Napingana na Dunia nzima, Kenya inaangamia!

Napingana na Dunia nzima, Kenya inaangamia!

Hivi tangu lini mmeanza kuwaza gharama Ungekuwa hata na busara kidogo tu ungeanza kumsumbua na kumlaani mwenyekiti wenu aangalie zile gaharama zilizotumika kwenye mchakato wa katiba mpya lakin chama anachokiongoza kimeamua kuteka mchakato, pia uchaguzi wa Zanzibar, marudia yale kwako haikuwa gharama kwasababu CCM walikuwa wanatafuta unachokitaka ila kwa Kenya ni gharama. Unataka Uhuru amfikirie raia wa Kibera ila CCM wao wasimfikirie yule raia wa Mto pepo, Jumbi etc....haya ni maajabu ya karne.
Ugonjwa mkubwa unaolisumbua taifa hili ni unafiki wa CCM, kama Mungu atatausaidia kuwaangamiza CCM nakuhakikishia taifa hili litapiga hatua mapema, ukitaka kujua hebu rudi nyuma kwenye kampeni za awamu hii halafu ujiulize ile mikwara yote ile kuhusu maendeleo mpaka leo tumeishia kuhangaishana na Tundu Lisu na kuweka watu mahabusu tu?
 
Wewe umesema waafrika wote wanashangilia, na tena unasema wanataka kuwafurahisha wazungu,, kiujumla wazungu na waafrika wamefurahi,, sasa wewe usiyetaka kufuata mkumbo uko kundi gani?,,

Sent using Jamii Forums mobile app
Usihangaike na mtu aliyekabidhi kila kitu. Maamuzi yote yako kwenye remote.

ACHA nikae KIMYA...!
 
Yanakuhusu? Nyie endeleeni kudhulumu wapumbavu na malofa kama mnavyowaita. Ya Kenya yako level nyingine kabisa.

ACHA nikae KIMYA...!

Kama ulitaka kukaa Kimya haukuwa na na haja ya kuandika ulivyoandika!
 
Hivi tangu lini mmeanza kuwaza gharama Ungekuwa hata na busara kidogo tu ungeanza kumsumbua na kumlaani mwenyekiti wenu aangalie zile gaharama zilizotumika kwenye mchakato wa katiba mpya lakin chama anachokiongoza kimeamua kuteka mchakato, pia uchaguzi wa Zanzibar, marudia yale kwako haikuwa gharama kwasababu CCM walikuwa wanatafuta unachokitaka ila kwa Kenya ni gharama. Unataka Uhuru amfikirie raia wa Kibera ila CCM wao wasimfikirie yule raia wa Mto pepo, Jumbi etc....haya ni maajabu ya karne.
Ugonjwa mkubwa unaolisumbua taifa hili ni unafiki wa CCM, kama Mungu atatausaidia kuwaangamiza CCM nakuhakikishia taifa hili litapiga hatua mapema, ukitaka kujua hebu rudi nyuma kwenye kampeni za awamu hii halafu ujiulize ile mikwara yote ile kuhusu maendeleo mpaka leo tumeishia kuhangaishana na Tundu Lisu na kuweka watu mahabusu tu?

Hilo binafsi nililipinga sana lkn sina uwezo wa kubadilisha chochote zaidi ya kupinga kama ninavyofanya sasa hivi, hata sisi tulipoteza fedha nyingi kwenye huu ujinga wa Katiba ile fedha tungeiwekeza kwenye Elimu ya watu watu ingetusogeza mbele, fikiria hata tu tungerudisha Elimu ya watu wazima kwa kutumia ile fedha ingesaidia watu wangapi nchi hii?
Isitoshe mimi sina Mwenyekiti yoyote yule, mimi ni mimi najiongoza siongozwi, na ndiyo maana maoni na mawazo yangu yako tofauti na Mainstream!
 
Waafrika kwa kusifiana ujinga tuko vizuri. Hakuna uchaguzi huru na wa haki duniani kwani lazima % fulani ipoteze na haitafurahi hata kama ni 10% tu. Hata maamuzi ya halali kama ya Mungu huwa hayampendezi kila mtu sembuse ya watu! As for Kenyan ninachoona ni uroho wa madaraka tu,kwani Raila akishindwa tena atamshika mkono Uhuru amwambie hongera,sidhani.Uharibifu wa rasilimali na muda tu kwa tamaa za wachache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada ebu jifunze kuficha ufinyu wako wa kuelewa mambo. Hivi unafikiria walifanya maamuzi huo hawakujua mambo ya gharama.Haki itendeke pale inapoonekana kuna dhuluma ktk haki gharama yoyote itumike ili haki irudi.Kenya ilo vizuri ktk legal system.Au unafikiria Kenya ina kaimu Jaji mkuu?.......Wakenya watabaki kuwa wa mfano kwa mambo mengi sana kwa Nchi za EAC,Kiuchumi,kisiasa,Demokrasia,na uhuru wa mahakama.
 
