Napingana na Dunia nzima, Kenya inaangamia!

Hata wewe ni typical Mwafrika, unataka kuprove kitu kwa Muzungu hkn kingine, kama ungewajali Wakenya hivyo angalau ungeguswa na gharama na fedha wanazopoteza kwa ujinga tu, fedha ambayo wangewekeza kwenye ustawi wa jamii yao!
Sio kuprove kwa muzungu bali kama kuiga demokrasia ni kuukumbatia uzungu, kwanini tusingeendelea na kingship regimes za kiafrika kuliko kuikimbia haki kwa kisingizio cha gharama.
Kumbuka Kenya ni taifa la kibepari tangu enzi na sifa kuu ya mabepari ni demokrasia si kama sisi na ujamaa wetu tunaoendelea kukumbatia mfumo wa chama kimoja kwa maigizo ya chaguzi kandamizi.
CHEAP IS EXPENSIVE young man. Usipende sana slope. Kwa Karne hii hukupaswa kuwa na mawazo mgando kiasi hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kwakweli wewe ni msomi nimekukubali na uchumi wao utashuka sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeandika hoja vizuri na nimekuelewa lakini we unaona sawa ugandamizaji wa democracy?
 
Huyu mwana lumumba Pure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Where when did you learn upuuzi huu? Twisted ehh?
 
Viongozi wa africa wanachojali ni maslahi yao na si maslahi ya TAIFA....ila NATABIRI VURUGU ZITATOKEA HAPO..ni BORA UHURU aendelee na USHINDI KTK MARUDIO HAYO YA UCHAGUZI....lakini AKIJA KUSHINDA RAILA nae pia hatokubali hapo ndy shida itakapoanza.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Demokrasia ina gharama kubwa, sio cheap-Prof Haroub Othman (RIP) nyinyi endeleeni kutuburuza Kaka ila Wajukuu zenu watakuja kufukua makaburi yenu ili wapime DNA kama kweli mlikua mna uhusiano nao!

Sidhani kama watapima DNA kujua kama tulikuwa tuna uhusiano nao Bali watapima DNA kutaka kujua tuli relate zaidi na mnyama yupi ki akili sorry to say that.
 
Hata wewe ni typical Mwafrika, unataka kuprove kitu kwa Muzungu hkn kingine, kama ungewajali Wakenya hivyo angalau ungeguswa na gharama na fedha wanazopoteza kwa ujinga tu, fedha ambayo wangewekeza kwenye ustawi wa jamii yao!
Kwa hiyo ww unaona hapo ni mzungu anaye ridhishwa?

Vipi kuhusu msanduku ya kura na karatasi zilizokwenda kutupwa?

Hivi na ww kama mwafrika ulivyo ona makinikia wanayashkilia kwann hukutoa ushauri huu kwasabb itaingiza taifa kwenye deni kubwa? Na pesa hizo zingekwenda kusupply dawa Hosp ?

Vipi kuhusu bombadia mbona hukushauri?

Vipi kuhusu Zanzibar mbona hukushauri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I thought observers wote wazungu ndo walisema uchaguzi ulikua huru na sawa ,
Sasa unasema tunajiprove kwa wazungu

2013 wazungu walisema kenya wasimchague Uhuru juu ya kesi za ICC ,mabalozi wengine wakitamka wazi kwamba hawamtaki Uhuru
Hadi Balozi wa uingereza alitamka "choices have consequences "
 
Sina kuchangia endelea kupingana na dunia nzima kwa hoja zako hizi za ovyo kabisa yaani kama vile hujui maana ta mahakama kwa kuwa tu umezoea uchaguzi wetu hata kama taratibu zikikiukwa akitamka Lubuva na yule mpuuzi wa Zenji baaasi nuna kwa miaka mitano kusubiri uchaguzi mwingine!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachoamini mimi ni kua bado Kenyata atakwenda Ikulu

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
...Kumbuka Kenya ni taifa la kibepari tangu enzi na sifa kuu ya mabepari ni demokrasia...
Hakuna cha ubepari wala nini, sema tu wakenya wamejifunza baada ya kucharangana mapanga 2007. Uhuru naye kajirudi baada ya kuponea chupuchupu ICC.
 
Hata wewe ni typical Mwafrika, unataka kuprove kitu kwa Muzungu hkn kingine, kama ungewajali Wakenya hivyo angalau ungeguswa na gharama na fedha wanazopoteza kwa ujinga tu, fedha ambayo wangewekeza kwenye ustawi wa jamii yao!
Mkuu kwahiyo wewe kwako fedha inathamani kuliko uhai wa wanadam?/kumbuka kilichotokea Kenya 2007 kama na kilitokea vile kwa sababu hakukuwa na katiba iliyo bora,ila sasa wamerekebisha na ndio maana umeyaona hayo yaliyotukia.Fedha makaratasa hasara roho bana we vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe ni typical Mwafrika, unataka kuprove kitu kwa Muzungu hkn kingine, kama ungewajali Wakenya hivyo angalau ungeguswa na gharama na fedha wanazopoteza kwa ujinga tu, fedha ambayo wangewekeza kwenye ustawi wa jamii yao!
Hapa Kenya watu wengi wameuawa kwa sababu ya demokrasia. Na bado Wakenya wengi wako tayari kukufa Ili tu wailinde demokrasia. Wewe unaona kama hio ni ujinga, sisi tunaona demokrasia ni muhimu sana. Halafu mambo ya pesa isikusumbue akili kwani Kenya sio nchi masikini. Tutapata pesa virahisi tu wewe kaa kitako ungoje miezi miwili tuone kama Kenya haitapata hio pesa unayolialia hapa kuhusu.
 


Na ndiyo maana ukisoma utaona kuna kahali nimesema kwenye masikini kama hizi zetu huwezi kuwa na 100% free and fair election hata ufanye nini ni lazima kutakuwa na matukio kama hayo, sasa kama kila mtu akikata rufaa utarudi chaguzi ngapi? Kuna sababu kwa nini hata Wazungu wenyewe wkt wanatawla Afrika hawakuruhusu huu ujinga!

Nimesoma mahali Uchaguzi wa Kenya umegharimu 0.5 billion US dollars sasa baada ya miezi mitatu wanatumia tena kiasi hichi hicho cha fedha, hii ni fedha nyingi sana kwenye nchi ambayo hata chakula watu hawana!
 


Sasa kama hauna cha kuchangia mbona tayari umechangia?
 


Swala siyo kupata pesa, najua pesa ipo lkn swala ni unaitumiaje hiyo pesa? Kenya watu hata Ugali wanashindwa kupata, unajua Ugali ni chakula simple kkl vyote Duniani yaani ni maji tu hakuna mafuta, chumvi wala kiungo chochote kile yaani ukiondoa matunda ya porini hakuna chakula simple kama hicho lkn bado watu hawawezi kumudu na wanakufa halfu hiyo nchi inatumia 1 billion USD ndani ya miezi 3 kufanya uchaguzi ambao hata hivyo matokeo yanajulikana, huo ni UJINGA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…