Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Narudia tena, Usafiri wa daladala hapa Dar es Salaam ni kwa ajili ya watu masikini

Siyo kwa maskini, ni kwa ajili ya watu wanaohitaji kutumia usafiri wa daladala kwa wakati husika.....mfano wengine wana magari yao lakini wakati mwingine hutumia daladala kuepuka usumbufu wa kuendesha, maana kuendesha gari siyo rahisi kama mtoa mada unavyofikiria au kama wanapiga bajeti ya mafuta....
Usumbufu wa kuendesha?
Yaani unaona bora ubanwe kwenye daladala na kila aina ya kadhia kisa gari linakusumbua kuendesha?
 
Huo ndo ukweli.
Na ukiona eti una gari na umeshindwa kuweka mafuta ukaja kupanda daladala bado upo kundi lilelile tu. Mtu na pesa zako huwezi kubali kudhalilika na vurugu za daladala za dar aisee.

Mtu na ndambi yako na tai shingoni unapapambana kupata siti 😂😂, daah aisee.

Umaskini mbaya jama, tuukatae.
 
Usumbufu wa kuendesha?
Yaani unaona bora ubanwe kwenye daladala na kila aina ya kadhia kisa gari linakusumbua kuendesha?
Mkuu kwani wote wana mbanano kwenye daladala, wengine wanapandia mwanzo wa gari na hajawahi kupata usumbufu.....kujua adha ya kuendesha gari daily subiri ununue la kwako utaelewa tu. Ulishajiuliza kwa nini wengine wenye uwezo wanaajiri madereva, au unafikiri hawajui kuendesha...
 
Naunga Mkono Hoja! NAKAZIA kupanda Daladala ni Umasikini na hakuna anaye enjoy kupanda Daladala, tunapanda ili tufike tu! Haiwezekani eti Diamond apaki Rolls Royce aone usumbufu halafu apande Daladala [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]wote mnaompinga mtoa mada ni Masikini.

Nauchukia Umasikini

Nauchukia Umasikini

Nauchukia Umasikini

Hata kutumia Tecno au Infinix Pia ni Umasikini.. Goodnight EVERI BADI

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwani wote wana mbanano kwenye daladala, wengine wanapandia mwanzo wa gari na hajawahi kupata usumbufu.....kujua adha ya kuendesha gari daily subiri ununue la kwako utaelewa tu. Ulishajiuliza kwa nini wengine wenye uwezo wanaajiri madereva, au unafikiri hawajui kuendesha...
Sawa mkuu! Ngoja siku nikinunua gari ndiyo ntajua usumbufu wa kuendesha gari kila siku..
 
Habari wanajukwaa!
Natumaini hamjambo,
Hii sio kashfa bali ni ukweli mtupu. Usafiri wa daladala hapa Dar ni kwaajili ya maskini.
Vijana tutafute pesa huku tukimwomba Mungu atuepushe na Usafiri huu uliojaa karaha na kadhia.
Haiwekani mtu una pesa zako usimame Kariakoo mpaka Mbagara, au usimame Kariakoo mpaka Tegeta.
Jioni ukitoka mjini kwenda pembezoni mwa jiji unavizia basi la kugeuka nalo ili upate siti, nako ukishangaa hupati.
Makonda jioni wanaringa kama wasichana mabikira.
Watu wananuka sigara mnapumuliana.
Mwendokasi nako niliwahi kupanda jioni nako hali ni ngumu. Kuna mfanyakazi mwenzangu alikatwa kidole na mlango wa mwendokasi asubuhi wakati anakuja kazini.
ili kuweka uwiano sawa ungeanza kuelezea maana ya maskini na tajiri
 
.

Screenshot_20210720-001626_Google.jpg
 
Back
Top Bottom