Napinga LATRA kuwafungia KATARAMA kwa visingizio cha kuchezea kidhibiti mwendo

Napinga LATRA kuwafungia KATARAMA kwa visingizio cha kuchezea kidhibiti mwendo

Naona latra umekuja na zile ID almaarufu za msaada: "joined 5 Jul 2020, posts 12 na reaction scores 5.

Hata hivyo isiwe kesi.

Hapa mnaongelea chipsets na software ya vifaa vyenu vis a vis operator asiyekuwa na ujuzi wowote na vifaa vyenu.

Tumeona wangapi wakibambikiziwa bangi, madawa, nyara za serikali, bunduki, risasi nk, sembuse hili?

Kumbe kipi kibongo bongo kinaisimamisha mamlaka ipi kuto hujumu biashara ya mtu panapo nafasi?

Tumesikia watu kuporwa hata uhai na mamlaka zetu hizi hizi, sembuse hili?

Kwani kama nia ilikuwa ni njema kuzuia magari yasiende zaidi ya 80km/h, kumbe kwanini yasiagizwe magari yenye maximum speed 80km/h tu mkaachana na hivyo vifaa vyenu?

Au kwanini basi latra msiwe na magari ya mfano tuone mtakavyo yaendesha vyema zaidi?

Kulikoni kuweka vifaa vyenu kwa watu kisha kuwalaumu wao? Si mkae navyo wenyewe?

Hudhani hili la kuweka vifaa vyenu kwenye maeneo ya wengine kunaacha mianya ya kutwishana mizigo isiyokuwa na uhalali wowote?

Mnamlaumu vipi mtu kwenye vifaa vyenu ambavyo mwenye bus hana ujuzi navyo kwa lolote?

Ninakazia:

Kwa hakika na lawyer mzuri "kulikuwa na mabilioni kwenye fidia hapa!"
Uko sahihi sana,na umeliweka vizuri sana..washapata malalamiko mara kibao kuhusu vile vifaa vyao kuungua.
 
Uko sahihi sana,na umeliweka vizuri sana..washapata malalamiko mara kibao kuhusu vile vifaa vyao kuungua.

Ngoja tumwite maana amekuwa kama kaja kubeep na kuingia mitini.

Ndugu "latra" aka wanton6 kuna miito yako huku mingi ya kutosha:

"Ulisema tutaelewa tu, tunaona ndiyo kama umelikoroga zadi."

Mwongozo wako tafadhali.
 
Back
Top Bottom