada..? Haha
Lazima mtoa mada atakuwa kibuyu zaidi yetu
Huyu zaidi ya kibuyu!! Mwanaume mzima na kengele zake anataka kusaidiwa pasu kwa pasu eti!! Hawa ndio wanasababisha wanawake wafanye vitu vya ovyo ili kusaidia familia, kwa maneno yake haya anaonekana sio muwajibikaji kabisaa.!!
 
Back
Top Bottom