Kumpa kijana huyu mikoba ya kufundisha Arsenal itakuwa kamari ya kijinga sana kuicheza na nachukua nafasi hii kupinga kabisa njama hizo .
Arteta aliyezaliwa 26/3/1982 hana uzoefu wa maana wala ujasiri wowote wa kuipa Arsenal mataji , katika kipindi alichoitumikia Arsenal pamoja na kupewa Arm band hakuwahi kutoa mchango wowote wa kusaidia timu yake , hata kwa kuhamasisha kwa maneno tu kama wafanyavyo Ma Captain wa vilabu vingine , aliitwa Man City kuwa kocha msaidizi July 3 2016 , mpaka sasa ni chini ya miaka miwili , huyu si wa kupewa timu tajiri kama Arsenal
Arsenal inahitaji kocha mzoefu mwenye mafanikio yasiyotiliwa mashaka , Au la kama viongozi wanapenda kumpa kazi hiyo yule aliyechezea klabu yao basi nafasi hiyo wapewe wachezaji wenye uchungu mkubwa waliotoa jasho na damu kuipa timu mataji , wachezaji hao wapo na majina yao yanafahamika , lakini si Arteta .
Nakala imfikie Arsene Wenger .