Hilo binafsi nililipinga sana lkn sina uwezo wa kubadilisha chochote zaidi ya kupinga kama ninavyofanya sasa hivi, hata sisi tulipoteza fedha nyingi kwenye huu ujinga wa Katiba ile fedha tungeiwekeza kwenye Elimu ya watu watu ingetusogeza mbele, fikiria hata tu tungerudisha Elimu ya watu wazima kwa kutumia ile fedha ingesaidia watu wangapi nchi hii?
Isitoshe mimi sina Mwenyekiti yoyote yule, mimi ni mimi najiongoza siongozwi, na ndiyo maana maoni na mawazo yangu yako tofauti na Mainstream!
Kama wafuasi wote wataonyesha kupinga na kuhoji kama unavyofanya wewe basi hata huyo mwenyekiti atakuja siku upiga magoti aombe radhi kwa uharamia unaofanywa na chama chake, tatizo linakuja waliotumwa kusema ndio na kushangilia kila kitu wapo wengi na akili zipo kwenye kabati la mwenyekiti wao wamebakia na mafuvu tu.
Mnapokemea ya Kenya mkumbuke kutoa mifano ya mambo ya kijinga yanayofanywa barani Afrika mengi yapoTanzania huko mkirejea uchaguzi wa Zanzibar na mchakato wa katiba mpya, nafikir maandiko yenu yatasadia sana kuwakumbusha mnaotaka wakumbuke.
Hata hili la kuzuia mikutano ya wapinzani na kamatakamata mkumbusheni mwenyekiti wenu kuwa sio kipaumbele chenu na halikuwepo kwenye ILANI yenu sasa yeye anatekeleza ilani ipi, na mumbieni amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuzuia ila mbona viwanda vimechelewa sana na maendeleo ambayo ndio yapo kwenye ilani bado vinasuasua? Nakuhakikishia mkiamua kumuambia ukweli bila kuogopa nchi hii itakuwa mbali kama anavyoota iwe.
Kenya wamejaribu na wameweza kuwadhibiti viongozi ila kwetu ni SIPANGIWI, SIJARIBIWI, NIMECHUKUA FOMU MWENYEWE, MIMI NDIO MIMI, NIMESEMA....nafsi ya kwanza umoja kila kona ila pamoja na hayo yote bado viwanda bado ni wimbo.
Hebu CCM tusaidieni kuusema ukweli na kukosoa kama mnavoweza kuwakosoa WAKENYA kwani hawa watu baada ya miaka isiyozidi 10 watakuwa vijijini kwao huko wakifuga kuku huku nchi inaendelea, kwahiyo hata wakiwachukia leo na hata kuwafukuza kazi kwenye vitengo vyenu vya ajira za chama (RC, DC,WAKURUGENZI, MAKATIBU, MAAFISA UTUMISHI na TAWALA etc) baada ya miaka yao ya kutawala na kuishi mjini watawaachia na mtazipata tena kwa haki na usawa bila kuwapigia magoti.
 
Mimi sifwati mkumbo, najua kinachowasumbua Waafrika wengi ni inferiority complex, Mwafrika anafanya jambo ili asifiwe na Muzungu na kamwe hafanyi kwa manufaa yake na watu wake, ukiangalia Waafrika wote wanashangilia Umafia uliofanywa na Mahakama ya Kenya kwa sababu wanataka kuprove kwa Muzungu kwamba nao pia ni Binadamu kwa kigezo cha Muzungu na Raila Odinga kwenye hotuba yake ni kama vile uamuzi huu ni kwa ajili ya kuprove kwa Muzungu kwamba sisi (Waafrika) hatuko wanavyotufikiria!

Kwangu mimi Katiba ya Kenya ni mzigo kwa nchi hiyo, fikiria wanakwenda kufanya Uchaguzi mwingine ndani ya Miezi 3, nani analipia hiyo gharama? Nchi ya Kenya hata chakula kwa watu wake ni shida kwa nini wasiwekeze hiyo fedha hata kwenye Kilimo? I mean matokeo hayatakuwa tofauti Wakikuyu 100% watampigia Uhuru Kenya, sasa kwa nini kupoteza fedha?
Ikumbukwe huyo Raila Odinga alisema ,,this time we will not go to court" na akaendelea kusema haiwezekani Matakwa ya Wakenya yaamuliwe na watu 7 akimasnisha Mahakama, lkn leo hii anasimama na kujigamba kwamba Mahakama ya Kenya imemuonyesha Muzungu kwamba inaweza kutoa haki kwa sababu tu imeamua alivyotaka yeye, vp khs sasa Mamilioni ya Wakenya waliomchagua Uhuru Kenya? Mbona wao wamenyimwa haki yao na watu 7 tu?

