Napinga LATRA kuwafungia KATARAMA kwa visingizio cha kuchezea kidhibiti mwendo

Napinga LATRA kuwafungia KATARAMA kwa visingizio cha kuchezea kidhibiti mwendo

LATRA wametoa taarifa kwa umma kuhusu kufungia leseni ya usafirishaji Abiria ya Kampuni ya KATARAMA kwa kigezo kuwa wanachezea vidhibiti mwendo. Sina tatizo na hilo.

Ila kama ni kweli basi, naomba wawe fair kwa makampuni mengine pia, nilidhani Abood ya Bukoba na Mwanza wangekuepo, nilidhani Kampuni ya Baraka inayoenda kusini wangekuepo kwenye list. Ukweli ni kwamba, karibia mabasi yote (90%) wanachezea vidhibiti mwendo. Mimi ni mdau WA Safari na Road Safety issues.

Usiku wa Leo, au hata jioni hii lipia route yoyote ile, fanya observation yako kama ABC au Superfeo wanatembea speed 80km/HR angalia kama BM anatembea hio speed , sijamtaja Tilisho wala KSK....wala Buti la Zungu au Njombe Express.......hakuna anatembea huo mwendo. Wachunguze mabasi ya Kigoma ukiacha Kasulu express (mbovu) wengine wote ni Moto mwanzo mwisho. Mbona ALLY'S hayupo Kwenye list??

Nashauri LATRA wa-revise hio speed 80, it is unrealistic no matter what!

Pili, ni uchawi kufungia Kampuni wakati ni individuals, wafungiwe madereva maana owner sio anaye monitor speed ya gari.
View attachment 3094139
Kwani ukipinga ndio itazuia utekelezaji wa sheria?

Mwisho kama unadhani hiyo speed haifai peleka mswaada bungeni,Latra wanatekeleza sheria.

Latra/Polisi msicheke na kima Kwa gharama za uhai Wetu.Na Polisi futeni leseni za hao madereva.
 
Back
Top Bottom