Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wakati nafikiria kuandika uzi huu, niliogopa kidogo kwa hofu hiyo hiyo ya kutekwa, lakini nikajipa moyo kwamba tukinyamaza hapa JF ni nani mwingine atasema?
Kwa Rais kusema hadharani kwamba masuala ya kutekwa watu yanayoendelea kwenye nchi anayoiongoza ni Drama, si tu kwamba ni uongo lakini pia ni kejeli isiyokubalika, Yaani watu watekwe na kupelekwa polisi na baadaye kutupwa kusikofahamika halafu tuaminishwe kwamba hizo ni Drama! ili kuamini jambo hili Tunapaswa tusiwe na akili kabisa au tuwe tumenyofolewa ubongo.
Ni kweli kwamba Mkubwa hakosei, lakini kwenye hili Mama Kakosea na anapaswa kuomba radhi, Vinginevyo awe tayari kuhusishwa na utekaji unaoendelea na kwamba Yeye ndiye anayewatuma Watekaji na ameamua kufunika ili kuepuka lawama.
"Nchi yetu ina sifa kubwa sana ndani ya ukanda wetu na duniani, sasa zikitoka ripoti hizi huyu kauawa, huyu katekwa, huyu kafanywaje aahh, na yakitokea mbio serikalini"
"Tukizungumza haya ya kutekwa haya, unasema katekwa nani? unasikia mtoto alijiteka mwenyewe anapiga simu kwao zitoke pesa, huku mama kamtekesha mwanawe ili baba atoe pesa, yani vidude vya drama drama tu hivi lakini vinavyoandikwa kwenye vyombo vya habari ni kama serikali imelala watu wanatekwa tekwa tu hovyo, naomba sana tusiyafumbie macho" - Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Machifu Ikulu Dodoma
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Rais Samia: Machifu waambieni wanasiasa ukweli vyeo havipatikani kwa kuua watu