Napitia wakati mgumu mno kufanya maamuzi ya ujenzi

Kishoka1

Member
Joined
Apr 27, 2024
Posts
8
Reaction score
54
Ndugu wana Jf mimi ni kijana hizi nyumba za kupqnga zimenichosha, kutwa kelele za kugombezwa na mama mwenye nyumba mbele ya wanangu wawili ni fedheha. Nimejipigapiga nimeuza maeneo ya urithi ili angalau nijistili na familia yangu Sasa changamoto mimi ni mgeni wa masuala ya ujenzi..nimeleta uzi huu kuomba kwenu ushauri na makadirio ya ujenzi kwa ramani yangu hii ambayo imeambatana na post yangu, Naomba kujua hesabu ya tofali, cement, mchanga pamoja na idadi ya bati itakayotumika mpaka nyumba yangu ikamilike.

NB, Eneo ninalotaka kujenga ni tambarare0 Asanteni.0
 
Ukijenga box kama hili lazima uweke jiko na dinning room. Na kwa nini ujenge box, uuze ardhi ya urithi ndiyo ujenge au huna kamba weye?
 
Ndugu yangu.
Mchoro wako hauna vipimo.
Malizana na mchora ramani akupe mchoro uliokamilika ili tuweze kukusaidia kwa usahihi zaidi.
Nikutakie maandalizi mema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…