Napoteza pesa bila kuelewa

Hamna cha chuma ulete wala mjomba chuma ulete,wewe mwenyewe unawatunuku wateja hela,Kingine kua makini na maburungutu mteja ameyafunga kwa mafungu laki laki,Katikati wanapachika 2000 humo so acha kabisa kuhesabu hela za wateja kwa style hii hapa chini utaumia kila iitwayo leo useme chuma ulete chuma ulete kumbe n uzembe wako..

Usitumie hiii style kwenye kuhesabu hela MARUFUKU tena ACHA KABISA 👇 👇




ukihesabu hela acha kabisa Hata kama wateja wamepanga foleni wasikuchanganye hao ndio wezi wapo humo humo so epuka hiyo style maana matokeo yake ukihesabu hivyo ndani wanakupachkia 2000 na si unajua buku mbili kama una wenge usipoiona nzma unaweza dhani ni 10 kumbe walaaaaaa ni kasimba ka 1 kamejificha ndan ya kundi la Tembo.




Huo ni mfanno👆👆👆 wenzako wanavyochanganyiwagwa mkwanja kwenye hayo maburungutu so kuwa makini sana kwa maelezo yako nina uhakika ushachezewa Rough mahali bila wewe kujitambua.


Unapohesabu hela uwe kama mtoto hesabu hela kama mshamba flani taratiiiibuuuu na polepole na kwa kujiamini,Mteja asikupe presha maana wateja wanaotaka kukutapeli huja kama wa nne dukani kwako kila mmoja akijifanya yuko peke ake,Mmoja atakupa maburungutu yenye noti za 200 ndani then mteja huyu atakua mstarabu sana,Then hao wenzake wa nyuma watatu watakupa presha OOOOH WE dada hesabu haraka oooh wee dada unatuweka foleni oooh this oooh that

Wasikuchanganye hao,hesabu hela zako taratbu tena ukiona wamezidi kelele acha kuhesabu waangalie Simama kabisa kuhesabu wambie kwa kujiamini "NAOMBA MNYAMAZE" ukiona huyo mteja aliyekupa hela yupo upande wao anawasapoti Mrudishie hela zake mwambie samahani Kaweke hela zako kwa wakala Yuleeeee.


Unapohesabu hela zako hesabu kwa style hiiii 👇👇



Hesabu noti Moja Moja iangalie kama ni nzima yote maana wanamtindo wakuweka vipisi vya elfu kumi kati kati,kuwa makini sana mkuuu,usipokutana na 2000 utakutana na vipisi vya elfu 10 kuwa makini so hesabu hela kama hapo juu ione noti nzima kisha ukijiridhisha hii LAKI weka pembeni chukua burungutu lingine.


Usihesabu hela unazopewa kwa kufungwa fungwa Kunjua noti zote zikae wima ndipo uanze ku count.
 
Kua kauzu usipende kucheka cheka wateja wasikuzoeee yani NUNA 24hrs wakuogope hadi akijifkiria kuja kukutapeli au kufanya ujinga aanze jiuliza yule jamaa sijawahi ona JINO lake leo hiii anidake nataka mtapeli si atanila na kachumbari!

yes uwe hivyo kucheka mpk X MASS ukauzu ndio ulinzi wa hiyo biashara yako
 
unawapa wewe mwenyewe wateja pesa TRUST ME
 
Hahahahaha umeandika lugha nzito ya kibabe ya biasharaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaha umeandika lugha nzito ya kibabe ya biasharaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna namna mkuu unafkiri utafanyaje,ukiwachekea kesho atakuletea NOTI feki na anajua hutoweza mfanya kitu maaana si mashost urafiki mwingi,ukimdaka atajichekesha huku anashangaa" haaaa jamani hiyo ni feki hata mmi siijui"

kumbe liongo likubwa lilikua linataka kukuliza kwasababu umemshtukia atajichekesha chekesha sasa dawa yao ni ukauza kwa kwenda mbele Unamuangalia mteja hadi anahisi kuna mtu nyuma yake unamuangalia kumbe mko wawili tu.
 
Hahaha uso mzito kama uji wa mhogo uliopoa. Lazima ajipange vizuri kukuibia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu kingine apo kwenye biashara yako huwa unatabia ya kuhudumia wateja uku unaongea na simu au kuna kigenge cha vijana huwa unauhudumia wateja uku ukiwa unapiga story na vijana wenzako???????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia majority ya comments katika uzi huu unaweza kuwaelewa vizuri watz na imani za kishirikina; wasomi, wasiosoma, washika dini, na wasiokuwa na dini wote tunaamini sana ushirikina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks much mkuu, great advice

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Hivi vituko vipo sana. Ushapigwa code mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio style yangu kwenye biashara nikiona wateja wamekaa kiwizi wizi natoa mimacho kama nimebanwa na mlango hadi akili inawakaa sawa
Sent by Diaspora
 
Hii ndio style yangu kwenye biashara nikiona wateja wamekaa kiwizi wizi natoa mimacho kama nimebanwa na mlango hadi akili inawakaa sawa

Sent by Diaspora
Kuna wakati wateja hawatakiwi kuelewa wewe una bandama au hauna

unawaacha hapo kati kati,hii style imenisaidia sana wateja wanaokopa kuniogopa

maana ni mtu nisiezoeleka,na wateja wakikuzoea tu "wanaanza kuku kopa" ila ukiwa kauzu

Akiwa hana hela au la maana ofisini anasepa yeye mwenyewe bila hata wewe kumfukuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…