Huu ni ushauri wa bure kwa Mchungaji Msigwa
Historia haiongopi. Dr Slaa alipondoka CDM alikwenda moja kwa moja Serena Hotel akiwa na CCM.
Hapa JF tulimwambia kuhama chama si tatizo, kugeuka na kula matapishi ni tatizo
Msigwa amekuwa CDM kwa muda mrefu ndani ya kamati kuu ya chama.
Bila kujali nini kimemuondoa na kwa kuzingatia haki yake ya kufanya siasa, itashangaza kama ataanza kuisema Chadema. Msigwa ni Mchungaji mtu anayebeba dhamana ya uaminifu wa kiroho na mwanasiasa.
Kauli za Msigwa akiwa CDM zilikuwa za kisiasa zikibebwa na 'uaminifu' kama Mchungaji.
Kwa miaka mingi ametunga na kusimamia sera za CDM. Matatizo ya vyama siasa hayakukosekana.
Ni Msigwa huyo wiki iliyopita alisema ' kuetetea sera za chama ni wajibu''
Msigwa aliyeandika sera na kuzisimamia tena wiki moja iliyopita akiwa mwanasiasa na Mchungaji sasa anakwenda 'kueleza uongo wa CDM'' na siyo sera alizotunga , kuzisimamia na kuzisimamia
'Kuusema 'Uongo'' wa CDM aliousimamia utaondoa sifa yake ya Uchungaji achilia mbali siasa.
Namshauri kwa dhati kabisa, Msigwa asimamie sera za CCM na kuzieleza vema! Ni haki yake
Ni haki yake pia kueleza ''uongo wa CDM na Saccos'' lakini haki hiyo itamuondolea heshima yake mbele ya jamii.
Kwamba kwa miaka mingi hakuliona hilo? Kwamba leo anakula matapishi yake, ni mzima kiroho na kiafya?
Msigwa, kuna maisha nje ya siasa, isijefika mahali jirani akatilia shaka kuomba chumvi nyumbani kwako.
Ikafika mahali watoto wako wakaacha kutumia jina la ubini kuepuka fedheha ya muda mfupi na mrefu.
JokaKuu Tindo