Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Leo ndio nasikia kutoka kwako kuwa kuzaa ni 50% ya majukumu ya familia, inashangaza!!

Kwanza picha inaanza kwa mume kumpiga miti mke,

Uja uzito tangu umeanza hadi miezi sita ni hakuna uchungu

Uchungu wa uja uzito unaanza labda miezi Saba Hadi tisa na siku yenyewe ya labour!

Hio ni miezi mitatu ya uchungu wa kuzaa

Mtoto akizaliwa Kuna jukumu la kulea mtoto, hapa baba anashiriki. Kubeba mtoto, kumuogesha, kumvisha, kucheza nae kwenye kochi, kumpeleka hospitali n.k

Uchungu wa miezi mitatu wa kuzaa haiwezi kuthaminishwa na uchungu wa kutunza maisha ya watu wa familia kwa miaka 30

Mwanamke mwenyewe ukimwambia achague kukaa pekeyake miaka 30 bila kupewa uchungu wa kuzaa, au kukaa na mume ampe uchungu wa kuzaa atachagua Nini?

Kumbuka Eva alizaa kwa uchungu Kisha akaendelea na kazi za shamba ili kutunza familia yao

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ulishawahi kubeba mimba mkuu?
 
Ndio, napinga!,

Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!

Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.

Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.

Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!

Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!

Kwa Wakristo ipo wazi;

"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"

Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.

"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"

Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?

"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"

Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.

Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?

"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"

Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.

Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.

Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.

Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.

Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,

Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.

Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!

Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!

Ikumbukwe dunia imebadilika.

Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.

Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.

Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.

Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?

Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.

What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?

Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!

Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"

Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.

Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!

Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?

Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?

Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!

Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?

Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.

Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!

Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.

Mume akifa unadai urithi wa mali zote!

Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hutaki kuwa provider wa familia yako na unataka kuwa kichwa cha familia.

Are you serious? Unless unataka wote muwe vichwa vya familia.
 
wewe hii dhana umetoa wapi mkuu?

maandiko yanatuambia mwanamke atazaa kwa uchugu na mwanaume atakula kwa jasho lake.
maana yake mwanaume kazi yako ni kupambana na kuhakikisha familia ina kula vzr na kuishi vizuri.

maandiko yanatumbia mwaanaume ni kichwa cha familia{mke wake}
Eva alizaa kwa uchungu Kisha akaendelea na kazi za shamba ili kutunza familia yake kwa ushirikiano na mumewe kipenzi Adam

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hutaki kuwa provider wa familia yako na unataka kuwa kichwa cha familia.

Are you serious? Unless unataka wote muwe vichwa vya familia.
Adamu alikuwa kichwa Cha familia, but asubuhi alimchukua mkewe Eva kwenda kushirikiana kulima na kuvuna ngano!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Adamu alikuwa kichwa Cha familia, but asubuhi alimchukua mkewe Eva kwenda kushirikiana kulima na kuvuna ngano!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kushirikiana haiondoi jukumu la wewe kuwa provider. Na akikusaidia ni kuwa amekusaidia tu kama msaidizi wako ila mwenye jukumu ni wewe. Uanaume si mchezo ni kubeba mizigo.

Jiulize kwa nini walikula tunda wote lakini aliyeulizwa ni Adam na sio mkewe.
 
Nimeshaandika kwa ufupi kwenye Makala yangu!

Ila nikujuze tu, asilimia zaidi ya 80 ya ndoa za Tanzania, Afrika na ulimwenguni kote wamama wanawajibika!

Ni Wanawake wachache wanaohisi ndoa ni fursa Yao ya kujinufaisha kimaisha

Ni Wanaume wachache waliolewa mafanikio ya kiuchumi wanaweza kuhudumia familia kwa 100% wanaeneza propaganda chafu ya kuaminisha jamii kuwa mwanamke hapaswi kuwajibika kwenye familia

Propaganda Hizi zinaharibu upendo na mshikamano wa wanandoa ktk kujenga familia kwa Hali na mali
Asili ya ndoa bado hajaijua. Tafiti kidogo tu
 
Vijana shupavu hao,kazi ni kubwa sana inakuja mbele yenu.

Wewe nakumbuka kuna sehemu umeni-diss kwamba mimi sina akili na ni kwenye mada hizi hizi za ndoa,sasa kama wewe mwenye akili ndiyo huyu unaewaza umtie mkeo mimba azae then apeleke mwanao shule sijui nani atakuwa akili hana.
Heshimu mawazo ya Weakman
 
Ndio, napinga!,

Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!

Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.

Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.

Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!

Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!

Kwa Wakristo ipo wazi;

"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"

Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.

"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"

Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?

"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"

Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.

Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?

"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"

Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.

Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.

Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.

Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.

Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,

Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.

Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!

Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!

Ikumbukwe dunia imebadilika.

Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.

Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.

Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.

Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?

Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.

What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?

Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!

Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"

Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.

Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!

Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?

Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?

Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!

Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?

Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.

Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!

Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.

Mume akifa unadai urithi wa mali zote!

Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ni sahihi kushirikiana hata Mithali 31 inamuongelea vizuri sana mke mwema jinsi gani anashiriki kwenye uchumi wa familia. Kwa sehemu ndogo nimenukuu

(Mithali 31:10; Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Moyo wa mumewe humwamini,Wala hatakosa kupata mapato. Mithali 31:16; Huangalia shamba, akalinunua;Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu etc..)

Kikubwa tutambue Mume ana nafasi pia katika kufanya ndoto za mke wake zinatimia, muwape nafasi!!
 
Wanawake wanataka 50/50 kwenye kila kitu kasoro hapo kwenye kujumuishwa katika ulipaji wa bills ndipo wanataka jukumu lote libebwe na mwanaume kwa 100%. Kupitia movements za 50/50 wanawake wanawataka ajira na ukishapewa ajira maana yake unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi utawajibika kujihudumia mwenyewe au kuchangia kitu mezani, cha kushangaza ferminists wanataka ajira na bado wanataka kuhudumiwa na mwanaume ndipo hapa unakuja utata. Binafsi naona kama mke ni mama wa nyumbani mwanaume abebe jukumu lote la ustawi wa uchumi kwenye familia na kama mke ana shughuli ya kumuingizia kipato basi bills zilipwe na wote mke na mume kwa kuzingatia uwiano wa vipato vyao.
 
Back
Top Bottom