Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

wacha kukurupuka mxiuuu 😂😂
Bora umenistua aisee!! 😂😂😂
Na mwenyewe hana wasiwasi kaonyesha alivyo weak km username yake
Subiri vijana wa hovyo wawajibike na mkewe ndio akili itamkaa vzr
 
Huyu zaidi ya kibuyu!! Mwanaume mzima na kengele zake anataka kusaidiwa pasu kwa pasu eti!! Hawa ndio wanasababisha wanawake wafanye vitu vya ovyo ili kusaidia familia, kwa maneno yake haya anaonekana sio muwajibikaji kabisaa.!!
Pasu kwa pasu imesemwa wapi?

Kama mke ana uchumi mkubwa afanye zaidi.

Kama mume ana uchumi mkubwa afanye zaidi.

Maisha Yako hivyo tangu enzi na enzi.

Mababu na mababu zetu wamesaidiana kazi na wake zao, nyie wadada wa Leo mujione special kwa lipi
Unadhani malkia Elizabeth anahudumiwa na mume wake?
Unadhani mke wa mfalme wa Oman anamsaidia mumewe gharama za maisha?
Status za mume na mke zitaonesha mfumo wao utakuwaje!
But si Sheria kwamba mume ni provider, sababu historia ya maisha haijatufundisha hivyo
 
Mke anaelezwa vizuri mithali 31!nenda kasome uelewe!

Mke mwema anaamka asubuhi na kumwagilia mizabibu,husuka na kupata mapato na mumewe humwamini!!

Huyo ndio mke wa kimaandiko!

Huyu mvivu anaetoa papuchi akidhani ni malipo ya matunzo ni kahaba aliechangamka sema ni site tu haendi!!

Mwanamke anaetegemea vya kupewa coz anatoa papuchi huyo ni kahaba na sera hizi za kileo zinafundisha wanawake kuwa makahaba ndani ya nyumba ya mwanamme!

Kasome vizuri uelewe!!Tangu enzi na enzi kina Dorkasi walisuka na kuuza mazulia hata walipokufa watu wakalia Hadi wakafufuliwa!

Hawa ke was Leo wanauza uchi ili wapate matunzo kwa mkataba uitwao ndoa za kileo!!!

Ukahaba umehamia majumbani,Ni bora wakaenda site ikajulikana kuwa wanauza uke!
Umemaliza
 
Bora umenistua aisee!! 😂😂😂
Na mwenyewe hana wasiwasi kaonyesha alivyo weak km username yake
Subiri vijana wa hovyo wawajibike na mkewe ndio akili itamkaa vzr
ole wao ataondoa hio weak atawapakia futa😂😂😂
 
Pasu kwa pasu imesemwa wapi?

Kama mke ana uchumi mkubwa afanye zaidi.

Kama mume ana uchumi mkubwa afanye zaidi.

Maisha Yako hivyo tangu enzi na enzi.

Mababu na mababu zetu wamesaidiana kazi na wake zao, nyie wadada wa Leo mujione special kwa lipi
Unadhani malkia Elizabeth anahudumiwa na mume wake?
Unadhani mke wa mfalme wa Oman anamsaidia mumewe gharama za maisha?
Status za mume na mke zitaonesha mfumo wao utakuwaje!
But si Sheria kwamba mume ni provider, sababu historia ya maisha haijatufundisha hivyo
Na wewe jitahidi uwe km wao ili uhudimiwe mkeo.!! Wao wameweza vipi wewe ushindwe??
 
Ndio, napinga!,

Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!

Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.

Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.

Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!

Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!

Kwa Wakristo ipo wazi;

"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"

Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.

"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"

Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?

"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"

Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.

Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?

"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"

Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.

Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.

Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.

Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.

Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,

Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.

Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!

Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!

Ikumbukwe dunia imebadilika.

Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.

Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.

Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.

Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?

Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.

What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?

Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!

Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"

Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.

Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!

Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?

Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?

Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!

Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?

Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.

Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!

Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.

Mume akifa unadai urithi wa mali zote!

Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Nimejaribu kukuelewa kwa upande wako, ila watu wakisema majukumu ,hawamaanishi majukumu ni yanafanana. Kila mwanaume huwa anaweka rules zake kwenye ndoa yake ambazo ni za ziada ,ila kuna majukumu ambayo ni universal kwa WANAUME ,na mwanaume ili uwe mwanaume lazima uwe PROVIDER,sisemi ufanye kila kitu ila yale ya msingi fanya, usije ukaja kuwa unalaumu watu.
 
Na wewe jitahidi uwe km wao ili uhudimiwe mkeo.!! Wao wameweza vipi wewe ushindwe??
Dunia haipo hivyo!
Dunia haitakuja kuwa na usawa
Mimi nikiwa hivyo, wapo wengine wengi hawatakuwa hivyo!
 
Moja wapo ya ujinga uliozaa umasikini mkubwa Afrika ni huu wa pesa ya mwanamke haihudumii familia.

Yani nchi masikini kama TZ ambako hakuna ajira, hakuna vibarua alafu jukumu la kugharamia mahitaji ya familia liwe la mtu mmoja, na mtegemee hiyo familia ikue kiuchumi bila baba kuwa na presha na magonjwa yanayosababishwa na msongo wa mawazo.

Kuna kakundi kadogo sana kanakoingiza pesa hapa Tanzania ila kanagharamia watoto, wanawake, wazee n.k. huu ni ujinga hatuwezi kukua kiuchumi kwa fikra za kijinga kama hizi. Umasikini hauwezi kuisha Afrika kama tutaendekeza kuwa na watu tegemezi wasio na sifa za kuwa tegemezi.

zamani mwanamke alihakikisha jukumu la chakula cha takribani mwaka mzima ni lakwake kwa kulima akishirikiana na watoto na mume anatoa mahitaji mengine, ila leo unaishi na mwanamke anafanya kazi eti kuna wapumbavu wanakwambia pesa ya mke haiulizwi.

