Napinga Wakili Mwabukusi kuulizwa kwanini anataka kuiangusha serikali. Ni JWTZ peke yao ndio wana uwezo wa kuiangusha serikali

Napinga Wakili Mwabukusi kuulizwa kwanini anataka kuiangusha serikali. Ni JWTZ peke yao ndio wana uwezo wa kuiangusha serikali

Yale maneno aliyosema Wakili Mwabukusi kwamba jambo baya litatokea madai yao yasiposikilizwa, yale maneno ni vitisho tu.

Tumemsikia wote Wakili Mwabukusi anasema"Wasidhani tunaleta masihara. We mean business". These are idle words, empty words, hollow words. Kwa sababu huyu Wakili Mwabukusi hana silaha zozote.

Yule mwingine alikuwa anasema juzi,vSerikali imevunja Katiba. Kama ni halali kwa serikali kuvunja Katiba, basi ni halali kwa sisi pia kuvunja Katiba."

Haya ni maneno tu hawa watu wanaongea. Polisi wanakuwa too excited for no reason.

Ni kwamba tu kina Mdude hawajui hii ni nchi ya Chama kimoja, wanadhani wakiitukana serikali kuna mtu atakuja kuwasaidia. Mahakama Beijing inaweza kushindana na CCP?

Yule Wakili ilikuwa hakuna sababu yoyote kumkamata kwa sababu Mahakama ilikuwa imeshamuondoa makali.

Au labda ni vizuri kwa polisi kuwadhibiti watu wote hawa ambao hawakubali kushindwa, ambao wanataka kuikaidi Mahakama.

Sasa Jeshi (la Wananchi) lingekuwa restless, that would have been a different matter.

Lakini tunawapeleka watu kwenye torture chambers, ambao ni nothing, less than nothing.
hizo ndo akili za wanaccm nikwamba wamejikabithi hati miliki za taifa na wananchi wake
 
Hii nchi kuna muda huwa ina mambo ya ki mama mama, mlisema awamu yenu ni ya demokrasia hamkujua demokrasia inajumuisha kutofautiana ki mawazo?? Ukiona hoja zinazotolewa na upande X ni za upotoshaji kwa mini usizijibu kwa hoja sahihi?? Kujibu hoja za upande X kwa kutumia polisi kukamata watoa hoja ni sawa na kujibu hoja zao kwa kuwauliza Unajua Mimi ni nani?? Rubbish.

Huoni wamejibiwa vizuri.kutishia usalama wa taifa ni kosa ndio maana serikali ikajibu kwa kuwakamata na wakikutwa na hatia ni ukongaaa segerea kekooo
 
Hivi wanajeshi wetu hawawaoni wenzao wa Niger walivyomshughulikia bazoum?Maana hata hapa Tanzania tuna bazoum wetu ameanza kutumia polisi kutesa wazalendo.
 
#Mayor Quimby, umesikiliza hii habari uliyoiweka hapo vizuri?!

Mbona nakufahamu kwamba una akili vizuri tu.

Kweli umeshindwa kuelewa kinachozungumzwa hapo!

Nasikitika sana, mie nilikufahamu kama mtu unayeweza kuelewa hata habari tu , achilia mbali uchambuzi.

Habari ni tofauti kabisa na hii issue ya akina Mwabukusi.

Anyway una lengo lako.

Mbona zinaendana mkuu..ongeza upeo wa kufikiria utaeza chambua mambo kwa kina
 
#Mayor Quimby, umesikiliza hii habari uliyoiweka hapo vizuri?!

Mbona nakufahamu kwamba una akili vizuri tu.

Kweli umeshindwa kuelewa kinachozungumzwa hapo!

Nasikitika sana, mie nilikufahamu kama mtu unayeweza kuelewa hata habari tu , achilia mbali uchambuzi.

Habari ni tofauti kabisa na hii issue ya akina Mwabukusi.

Anyway una lengo lako.
DF40537D-F554-47CC-9919-2CD9F307ACF0.jpeg



Kuna source nyingi za hicho kifo cha jamaa.

Kikubwa ni frustration zake kuhusu uongozi wa Biden.

Alianza mikwara muda kwenye social media, sema anaishi Utah so hawakuona hatari sana. Hila alishaitwa March kuhojiwa na kutakiwa kuacha vitisho vyake kwa raisi wa nchi.

Na kwa nchi za wenzetu baada ya hapo anakuwa chini ya radar movement zake wana-monitor.

Biden ana ziara ya Utah siku chache zijazo; jamaa kapiga picha unayoiona hapo juu kaposti kwenye social media eti anasafisha sniper yake kwa kazi aliyoisubiri, japo ajasema kazi gani.

FBI awajachukulia hiyo threat lightly, wameenda na arrest warranty; purukashani wameondoka na maisha yake.

Ni hivi vitisho kwa serikali sio jambo la busara, ni haki ya watu kupinga, kukosoa au kutokubaliana na maamuzi ya serikali.

Ukianza kutishia viongozi au nchi kutotawalika unanunua ugomvi na vyombo vya kulinda amani ya nchi; ndio maana uwezi kukuta mtu yeyote huko tunapodhani wana demokrasia iliyokamaa anauthubutu wa kutishia serikali kutoweza kuongoza.
 
Back
Top Bottom