Pre GE2025 Napinga Kauli ya Rais Samia kwamba Utekaji ni Drama, hii ni dharau kwa Wananchi

Pre GE2025 Napinga Kauli ya Rais Samia kwamba Utekaji ni Drama, hii ni dharau kwa Wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Screenshot_2024-09-08-10-48-20-1.png
 
Hata katika hili ya kifo cha Ally RIP, Rais atasema ni drama. Atasema kuwa alijiteka halafu akajiua , kisha akajitupa vichakanai. Alaaniwe mtu huyu unaoufanyia dhihaka uhai wa binadamu wenzake. Laani ya Mungu wetu, tunakuomba Mungu wetu, ikawe juu ya huyu mtu na wazao wake kwani aliudhihaki uhai wa binadamu wengine. Kama alivyouona uhai wa wengine kutokuwa wa thamani, ndivyo hivyo hivyo ukawe wa kwake. Maana ulituasa kuwa tuwatendeavyo wenzetu ndivyo tutakavyotendewa na sisi wenyewe.

Tunaomba sana, wauaji walindwe lakini wasiwe salama, wayashike madaraka kwa gharama ya uhai wa binadamu wenzao, lakini kamwe madaraka yasikae nao kila uovu wautendao dhidi ya wengine ukawarudie mara tatu zaidi. Wewe ni Bwana wa haki, tunaomva uwalipe hawa malipo ya haki sawa na uovu wao.
 
Wakati nafikiria kuandika uzi huu, niliogopa kidogo kwa hofu hiyo hiyo ya kutekwa, lakini nikajipa moyo kwamba tukinyamaza hapa JF ni nani mwingine atasema?

Kwa Rais kusema hadharani kwamba masuala ya kutekwa watu yanayoendelea kwenye nchi anayoiongoza ni Drama, si tu kwamba ni uongo lakini pia ni kejeli isiyokubalika, Yaani watu watekwe na kupelekwa polisi na baadaye kutupwa kusikofahamika halafu tuaminishwe kwamba hizo ni Drama! ili kuamini jambo hili Tunapaswa tusiwe na akili kabisa au tuwe tumenyofolewa ubongo.

Ni kweli kwamba Mkubwa hakosei, lakini kwenye hili Mama Kakosea na anapaswa kuomba radhi, Vinginevyo awe tayari kuhusishwa na utekaji unaoendelea na kwamba Yeye ndiye anayewatuma Watekaji na ameamua kufunika ili kuepuka lawama.


"Nchi yetu ina sifa kubwa sana ndani ya ukanda wetu na duniani, sasa zikitoka ripoti hizi huyu kauawa, huyu katekwa, huyu kafanywaje aahh, na yakitokea mbio serikalini"

"Tukizungumza haya ya kutekwa haya, unasema katekwa nani? unasikia mtoto alijiteka mwenyewe anapiga simu kwao zitoke pesa, huku mama kamtekesha mwanawe ili baba atoe pesa, yani vidude vya drama drama tu hivi lakini vinavyoandikwa kwenye vyombo vya habari ni kama serikali imelala watu wanatekwa tekwa tu hovyo, naomba sana tusiyafumbie macho" - Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Machifu Ikulu Dodoma

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Rais Samia: Machifu waambieni wanasiasa ukweli vyeo havipatikani kwa kuua watu
Kuna jamaa anaitwa ChoiceVariable anasema mama Samia hakusema haya maneno yenye kuonyesha kuyapuuzia matukio ya kutekwa, kupotezwa, kuuwawa nk.
 
Yametimia! hatimaye amehusishwa na watekaji kikamilifu.

Mungu ibariki JF
 
Ni kutothamini uhai na maisha ya unaowaongoza....
Dini bado hazijaweza kushape viongozi... Vyeo vyao wanavithamini kuliko muumba wao
 
Back
Top Bottom