Kwangu mke akijishughulisha na jambo lolote linaloingiza kipato basi anao wajibu kwenye familia unaoendana na kipato chake.
 
Hizo pesa za kumlipa h/girl atazitoa wapi km anataka kusaidiwa majukumu na mkewe?!!
Mimi wifi niwe mkweli nitawajibika km mume nikiona kweli hapa ametingwa au kuna mradi wa familia pesa zake zinaenda huko kufanikisha hilo, otherwise wala sijigusi.!!
Wajibika
Familia ni wajibu wako!

Mumeo ndio ana mamlaka ya kukuruhusu kukaa bila kuprovide chochote!
Kama ni wewe mwenyewe unaamua kuacha mzigo wote kwa mume, huwezi jua huenda mume anakerekwa na hasemi kuogopa ataonekana weak man!

Na hapa nakuona kabisa unaitumia ndoa kujinufaisha!
Kama hauprovide hata robo, hizo pesa unapeleka wapi?
Unyonyaji wa kiwango Cha juu zaidi

Nyie ndo aina ya wanawake ambao munaolewa kwa misingi ya uchumi,
Mume akifilisika tu na ndoa inavunjika
 
Moja wapo ya ujinga uliozaa umasikini mkubwa Afrika ni huu wa pesa ya mwanamke haihudumii familia.

Yani nchi masikini kama TZ ambako hakuna ajira, hakuna vibarua alafu jukumu la kugharamia mahitaji ya familia liwe la mtu mmoja, na mtegemee hiyo familia ikue kiuchumi bila baba kuwa na presha na magonjwa yanayosababishwa na msongo wa mawazo.

Kuna kakundi kadogo sana kanakoingiza pesa hapa Tanzania ila kanagharamia watoto, wanawake, wazee n.k. huu ni ujinga hatuwezi kukua kiuchumi kwa fikra za kijinga kama hizi. Umasikini hauwezi kuisha Afrika kama tutaendekeza kuwa na watu tegemezi wasio na sifa za kuwa tegemezi.

zamani mwanamke alihakikisha jukumu la chakula cha takribani mwaka mzima ni lakwake kwa kulima akishirikiana na watoto na mume anatoa mahitaji mengine, ila leo unaishi na mwanamke anafanya kazi eti kuna wapumbavu wanakwambia pesa ya mke haiulizwi.

Kwangu mke akijishughulisha na jambo lolote linaloingiza kipato basi anao wajibu kwenye familia unaoendana na kipato chake.
Cha ajabu, kule kwa wenye akili na walioendelea, ujinga huu haupo
 
Ndio, napinga!,

Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!

Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.

Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.

Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!

Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!

Kwa Wakristo ipo wazi;

"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"

Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.

"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"

Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?

"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"

Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.

Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?

"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"

Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.

Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.

Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.

Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.

Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,

Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.

Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!

Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!

Ikumbukwe dunia imebadilika.

Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.

Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.

Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.

Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?

Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.

What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?

Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!

Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"

Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.

Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!

Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?

Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?

Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!

Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?

Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.

Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!

Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.

Mume akifa unadai urithi wa mali zote!

Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

utafiti kidogo tu utajua asili ya ndoa, muasisi wa ndoa, miiko na miongozo ya ndoa. Ukiyajua haya, itakufaa sana
 
Wajibika
Familia ni wajibu wako!

Mumeo ndio ana mamlaka ya kukuruhusu kukaa bila kuprovide chochote!
Kama ni wewe mwenyewe unaamua kuacha mzigo wote kwa mume, huwezi jua huenda mume anakerekwa na hasemi kuogopa ataonekana weak man!

hapa nakuona kabisa unaitumia ndoa kujinufaisha!
Kama hauprovide hats robo, hizo pesa unapeleka wapi?
Unyonyaji wa kiwango Cha juu zaidi

Nyie ndo aina ya wanawake ambao munaolewa kwa misingi ya uchumi,
Mume akifilisika tu na ndoa inavunjika
Siwajibiki km unavyotaka wewe, elewa point yangu kwanza.
Nitawajibika km pesa yake inaenda kutekeleza mradi wa familia. Na inaonekana kazi inafanyika!! Hapo nitamsaidia.
Ila km toka mwanzo sio muwajibikaji niwe mkweli sijigusi.!!
Pia inategemea na upendo wake kwangu, sio mwanaume ana kijiji cha michepuko pesa zake zitumike kunjunjia halafu zangu ziwajibike hilo pia asahahu..!!

Mwanaume mvivu katulia hajigusi na kazi yeyote kalegeza kengele zake eti kisa nina kipato cha kuhudumia familia, huyo naye asubiri kuandika talaka akafie mbele.
 
Huo uwajibikaji uwe kwenye kutoa pesa tu au na mengine tutashirikiana?!!
Sawa nitakubali kuwajibika ila na wewe usiwe mkali nikiomba tuwajibike wote kwenye kufua, kupika na usafi wa nyumba. Sababu hata maandiko yanasema, “ Mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu” hapo naomba twende sawa.!!
Msiwe mnachagua vifungu vya kuwafurahisha na kuwalinda nyinyi…!!
Uduguu umeandika wee, au cm iko hacked?
 
Hali ni mbaya, sijui serekale iweke ndoa za waume wawili pia ili huyu jamaa yetu asaidiwe kwa ukaribu zaidi. Make anadai kama mke ni kuacha wazazi nae kaacha wakwake [emoji81]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom