EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,352
Gambo kama kiongozi, moja ya majukumu yake ni kutatua migogoro (conflict resolution) ikiwamo ile anayohusika yeye. Kushindwa kutatua mgogoro wake na "watumishi" wake ni moja ya kiashiria kuwa uongozi ulimshinda.
Tatizo zaidi ni kuwa mgogoro wao ulikuwa kikwazo cha maendeleo Arusha mjini. Maamuzi hayafanyiki kwa kuwa wanatunishiana misuli na wanashindwa ku-kompromaiz. Si kwamba ofisi/taasisi zote watu huelewana bali yanapokuja masuala ya kazi tofauti sharti zikae kando.
Uamuzi wa rais ni sahihi kabisa (kwa assumption kuwa sababu kubwa ni hiyo). Japo inasikitisha kuwa utenguzi umekuja wakati mbaya kwa watenguliwa hasa Gambo. Awe positive ajisahihishe, muda bado anao ikiwa ana ndoto kwenye siasa.
Hata Simbachawene, Mwigulu, Kicheere, nk walianguka kisha wakainuka.