Napinga LATRA kuwafungia KATARAMA kwa visingizio cha kuchezea kidhibiti mwendo

Napinga LATRA kuwafungia KATARAMA kwa visingizio cha kuchezea kidhibiti mwendo

Kufungiwa Karatama ni fitina za kibongo. Nakumbuka wakati Katarama linaaza safari zake, nilikuwa natoka Mwanza kuja Dar wakati tumefika Buhongwa kuna jiwe lilitupiwa kwenye basi upande wa mbele wa kushoto wa abairia kioo kikapasuka(abiria wakasema hizi ni hujuma) baada ya siku kadhaa nikasikia Latra wanataka kulifungia. Kuna mabasi nimewahi kupanda mfano; Ally's VVIP Ile basi ilikuwa inatembea mwendo wa 120-140 km/hr; Tahmeed nikiwa natokea Kenya--> Dar yule dereva alikuwa hashuki 130 km/hr. Hapo Ally's kaona ligi imekuwa ngumu​
 
Ndio Scania sio Mchina
 
Mbona GOLDEN DEER na dada yake NEW FORCE hawako kwenye list ilhali Hawa ndio chinja chinja wa kusini? Au NEW FORCE inamilikiwa na LATRA?
 
LATRA wametoa taarifa kwa umma kuhusu kufungia leseni ya usafirishaji Abiria ya Kampuni ya KATARAMA kwa kigezo kuwa wanachezea vidhibiti mwendo. Sina tatizo na hilo.

Ila kama ni kweli basi, naomba wawe fair kwa makampuni mengine pia, nilidhani Abood ya Bukoba na Mwanza wangekuepo, nilidhani Kampuni ya Baraka inayoenda kusini wangekuepo kwenye list. Ukweli ni kwamba, karibia mabasi yote (90%) wanachezea vidhibiti mwendo. Mimi ni mdau WA Safari na Road Safety issues.

Usiku wa Leo, au hata jioni hii lipia route yoyote ile, fanya observation yako kama ABC au Superfeo wanatembea speed 80km/HR angalia kama BM anatembea hio speed , sijamtaja Tilisho wala KSK....wala Buti la Zungu au Njombe Express.......hakuna anatembea huo mwendo. Wachunguze mabasi ya Kigoma ukiacha Kasulu express (mbovu) wengine wote ni Moto mwanzo mwisho. Mbona ALLY'S hayupo Kwenye list??

Nashauri LATRA wa-revise hio speed 80, it is unrealistic no matter what!

Pili, ni uchawi kufungia Kampuni wakati ni individuals, wafungiwe madereva maana owner sio anaye monitor speed ya gari.
View attachment 3094139
LATRA wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kama unayajua baadhi ya mabasi ambayo yanachezea mfumo wa kudhibiti mwendo ni vyema ukawasilisha kwa Mamlaka husika kwani utakuwa umefanya jambo jema na la kizalendo kuliko kutetea makosa ambayo yanaweza kugharimu maisha ya watanzania wengi zaidi.
 
Saidia Kuokoa maisha ya wengine, wasilisha lalamiko lako kwa LATRA kupitia 0800110019/0800110020
kupiga kelele mitandaoni haisaidii.
 
Back
Top Bottom