Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kuzunguka, ni fact endelevu kwenye maisha!Kazunguka sana ila ndo point yake hiyo
Eti unakuta wote mnafanya kazi na pesa mnapata wote,halafu wewe ndio wa kubeba majukumu peke yako,hell no, kwangu hii haikubaliki....Ndoa ni kichaka cha mwanamke kujitajirisha.... Kataaa
So, hapo kwako pia natumaini kazi kama za kuosha vyombo, kupika na kufua mnagawana pia na mke wako otherwise utakuwa ni mnafki tuSio kuzunguka, ni fact endelevu kwenye maisha!
Mama yako alikuwa anamsaidia baba Yako
Bibi Yako alikuwa anamsaidia Babu Yako
Sijaleta andiko hili Ili kujenga mwenendo mpya wa maisha, Bali kujinga mfumuko mpya wa maisha wa baadhi ya wanawake kulilia kujitenga na familia
Huo ni mfumo wa kikahaba, ambapo kahaba anapelekwa lodge anahudumiwa Kila kitu!
Sasa mentality hii inataka ipelekwe kwenye familia na kuundiwa Sheria iwe Sheria maalumu ya ndoa
No!
Usaidiweee naunga mkono usaidiweEti unakuta wote mnafanya kazi na pesa mnapata wote,halafu wewe ndio wa kubeba majukumu peke yako,hell no, kwangu hii haikubaliki....
Age is just a number usijidai sana na hizi fake ID naamin vp ww dada yangu?Mimi dada yako nimewahi kuliona jua naachaje kuwa na akili??
What if mimi ndio nalisha na kuvishq?Hongera kwa kulishwa na kuveshwa ukiwa umejikalia bila kumsapoti mume kwa lolote
Eva mwenyewe alishirikiana began kwa began na Adamu kulima ngano na kufuga kondoo kwa ustawi wa familia yao
Wewe ulitakiwa uwe mwanamke.Kwa maandishi haya, wapi panaelekeza mke si msaidizi wa provisions za nyumba?
Ndio unavyojidanganya?? Wewe nakuzaa huku napiga deki.Age is just a number usijidai sana na hizi fake ID naamin vp ww dada yangu?
Basi aache kazi, ahudumiwe!Eti unakuta wote mnafanya kazi na pesa mnapata wote,halafu wewe ndio wa kubeba majukumu peke yako,hell no, kwangu hii haikubaliki....
Babu yangu hakuosha vyombo, na bado bibi alijumuika nae katika shughuli za uzalishaji maliSo, hapo kwako pia natumaini kazi kama za kuosha vyombo, kupika na kufua mnagawana pia na mke wako otherwise utakuwa ni mnafki tu
Ni Jambo jema Kama uchumi wako unakuruhusu ukilinganisha na mumeo ambaye hajayapata maishaWhat if mimi ndio nalisha na kuvishq?
Evelyn SaltUsaidiweee naunga mkono usaidiwe
Wacha weeee, kimsingi unakua mmeoana shemegi au sio.....Evelyn Salt
Issue sio kusaidia
Bali ni kuwajibika kwa familia yake
Mwanamke sio kabati kwamba limenunuliwa kuwekwa ndani,
Familia ni ya Mume na mke
Ni majukumu yao pamoja!
Mume akifa, familia inabaki na mama na Wala haipelekwi kwa ndugu wa mume
Mali zote za familia zinabaki na mama na Wala hazipelekwi kwa ndugu wa mume
Mume na mke wakiachana, Mali yote ni mgao wa nusu kwa nusu na wala haibaki kwa mume ambaye wewe unamuona ndio mwenye familia
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Yes, marrying each other!Wacha weeee, kimsingi unakua mmeoana shemegi au sio.....
Shemegi umeoana??? Au bado unatafuta?
Let us marry dear Evelyn Salt!Shemegi umeoana??? Au bado unatafuta?
Karibu tuoane....Let us marry dear Evelyn Salt!
Mimi na wewe tukiungana na kushirikiana kwa upendo, tutaijenga familia yetu yenye furaha kubwa Hadi kifo kitapotutenganisha!
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Tuanzie hapo kwene WEAK MANNdio, napinga!,
Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!
Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.
Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.
Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!
Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?
Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!
Kwa Wakristo ipo wazi;
"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"
Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.
"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"
Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?
"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"
Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.
Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?
"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"
Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.
Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.
Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.
Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.
Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,
Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.
Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!
Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!
Ikumbukwe dunia imebadilika.
Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.
Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.
Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.
Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?
Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.
What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?
Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!
Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"
Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.
Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!
Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?
Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?
Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!
Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?
Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.
Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!
Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.
Mume akifa unadai urithi wa mali zote!
Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app