Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema hakuna Kiongozi wa ngazi yoyote wa Chama hicho anayeweza kufanya Maamuzi ya Peke yake (Maamuzi Binafsi) ambayo yanaweza kutengua adhabu aliyopewa Mwanachama yeyote yule na Vikao halali vya Chama.
Njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kutumia Vikao vile vile vya Chama, ambavyo kwa namna yoyote havitaweza kuketi ili kujadili Ujinga huo, Halima Mdee na Wenzake walishafukuzwa na Chadema kwa vikao halali vya Chama vilivyotumia pesa nyingi za Chama kuviitisha, Chadema haina hela za kuchezea ili kuitisha vikao vya masihara, hili limeisha na waendelee kujiambatanisha na CCM kama walivyofanya kwa miaka mitano yote.
Dkt Slaa aliondoka Chadema kwa kisingizio cha Lowassa, akiwa yeye ndiye kamleta Lowassa! akahongwa Ubalozi waziwazi , namna alivyoingizwa Hotelini kwa Press iliyoandaliwa na serikali ili kutukana Chadema kila mtu aliona (Video zile zingalipo hata leo), Huyu hata Shambulio la kumuua Tundu Lissu aliita Shambuloo la Kawaida, na kwamba mashambulio kama hayo hata huko Ulaya yanafanyika, huyu aweza kurudi Chadema, Chama alichokituhumu kuleta Choo sebuleni ili iweje?
Napinga kabisa jambo hili kufanyika, Chadema ina lundo la Wamama wenye uwezo mkubwa sana wa kuwa viongozi, hakuna sababu ya maana wala ya kijinga ya kuwarejesha Mamluki, Naapa kutoshirikiana nao katika lolote hata kama watarejeshwa (Maana Chama si changu peke yangu)
Wengine wanaweza kusema kwamba Nina roho mbaya na labda nashindwa Kusamehe, lakini ni wapi kwenye Vitabu vya Mungu imeandikwa Tumsamehe Shetani? Pamoja na Mwenyezi Mungu kusisitiza mno Msamaha na kusamehe lakini hakuwahi kuagiza kusamehe Mwovu Shetani.
Naomba Kuwasilisha.