Isitoshe kwenye Nchi masikini kama Kenya haiwezekani kuwa na free and fair election kwa 100% ni lazima kutakuwa na matatizo tu, hata huo uchaguzi wa marudio kama Raila Odinga akishindwa na itatokea hivyo hatokubali atarudi Mahakamani tena na ushahidi mwingine ambao ni rahisi kuupata na kuita Uchaguzi mwingine tena, na Je watarudia chaguzi ngapi? Na nani atalipia hiyo gharama?

Of course kwa Muzungu ni win -win situation kwani anapata tenda za kusupply kila kitu kuanzia karatasi za kupigia kura mpaka computer!

Hivyo kwa maoni yangu sijaona chochote cha kufurahia wala kujifunza isipokuwa tu ni Blackman trying to prove his worthy to a Whiteman, hkn kingine, hata hotuba ya Raila Odinga baada ya Uamuzi wa Mahakama mlengwa hakuwa Mkenya wa Kibera bali ni International community aka Muzungu!

Fikiria nchi yote imesimama mwaka mzima kufanya uchaguzi usiokwisha, Nairobi stock exchange imesimama, sasa wanaanza Kampeni tena hivyo hkn kazi mpaka 2018, nani analipia hii gharama?

Kenya hali siyo shwari kama mnavyodhania, ndiyo Muzungu atasifu lkn kuna wimbi kubwa la tsunami linakuja upande wenu, Muzungu alitawala Afrika hakuruhusu hiyo Demokrasia mnayojaribu kumridhisha nayo na kulikuwa na sababu kwa nini hakuruhusu huu ujinga kwani maadamu watu bado ni masikini hata mahitaji ya lazima kama chakula hakuna huwezi kuwa na demokrasia, Muzungu anajua kwamba ,,a hungry man is not a from man" , ...
Angalau sisi tuna katiba Mpya tuliyoiandika wenyewe, wewe hapo ulipo mnaongozwa na kaiba na sheria zilizoandikwa na mkoloni!
 
Kama wafuasi wote wataonyesha kupinga na kuhoji kama unavyofanya wewe basi hata huyo mwenyekiti atakuja siku upiga magoti aombe radhi kwa uharamia unaofanywa na chama chake, tatizo linakuja waliotumwa kusema ndio na kushangilia kila kitu wapo wengi na akili zipo kwenye kabati la mwenyekiti wao wamebakia na mafuvu tu.
Mnapokemea ya Kenya mkumbuke kutoa mifano ya mambo ya kijinga yanayofanywa barani Afrika mengi yapoTanzania huko mkirejea uchaguzi wa Zanzibar na mchakato wa katiba mpya, nafikir maandiko yenu yatasadia sana kuwakumbusha mnaotaka wakumbuke.
Hata hili la kuzuia mikutano ya wapinzani na kamatakamata mkumbusheni mwenyekiti wenu kuwa sio kipaumbele chenu na halikuwepo kwenye ILANI yenu sasa yeye anatekeleza ilani ipi, na mumbieni amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuzuia ila mbona viwanda vimechelewa sana na maendeleo ambayo ndio yapo kwenye ilani bado vinasuasua? Nakuhakikishia mkiamua kumuambia ukweli bila kuogopa nchi hii itakuwa mbali kama anavyoota iwe.
Kenya wamejaribu na wameweza kuwadhibiti viongozi ila kwetu ni SIPANGIWI, SIJARIBIWI, NIMECHUKUA FOMU MWENYEWE, MIMI NDIO MIMI, NIMESEMA....nafsi ya kwanza umoja kila kona ila pamoja na hayo yote bado viwanda bado ni wimbo.
Hebu CCM tusaidieni kuusema ukweli na kukosoa kama mnavoweza kuwakosoa WAKENYA kwani hawa watu baada ya miaka isiyozidi 10 watakuwa vijijini kwao huko wakifuga kuku huku nchi inaendelea, kwahiyo hata wakiwachukia leo na hata kuwafukuza kazi kwenye vitengo vyenu vya ajira za chama (RC, DC,WAKURUGENZI, MAKATIBU, MAAFISA UTUMISHI na TAWALA etc) baada ya miaka yao ya kutawala na kuishi mjini watawaachia na mtazipata tena kwa haki na usawa bila kuwapigia magoti.

Nimekwisha sema sina Mwenyekiti yoyote yule Dunia hii, Mimi ni Mimi na ninajiongoza!
 
Angalau sisi tuna katiba Moya tuliyoiandika wenyewe, wewe hapo ulipo mnaongozwa na kaiba na sheria zilizoandikwa na mkoloni!

