Napinga Uteuzi wa Kagurumujuli kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, hana Sifa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ifike Mahali viongozi wa Tanzania na hasa Mamlaka ya Uteuzi ijaribu kuwaheshimu Wananchi wake , hata kama ni Wajinga, duni ama Mbumbumbu.

Uteuzi wa Kagurumujuli, kada wa CCM aliyesababisha mauaji ya kijinga ya Akwilina alipokuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, akishirikiana na Lazaro Mambosasa, umelenga kudhalilisha Wananchi wote waliopiga kelele kuhusu mauaji hayo ya kishamba na ni sawa na matusi ya nguoni Kwa familia ya Akwilina.

Kwa kufupisha ni kwamba Kagurumujuli hafai kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa vile ana tuhuma za mauaji, aweza kusababisha mauaji mengine tena.

Mwl Nyerere aliwahi kuwaambia wananchi wa Tanzania kwamba ANAYEKULA NYAMA YA MTU HAACHI.

Nashauri Uteuzi wake Utenguliwe mara moja.
 
Mbowe alipata zero ila anasifa ya kukuongoza ww na mmeo ila huoni shida
USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Nishawaambia yale maridhiano ni danganya toto
CCM haina dhamira nzuri kwa watanzania. Simameni kama chama cha ukombozi dhidi ya mkoloni CCM.

Hizo teuzi ni majibu ya namna gani chama tawala kinavyowaona nyie wapigania haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…