Napinga Njama zozote za kuwarejesha Wasaliti Chadema akiwemo Dkt Slaa na Halima Mdee, Walishafukuzwa na Baraza Kuu

Napinga Njama zozote za kuwarejesha Wasaliti Chadema akiwemo Dkt Slaa na Halima Mdee, Walishafukuzwa na Baraza Kuu

Kweli kabisa Hawa mamluki wa CCM wataleta mtafaruku bora waende jumla wakaunge mkono juhudi
 
Dr Slaa siyo msaliti, Hajawahi kufukuzwa na CHADEMA na hajawahi kujitoa CHADEMA.

Yeye kuteuliwa kuwa balozi haina tofauti na Jussa kuteuliwa na Mkapa kuwa mbunge au Mbatia kuteuliwa na Kikwete kuwa mbunge, hii haiwafanyi kuwa CCM!
Mdee na Slaa ni kitu kimoja tofauti yao ni jinsi tu.
 
Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema hakuna Kiongozi wa ngazi yoyote wa Chama hicho anayeweza kufanya Maamuzi ya Peke yake (Maamuzi Binafsi) ambayo yanaweza kutengua adhabu aliyopewa Mwanachama yeyote yule na Vikao halali vya Chama.

Njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kutumia Vikao vile vile vya Chama, ambavyo kwa namna yoyote havitaweza kuketi ili kujadili Ujinga huo, Halima Mdee na Wenzake walishafukuzwa na Chadema kwa vikao halali vya Chama vilivyotumia pesa nyingi za Chama kuviitisha, Chadema haina hela za kuchezea ili kuitisha vikao vya masihara, hili limeisha na waendelee kujiambatanisha na CCM kama walivyofanya kwa miaka mitano yote.

Dkt Slaa aliondoka Chadema kwa kisingizio cha Lowassa, akiwa yeye ndiye kamleta Lowassa! akahongwa Ubalozi waziwazi , namna alivyoingizwa Hotelini kwa Press iliyoandaliwa na serikali ili kutukana Chadema kila mtu aliona (Video zile zingalipo hata leo), Huyu hata Shambulio la kumuua Tundu Lissu aliita Shambuloo la Kawaida, na kwamba mashambulio kama hayo hata huko Ulaya yanafanyika, huyu aweza kurudi Chadema, Chama alichokituhumu kuleta Choo sebuleni ili iweje?

Napinga kabisa jambo hili kufanyika, Chadema ina lundo la Wamama wenye uwezo mkubwa sana wa kuwa viongozi, hakuna sababu ya maana wala ya kijinga ya kuwarejesha Mamluki, Naapa kutoshirikiana nao katika lolote hata kama watarejeshwa (Maana Chama si changu peke yangu)

Wengine wanaweza kusema kwamba Nina roho mbaya na labda nashindwa Kusamehe, lakini ni wapi kwenye Vitabu vya Mungu imeandikwa Tumsamehe Shetani? Pamoja na Mwenyezi Mungu kusisitiza mno Msamaha na kusamehe lakini hakuwahi kuagiza kusamehe Mwovu Shetani.

Naomba Kuwasilisha.
Chadema kwa vikao halali vya Chama vilivyotumia pesa nyingi za Chama kuviitisha, Chadema haina hela za kuchezea ili kuitisha vikao vya masihara, hili limeisha na waendelee kujiambatanisha na CCM kama walivyofanya kwa miaka mitano yote.
 
Mbona msimamo wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, ndugu Tundu Lissu uko wazi kabisa kuhusu hao Wabunge 19 wa Viti maalumu

Fatilia interview yake na Crown FM akiwa na Salim Kikeke
Hawezi fuatiliaa maana matokeo yamekuwa tofauti na alivyotarajia,huoni Kawa ka aliyerukwa akili
 
Dr Slaa siyo msaliti, Hajawahi kufukuzwa na CHADEMA na hajawahi kujitoa CHADEMA.

Yeye kuteuliwa kuwa balozi haina tofauti na Jussa kuteuliwa na Mkapa kuwa mbunge au Mbatia kuteuliwa na Kikwete kuwa mbunge, hii haiwafanyi kuwa CCM!
Ni ajabu mpaka leo hawataki kukiri kuwa kumleta lowasa lilikuwa kosa kubwa. Ni upumbavu kudai lowasa aliletwa na Dr Slaa.
 
Usimwamshe aliyelala ,mwaache afanya anavyotaka CHAMA kimfie mapema ,usimsanue.

Awarudishe wote kina GAUCHO ,SILINDE ,LIJUA LIBUTU ,PASTOR KINYAMBE ,MASHILINGI ,MIKWABWE ,DR MOLELI ,GEKULI ,SLAA ,ZITTO ,KITILA ,TWO2 etc
 
Hawezi guatiliaa maana matokeo yamekuwa tofauti na aluvyotarajia,huoni Kawa ka aliyerukwa akili
Kwasasa jamaa amebadirika ghafla

Ameamua kui attack uongozi wote wa Kamati kuu yao kwamba sio lolote sio chochote

Hii ni baada ya timu yake kushindwa Uchaguzi Mkuu

Sijui anakwama wapi, Lissu amesema yeye sio mtu wa visasi

Sijui jamaa ana wasiwasi gani na uongozi mpya 🙌
 
Dr. Slaa bora arudi, ni muhimu japo hana msimamo, tabia zake zimeshajulikana arudi chamani ila wale wabunge waende na maji wakajiunge na vyama vingine. Hata wakirudishwa chamani hawatakuwa potential, si waaminifu. Na kama wakirudishwa wapewe majimbo wakagombee wasitegemee viti maalum waachie wanawake wengine wapya
 
Sasa kama mlimleta Lowassa na kumsafisha,

Kosa la Slaa ni lipi?

Atarudi nyumbani.
 
Lissu kuna kitu hajaweka wazi na Dr Slaa hajawahi kukataa kuwa hakuwamo kwenye mchakato wa kumleta Lowassa, ila mna msingizia tu Dr Slaa yeye amesema zaidi ya mara mbili ilivyokuwa.
Ukweli ni kwamba lowasa alinunua nafasi ya kugombea urais chadema kwa pesa ndefu, mbowe na lisu walipata mgao.

Ni lisu aliyetoka kwenye media kutudanganya kuwa wamemchukua lowasa baada ya kufanya utafiti na kujiridhisha kuwa alikuwa na nafasi ya kushinda urais.

Nachoshindwa kufahamu mpaka leo ni, mabadiliko gani wananchi tungeyapata kama lowasa angeshinda.
 
Kwasasa jamaa amebadirika ghafla

Ameamua kui attack uongozi wote wa Kamati kuu yao kwamba sio lolote sio chochote

Hii ni baada ya timu yake kushindwa Uchaguzi Mkuu

Sijui anakwama wapi, Lissu amesema yeye sio mtu wa visasi

Sijui jamaa ana wasiwasi gani na uongozi mpya 🙌
Uongo hautakuondolea umasikini unaokuandama
 
I think kushiriki kwa Slaa kuja kwa Lowasa CHADEMA kuwa ni alitaka Lowasa aje CHADEMA lakini awe mwanachama wa kawaida kwanza na siyo mgombea. Ila Lowasa yeye alikuja na mission moja nayo ni kugombea tu na hataki habari nyingine yoyote!.
 
Back
Top Bottom