Hapana Katiba ya Tanzania haijaandikwa na Mkoloni, bali iliandikwa mwaka 1977 kama sikosei sina uhakika na mwaka lkn nina Uhakika haikuandikwa na Mkoloni!
 
Hapana Katiba ya Tanzania haijaandikwa na Mkoloni, bali iliandikwa mwaka 1977 kama sikosei sina uhakika na mwaka lkn nina Uhakika haikuandikwa na Mkoloni!
Basi pia sisi tunayetu mpya tunayoifywata.

Alfu kujibu swali lako la gharama, Katiba yetu iko wazi na pia very robust kabisa kuhusu mambo ya uchaguzi.
Uchaguzi ukifanyika LAZIMA majibu yatangazwe chini ya siku saba.
*kama hakuna mshindi amepata zaidi ya 50+1% uchaguzi unafanywa run-off ya mgombea wa kwanza na wapili, huo ichaguzi mpya unafanywa baada ya siku 14.
*kama kuna mgombea hakuridhishwa (kama ilivyo fanyika uchaguzi huu) basi ako na siku saba kufikisha kesi mahakamani, na mahakama iko na siku 14 kusikiza na kuamua kesi.
*kama kesi itaanguka basi rais mpya aapishwe baada ya wiki mbili mahali wazi (public place) .
*kama kesi itashinda, basi uchaguzi mpya ifanyike baada ya siku 60..

---Tume ya uchaguzi ikiwa inapiga bajeti mwezi march, huwa wanapewa pesa za gharama yote ya uchaguzi hata ya kufanya run-off , yani pesa wanazo pewa zina account for all scenarios ili kusikue na constitutional crisis ambapo tume haina pesa za kutosha na hakuna mtu anaruhusa kwenda wizara ya fedha kutoa pesa nyingine wakati wabunge bado hawajafungua bunge rasmi. Kawaida huwa serekali mpya ikiingia iebc inaregesha zile pesa extra walizopewa kufanya re-run ili zitumike kwa mambo mengine na wizara ya fedha
 
Hapana Katiba ya Tanzania haijaandikwa na Mkoloni, bali iliandikwa mwaka 1977 kama sikosei sina uhakika na mwaka lkn nina Uhakika haikuandikwa na Mkoloni!
Sawa, Tanzania ni nchi nzuri iliyo na maendeleo na Kenya ni nchi mbaya isiyo na maendeleo. Hivyo ndio unataka kusikia sivyo? Sasa Umefurahi?
 
Basi pia sisi tunayetu mpya tunayoifywata.

Alfu kujibu swali lako la gharama, Katiba yetu iko wazi na pia very robust kabisa kuhusu mambo ya uchaguzi

Ni chaguzi ngapi Kenya inaweza kumudu kufanya? Tuseme kila atakayeshindwa aendelee kukataa na kukimbilia Mahakamani na Mahakama ifute Uchaguzi?
 
Sawa, Tanzania ni nchi nzuri iliyo na maendeleo na Kenya ni nchi mbaya isiyo na maendeleo. Hivyo ndio unataka kusikia sivyo? Sasa Umefurahi?

Kenya ilipaswa iwe mbali sana zaidi ya ilipo sasa hivi kwani Kenya haijawahi kuwa socialist country kama Tanzania, Kenya inafwata capitalistic system tangu siku ya kuanzishwa kwake, hivyo Kiuchumi ilipaswa iwe kwenye ligi ya akina Malaysia, Hong Kong na Taiwani huko, siyo hapa leo hii kukimbizana na kugombania Ugali na akina Uganda au Rwanda!
 
1. Gharama zinabebwa na vyama husika siyo taifa.

2. No one is above the law.

3. Ni bora kurudia uchaguzi kuliko kumwaga tena damu za wakenya.

4. Sheria ndo zimeamua na wala siyo maamuzi ya watu 7! Ingekuwa ni maamuzi ya watu tu basi Uhuru asingekubali.

Kinachowauma ni kuona jinsi Kenyatta anavyozidi kung'ara mbele za haki kwa kutii na kuheshimu katiba ya nchi. Akili yako haijafikia uwezo wa kuelewa yanayoendelea Kenya. You are still primitive. May be after 200 yrs you may have evolved to that level of understanding. Evolution is the gradual process and the biggest evolution is the evolution of brain. Your brain is still at Homo erectus level while other people's brain are involving to homo superior

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe ni typical Mwafrika, unataka kuprove kitu kwa Muzungu hkn kingine, kama ungewajali Wakenya hivyo angalau ungeguswa na gharama na fedha wanazopoteza kwa ujinga tu, fedha ambayo wangewekeza kwenye ustawi wa jamii yao!
Mbona gharama zinazotumiwa na serikali kuwanunua akina Lipumba na kuwalinda hazikuumi? You are a coward and hypocrite

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom