Napitia wakati mgumu

Napitia wakati mgumu

Baby Nana

Member
Joined
Jan 3, 2025
Posts
27
Reaction score
52
Wakuu habari zenu wakuu naomba ni share hali yangu japo nipate hata faraja maana naona naweza kupata ugonjwa wa moyo siku siyo nyingi mimi ni binti wa miaka 25

Mwaka 2017 nikiwa kidato cha nne niliugua ugonjwa wa ajabu sana miguu ilikuwa inawaka moto na kuhisi baridi sana muda wote pamoja na kufaganzi maumivu yalikuwa makali sana mpaka nashindwa kutembea. Mgongo wangu ulianza kuuma nikawa nakosa balance kati ya kiuno na mgongo naweza kukaa kwenye kiti nikawewesuka nikaanguka chini.

Pia masikio yangu yalianza kuuma na kuhisi kelele muda wote hali hii ilipelekea kuwa kiziwi nikiingia darasani sioni hata nikivaa miwani naona moshi tu au ukungu.

Nimeangahika sana kutafuta tiba kila napoenda naambiwa mambo mengi sana ikiwemo kurogwa hata maombi nimeenda sana. Hospitali nilipima vipimo karibia vyote ikiwemo CT-SCAN na kipimo cha uti wa mgongo walikosa ugonjwa.

Miaka mitatu nilisoma kwa shida sana. Hali hii inanifanya niwe mpweke najitenga na kuhisi hasira sana hata vitu vidogovidogo yaani hata mtu akiniambia nakupenda naona kama ananidhihaki 😞.

Kilichonileta huku ni kwamba..kwa maumivu ninayo kuwa nahisi nashindwa kufanya kazi ngumu na kutembea umbali mrefu alafu nakuwa naanguka anguka mtu aweza kuzani nakifafa kumbe Lah!.
Sasa nawaza nitafanya biashara gani wakati siskii vizuri na kutembea kwangu ni kwa shida.

Nikisema niombe kazi ni nani ata niajili na huku siskii vizuri na elimu yangu ni kidato cha sita nilishindwa kuendelea na masomo ya ngazi za juu kwasababu ya hali yangu kwani uchumi wetu ni wa kawaida hivyo pesa nyingi inahitajika kwa matunzo.

Jamani ikiwa kuna mtu amewahi kupitia kipindi kigumu kama hiki naomba anisaidie aliponaje ni dawa gani alitumia, malalamiko ni mengi kuwa sifanyi kazi sana na wakati wanaona kabisa sina nguvu halafu napata shida sana kila kitu mpaka niombe nasemwa naringa ni mjeuri nikisemeshwa najizima data wakati sisikii kuna muda mpaka najichukia naona sifai.

Mwaka jana nimepata kazi shule moja ( nipunguza kuanguka angalau natembea) ndo mpaka sasa nipo hapo nafundisha watoto nashukuru Mungu nimeweza uwezo wangu angalau nimeuona japo pesa nayo pata ni kidogo lakini angalau nina amani naweza kujinunulia mafuta hata vocha sema kitu kinacho niumiza kichwa Kuna muda nakubali kuwa hii hali ni yangu umekuwa ulemavu lakini MOYO unakataa kuwa sitakiwi kuwa hivi miaka nane sasa nateseka 😥😥😥 napenda niwe na kwangu nifanye mambo na familia kwa pesa nayo pata kufanya maendeleo itachukua muda sana.

Naomba ushauri wowote iwe dawa au lishe au hata mawazo ya biashara kuna muda akili inasimama kabisa haifanyi kazi 😔😔😔
 
Mmmmh mbona story zinaendana karibia 96% na mschana mmoja anaitwa Merry? sio wewe kweli tulikutana fb baada ya muda fln ukaniambia hali yako na ukaomba hela nikakwambia hela sina kama unahitaji msaada njoo geita ama tukukane kamanga hospital kwa Dr wa masikio gharama nitatoa mimi.

Baada ya kukuambia vile ulinipa sharti nije kwanza kwenu wanijue ...............kwa kifupi ulianza ujanja ujanja kama sio wewe nisamehe ila kisa chako kinaendana sana matukio uliyosema kilichotofautiana tu ni macho,kukoswa nguvu na kuanguka basi.Lakini kujitolea ualimu sawa na ulisema ni fundi cherehani na tatizo la msakio tangu ukiwa olevel.
Mkuu siyo mimi
 
Lakini mkuu hilo shart alilokupa ni kwa ajili ya usalama wake sioni kama ni ujanjaujanja au labda kama kuna mengine hukuyaweka wazi
 
Kama ni mroma na una amini Funga na kuSali Novena ya My.Ritha wa kashia ( Novena ya mambo yaliyoshindikana )...
Nasisitiza tena,. Kama unaamini

Lamomy Labella nakumbuka wakati unanielekeza siku ya kwanza sikuwa na amini,. Lakini kwa Juhudi za madaktari na Nguvu ya novena hii nilipona kabisa,. Ubarikiwe sana Jirani
 
Kama ni mroma na una amini Funga na kuSali Novena ya My.Ritha wa kasia ( Novena ya mambo yaliyoshindikana )...
Nasisitiza tena,. Kama unaamini

Lamomy Labella nakumbuka wakati unanielekeza siku ya kwanza sikuwa na amini,. Lakini kwa Juhudi za madaktari na Nguvu ya novena hii nilipona kabisa,. Ubarikiwe sana Jirani
Naomba unisaidie hiyo novena kama hutochali
 
Wakuu habari zenu wakuu naomba ni share hali yangu japo nipate hata faraja maana naona naweza kupata ugonjwa wa moyo siku siyo nyingi mimi ni binti wa miaka 25

Mwaka 2017 nikiwa kidato cha nne niliugua ugonjwa wa ajabu sana miguu ilikuwa inawaka moto na kuhisi baridi sana muda wote pamoja na kufaganzi maumivu yalikuwa makali sana mpaka nashindwa kutembea. Mgongo wangu ulianza kuuma nikawa nakosa balance kati ya kiuno na mgongo naweza kukaa kwenye kiti nikawewesuka nikaanguka chini.

Pia masikio yangu yalianza kuuma na kuhisi kelele muda wote hali hii
Pole sana nenda hospitali kubwa kama Hindu mandal pale au Aga khan wanaeza saidia kujua chanzo cha tatizo

kingine kubali tu hali halisi focus na mambo mazuri yanayokupa amani ya moyo unaeza conquer anything ukijiamini ukaeka hio ‘mimi sisikii’ pembeni have your confidence and go you got this.

Pia usijitenge na watu jichanganye kwa wingi inasaidia kumbuka maisha ni watu

Kila la heri
 
Umetumia tiba ya mkojo wa Ahsubui.

Do it at least 1-7days

Naamini utapata goodfeedback

Ukipona najua utakuwa shuhuda mkubwa wa hii tiba.

Mimi nilikuwa na hali Kama hiyo ikiwemo kuumwa na kichwa kila siku Ila nimepona.
 
Pole sana nenda hospitali kubwa kama Hindu mandal pale au Aga khan wanaeza saidia kujua chanzo cha tatizo

kingine kubali tu hali halisi focus na mambo mazuri yanayokupa amani ya moyo unaeza conquer anything ukijiamini ukaeka hio ‘mimi sisikii’ pembeni have your confidence and go you got this.

Pia usijitenge na watu jichanganye kwa wingi inasaidia kumbuka maisha ni watu

Kila la heri
Ila hospitali kubwa nimeenda Bugando hizo nyingine siwezi gharama zao
 
Back
Top Bottom